2023.03.04 Papa na Kamati ya wahariri wa Kipindi cha televisheni  cha "A sua immagine" 2023.03.04 Papa na Kamati ya wahariri wa Kipindi cha televisheni cha "A sua immagine"  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa na Kamati ya 'A sua Immagine':Hifadhi mshangao wa neno hilo!

Baba Mtakatifu amewaomba wasiache maneno hayo yawe ya kawaida na kugeuka maneno ya hewani au kuyapunguzia katika neno lililondikwa kwenye Skrini.Badala yake ni kuhifadhi mshangao wa maneno hayo ili kuweza kuyawasilisha.Ni muhimu hasa katika mabadiliko ya wakati tunaoishi.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 4 Machi 2023, alikutana na wahariri wa vipindi vya televisheni  hasa kipiondi cha “Sua Immagine,” katoliki katika  Televisheni ya Italia (RAI) na kuwakaribisha huku akimshukuru Padre Gianni Epifani kwa maneno ya hotuba yake. Ni furaha yake kuwa na timu ya kipindi hicho cha “Sua Immaginenkwani  zaidi ya Bi Lorena Bianchetti mwendesha kipindi hicho, hata wasikiliza, waharri, mafundi na wale wote ambao wanashirikana katika kipindi hicho. Amepanua salamu zake hata kwa wale ambao waliwatangulia wakati uliopita. Kama wajuavyo Baba Mtakatifu amethibitisha anavyo fuatilia kipindi hicho mara kadhaa hata kama ni sehemu tu, kipindi chao ambacho kilizaliwa kwa ushirikiano kati ya RAI na Baraza la Maaskofu Italia.

Papa amekutana na Kamati ya wahariri wa kipindi cha Televisheni "A Sua Immagine"
Papa amekutana na Kamati ya wahariri wa kipindi cha Televisheni "A Sua Immagine"

Kiukweli muda wa Dominika unaaendena na ule wa kuchungulia kwake dirishani kwa ajili ya sala ya Malaika, kwa sababu Papa anapofika kwenye ukumbi wa kusubiri kabla ya kwenda kwenye sala anatazama kidogo baada ya  misa kuhitimishwa. Kwa hiyo kipindi hicho anapenda kufuatilia kwa dakika chache na wakati mwingine anapata hata hisia kubwa ambayo kwa namna ya pekee  inapogusa. Kwa maana hiyo amependa kuwapongeza kwa yule ambaye kwa miaka 26 alichagua jina la kipindi hicho “A Sua Immagine”,  yaani “ kwa mfano wa sura yake.” Haya ni maneno ambayo yanarejea mwanzoni mwa Kitabu cha Mwanzo, mahali ambapo Mungu alipo maliza kazi ya uumbaji alisema: “Tufanye mtu kwa sura na mfano wetu” (Mw1,26). Tumeumwa kwa Sura ya Mungu! Hatupaswi kuzoea tu kilelezo cha mfano huo, na wala tusiishe kushangazwa, kwa sababu katika kila mwanadamu wa Mungu kuna mwanga na kwa namna ya pekee   cheche moja ya nuru yake. Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kwamba “katika kila mtu, mzuri na mbaya, kila mtu, ni mfano wake na  wito wenu ni kutafuta asili ya mambo na kujikomboa kutoka katika utamaduni huu wa usawa”.

Papa akiwasalimu Kamatiya wahariri wa Kipindi cha Televisheni cha 'A sua Immagine'
Papa akiwasalimu Kamatiya wahariri wa Kipindi cha Televisheni cha 'A sua Immagine'

Baba Mtakatifu amewaomba wasiache maneno hayo yawe ya kawaidia na kugeuka maneno ya hewani au kuyapunguzia katika neno lililondikwa kwenye Skrini. Bali inahitaji kuhifadhi mshangao wa maneno hayo, ili kuweza kuyawasilisha. Ni muhimu. Mabadiliko ya wakati tunayoishi, yanatushuhudia tendo la kupotea, kwa upande wa watu wengi, hasa katika dhamiri ya kuwa watoto wa Mungu, walioumbwa kwa mfano wake. Kuna haja ya kuyaishi. Kwa sababu pale katika sura hiyo ndimo kuna asili na msingi usiopunguza hadhi ya mwanadamu; asili na msingi wa kuwa wote ni ndugu, kwa sababu tu wana wa Baba mmoja, wapendwa na walioumbwa kwa sura Yake. Kwa kwenda sana na maono haya, kipind chao kinawakilisha nyuso na historia za wanaume na wanawake wa nyakati zetu. Anafanya kwa namna ya pekee kwa kutoa sauti kwa yule hasiye kywa nayo, mdhaifu zaodo na anayeteseka; anafanya hivyo kwa kusimulia anayeishi Injili katika sehemu za mbali ya kijiografia na maisha ya Italia na Ulimwenguni; anafanya kwa kufungua madirisha, kuhusu hali halisi, na mahali ambapo mara nyingi hayaonekana na rada yam aoni ya umma. Kwa njia ya wageni na video zinazoshuhudia, kila dominika baada ya dominika, kwa utaratibu na bila kelele uzoefu mwingi wa maisha na wa huduma hufanyika.

Kamati ya Wahariri wa Kipindicha A sua Immagine
Kamati ya Wahariri wa Kipindicha A sua Immagine

Inatukumbusha kuwa kuna vijana wenye uwezo wa juhudi na kujitolea kwa wengine; kwa kuonesha hata majanga ya kibinadamu, lakini kwa njia za historia ambazo zinaturuhusu kuhifadhi uhai wa tumaini na ili kuweza kuacha kukumbatiwa na uzuri wa Injili iliyo hai. Baba Mtakatifu anawatia moyo wa kuendelea na njia hiyo. Kuna haja ya utawandawazi wa mshikamano na sio wa kutojali au sintofahamu. Kutangaza Injili maana yake ni kushuhudia kwa maisha yetu ambayo kuna Mungu wa huruma ambaye anatusubiri, anatutangulia na ambaye alitupenda na ambaye anatupenda. Na kwa kazi yao maalum, wanaweza kuchangia mengi kwa maana hiyo. Na katika suala hilo, Papa amewashukuru wao  na Rai kwa sababu wanasaidia kutoa mwangwi kwa wito  ambao, mara baada ya Sala ya Malaika au Malkia wa Mbigu, Papa anakuwa ameutoa kwa kaka na dada katika hali ngumu sana. Kwa hivyo wanawasaidia watazamaji wasiwasahau, kuwa karibu nao katika sala, msaada thabiti na kujitolea kila siku. Papa amerudia kuwashukuru kwa kazi yao na jinsi wanavyoifanya. Anawasindikiza kwa baraka zake, na amewabariki wao wote na wapendwa waonna wakati huo huo hakusahau kuwaomba ili wamwombee.

PAPA NA KAMATI YA KIPINDI CHA TELEVISHENI CHA A SUA IMMAGINE
04 March 2023, 17:55