Papa:Toeni msamaha kwa kila mtu!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameongoza maadhimisho ya ibada ya kitubio katika moyo wa Roma kwenye Parokia ya Mtakatifu Maria wa neema, huko Trinfalie jijini Roma katika fursa ya Mpango wa masaa 24 kwa ajili ya Bwana. Ni katika Kanisa la kisasa ambalo linahifadhi historia ya kale: sanamu ya miujiza ya Mama Maria akimnyonyesha Mwanae na ambayo kulingana na mapokeo ililetwa kutoka Nchi Takatifu na mchungaji wa mmoja wa Kieremiti wa Calabria nchini Italia. Katika kibao kuna picha yenye uso mzuri sana, iliyohifadhiwa kwa upendo katika parokia hiyo na binti na mrithi wa Kanisa kuu lililojenga juu ya jingine la kizamani, ambalo lilikuwa karibu na Eneo liitwalo Porta Angelica.
Katika mahubiri ya Papa Francisko akiongozwa na maneno ya Mtakatifu Paulo asemayo “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo”. (Fil 3,7). Papa amesema ndivyo Mtakatifu Paulo amethibitisha katika Somo la kwanza lililosomwa. Na ikiwa tunajiuliza ni mambo gani ambayo yalifikiriwa kuwa muhimu katika maisha yake hadi kuapoteza ili kupata yake ya Kristo, tutaona kuwa ni yake kihalisa ya vitu, lakini yenye utajiri kidini. Kiukweli alikuwa ni mwanaume wa ibada safi na shauku, mfalisayo na mshika torati (cfr vv. 5-6). Na kumbe nguo ya kidini ambayo angeweza kujijengea sifa, ubatili, utajiri kitakatifu, kiukweli ilikuwa ni kizuizi kwake. Kwa hiyo Paulo anathibitisha “Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo” (rej Fil 3,8).