Salamu za rambi rambi za Papa kwa kifo cha Kard Karl-Josef Rauber
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ametuma kwa Askofu Peter Kohlgraf, wa jimbo la Mainz, telegramu ya rambirambi kufiatia na kifo cha Kardinali Karl-Josef Rauber, aliyefariki tarehe 26 Machi. Katika telegramu hiyo Papa anabinisha kuwa: "Maisha yake ya kipadre na kiaskofu yalidhihirishwa hasa na utumishi wake kwa mrithi wa Petro", pia akimkumbuka Kadinali wa Ujerumani katika jitihada za "kujitolea kwake kwa umoja wa watu wa Mungu katika Curia Romana na katika sehemu mbalimbali za dunia kama wa balozi wa Vatican."
Mchungaji wa kweli wa Kanisa
Baba Mtakatifu aidha ammfafanua Kardinali Rauber kuwa "Kama mchungaji wa kweli wa Kanisa, katika kila ishara yake alijazwa na upendo wa Kristo ambayo ilimfanya asiiweke kwa ajili yake mwenyewe, bali kuipitisha bila kujibakiza na kwa furaha kwa wanadamu." Kwa njia hiyo maombi ya Papa Francisko ni kwamba marehemu Rauber sasa anaweza "kusifu milele upendo wa huruma ya Mkombozi".
Kufuatia na kifo cha Kardinali Karl-Josef Rauber, Baraza la Makardinali linaundwa sasa na makadinali 222, kati yao 123 ni wapiga kura na 99 sio wapiga kura.