Tafuta

2023.03.26 Shule ya Mafunzo kwa wanafunzi wa Chama cha Matendo ya  vijana Katoliki. 2023.03.26 Shule ya Mafunzo kwa wanafunzi wa Chama cha Matendo ya vijana Katoliki. 

Ujumbe wa Papa Francisko kwa wanafunzi wa Chama cha vijana katoliki Italia

Papa amewaelekeza Vijana wa Chama cha Matendo katoliki Italia,maneno ya kuwatia moyo kwa njia ya video uliorekodiwa 25 Machi,katika fursa ya Mkutano mjini Vatican na Msimamizi wa Kitaifa,Askofu Giuliodori.Papa aliwaeleza kuwa hawasahau na kuhimiza wakuze mazungumzo kati ya babu na bibi zao.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi asubuhi tarehe 25 Machi 2023 katika fursa ya Mkutano mjini Vatican na Askofu Claudio Giuliodori, Msimamizi Mkuu wa Chama cha Matendo Katoliki cha Vijana Italia (ACI) na Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, alirekodi ujumbe mfupi kwa njia ya video kwa ajili ya vijana. Katika ujumbe huo aliwasahauri wabadilishe hali halisi na kuwauliza ikiwa wanafanya hivyo. “Ninyi mna uwezo wa kubadili hali? Eh, muwe makini. Kuna ukweli mzuri, ambao hukufanya uende chini, unapokuwa kwenye obiti. Lakini kuna ukweli mbaya na hii lazima ibadilishwe,” alisema Papa. Kwa kufafanua alirejea katika aina ya ukweli maradufu ule mzuri ambao unakuleta duniani, katika mtazamo wa unyenyekevu na ule mbaya ambao badala yake unakuingiza kwenye hali  hasi, ambayo inapunguza mawazo ya kawaida na kubaki kusema, daima imekuwa ikifanya hivyo. Suala hili Papa alithibitisha kuwa, lazima libadilishwe kwa sababu linafanya kuwa wafungwa

Askofu Claudio Giuliodori,Msimamizi Mkuu wa kikanisa wa Chuo Kikuu Katoliki na vijana Chama cha  Matendo ya Vijana katoliki
Askofu Claudio Giuliodori,Msimamizi Mkuu wa kikanisa wa Chuo Kikuu Katoliki na vijana Chama cha Matendo ya Vijana katoliki

Kwa maana hiyo vyama katoliki katika shule, lazima vigeuke kuwa mafundi wa amani, na wakuze daima mazungumzo kati ya vijana na wazee. Papa amewatia moyo vijana ambao, alirudia, kusema kwamba wanajua jinsi ya kufanya hivyo. Wakati mwingine ndoto ni zaidi. Lakini wanaweza! Na wana nguvu, vile vile wana udanganyifu.  Kwa njia hiyo basi wanapaswa kuadilisha ukweli. Papa aliendelea: “ Hacheni wengine wakusaidie, daima katika mazungumzo na wazee. Majadiliano ya vijana na babu ni muhimu sana. Lakini mbadilishe ukweli”  Papa kadhalika alitoa shukrani zake kwa kila kitu wanachofanya. Wanafunzi wanaobadilisha ukweli. Na waende mbele na ujasiri.  Hatimaye aliomba wamwombee na yeye anawaombea pia na aliwabariki wote.

Maendeleo elendelevu kufikia 2030

Kizazi 2030 ni mpango wa Shule ya Mafunzo ya Wanafunzi ambao ulileta pamoja kuanzia tarehe  24 hadi 26 Machi huko Montesilvano, mkowa wa Abruzzo, nchini Italia na  walikuwa wanafunzi elfu mbili ambao walitaka kuchukua jukumu la Maendeleo endelevu kufikia 2030 na ulimwengu wenye afya, ulimwengu wa haki na usawa, kama ilivyoelezwa kwenye tovuti ya Chama hicho cha Vijana Katoliki. Kwa mujibu wa taarifa yao waliandika kuwa: “Sio maneno, lakini njia tendaji za mabadiliko ya shule katika mwelekeo wa uendelevu, neno ambalo bado ni kidogo sana kati ya madawati. Mtu anaandika uendelevu na kusoma uwezo wa kuandaa siku zijazo kutoka katika chaguzi za sasa. Hii ndiyo changamoto ya kimisionari kwamba MSAC inakabiliwa na kuchukua Hatua ya Kikatoliki.”

28 March 2023, 16:11