Papa Ukuu wa upendo,umakini kwa wadogo&utamu wa Ubaba wa upendo
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wajumbe wa Shirika la Mtakatifu Yosefu (Giuseppini del Murialdo), Ijumaa tarehe 17 Machi 2023. Amemshukuru kwa Moyo Padre Tullio Locatelli kwa maneno ya hotuba yake aliyomuelekeza na kuwasalimia maaskofu waliokuwapo pamoja na Mama Orsola, Mkuu wa Shirika hilo na kuwashukuru wote. Wamekutana katika fursa ya miaka 150 tangu kuanzishwa kwa Shirika lao. Kiukweli, ilikuwa ni tarehe 19 Machi 1873 ambapo Mtakatifu Leonardo Murialdo alianzisha Chama huko Torino cha Mtakatifu Yosefu, kwa ajili ya kutunza na malezi hasa vijana wafanyakazi. Kwa hiyo Papa amefikiria sana kipindi hicho katika moto, katika kitovu cha Freemason, huko Torino mkoani Piemonto Italia, kwamba “kuna watakatifu wengi! Na tunapaswa kutafiti ni kwa nini katika kipinid hicho. Na kwa hakika ni katika kitovu cha Freemasonry lakini wachungaji na watakatifu walikuwa wengi”. Na walikuwapo huko Torino katika mantiki hiyo ngumu, ambayo ilikuwa imejikita katika umaskini mwingi wa kimaadili, kiutamaduni, na kiuchumi, mbele ya hayo yeye hakubaki kutojali kwani alikabiliana na changamoto na kuanza kazi, katikati ya Freemasonry. Kwa maana hiyo lilizaliwa shirika hilo katika uhalisia ambao katika mchakato wa karne na nusu imetajirisha watu, kazi na uzoefu wa kiutamaduni na zaidi ya yote upendo mwingi.
Ukweli huo ulioundwa leo hii una washirika wapatao mia tano watawa , Papa ameongeza kusema kuwa hao ni wachache ... inabidi wakue kidogo! - na, zaidi ya hayo, na Masista wa Murialdine wa Mtakatifu Yosefu ambao pia amewatakia heri katika kumbukumbu ya miaka sabini ya kuanzishwa kwao na Taasisi ya kilei yenye walei kadhaa, ambao wote wameunganishwa katika Familia moja. Mbegu iliyowekwa na Mungu katika Kanisa kupitia mikono mikarimu ya Mtakatifu Leonard Murialdo imeongezeka sana. Mwaka jana, Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa wakati wa ufunguzi wa maadhimisho haya ya jubilei, alimwandikia Mkuu wao na amewatakia waendelee kukua katika sanaa ya kuelewa mahitaji ya nyakati, na kuwapa ubunifu wa Roho takatifu. Kwa sababu huwezi kumtawala Roho, Yeye ndiye hutupeleka mbele. Kinachohitajika ni utambuzi na uaminifu. Aliwasihi wawe na uangalifu maalum kwa wadogo, ambao, leo hii kuliko wakati mwingine wowote, wanahitaji mashahidi wa kuaminika. Kwa hiyo anawatia moyo wasiache kuota, wakifuata mfano wa Mtakatifu Yosefu, Mlinzi wao, na Mtakatifu Leonard, katika roho ya ubaba halisi.
Papa Francisko wakati anapyaisha mwaliko wake amependa kususitiza kwao mambo matatu ambayo yanaonekana kwake kuwa muhimu kwa maisha yao na kwa utume wao. Nayo ni: ukuu wa upendo wa Mungu, umakini kwa ulimwengu unaobadilika na utamu wa kibaba wa upendo. Ukuu wa upendo wa Mungu, umakini kwa ulimwengu unaobadilika na utamu wa kibaba wa upendo. Uzoefu wa upendo wa Mungu uliashiria sana maisha ya Mtakatifu Leonard. Alikuwa anauhisi kuwa na nguvu, thabiti, isiyoweza kuzuilika, kama yeye mwenyewe anavyoshuhudia, akiandika: “Mungu ananipenda. Ni furaha iliyoje! (...) Hanisahau kamwe, ananifuata na kuniongoza daima!”. Papa ameongeza kusema “Leo hii mhubiri alituambia kuhusu hili”. Kwa hiyo alikuwa akiwaalika ndugu waache wapendezwe kwanza kabisa na na Mungu.
Kujiruhusu kupendwa na Mungu: hii ilikuwa siri ya maisha yake na utume wake. Sio upendo tu, hapana, ni kuacha kupendwa. Utovu huo, ule kutosheleza kwa maisha ya wakfu, ambayo hukua katika ukimya, katika sala, katika mapendo, na katika huduma. Na mwaliko huo unatuhusu pia: tujiruhusu kupendwa na Mungu ili tuwe mashuhuda wa kuaminika wa upendo wake; turuhusu upendo wake utuongoze katika mapendo, mawazo na matendo yetu zaidi na zaidi”. Sio sheria, sio masharti. Historia: wakati Mkuu wa Shirika la Wajesuit Padre Ledóchowski, alitaka kuweka pamoja hali ya kiroho ya Shirika katika kitabu, kudhibiti kila kitu kila kitu kilidhibitiwa ... pia kulikuwa na sheria ya mpishi, sheria, kila kitu kilidhibitiwa, kwa sababu Shirika la Yesu lilikuwa na sifa nzuri mbele yake na alituma nakala ya kwanza kwa Abate wa Kinediktini, naye alijibu: “Mpendwa Baba Mku, kwa hati yako hii umeua Jumuiya ya Yesu”. Unapotaka kudhibiti kila kitu, wewe unamfunga Roho Mtakatifu. Na kuna wengi, watawa kike na kiume, mapadre na maaskofu ambao wamemfunga Roho Mtakatifu. Tafadhali acha uhuru, acha ubunifu. Daima tutembea kwa kuongzwa na Roho.”
Papa amesema mtakatifu huyo alitambua kupokea thamani ya walei katika maisha na utume wa Watu wa Mungu. Katika nusu ya pili ya karne ya 19, karne moja kabla ya Vatikani II, alisema: “Mlei, wa tabaka lolote la kijamii, anaweza kuwa (...) mtume si chini ya kuhani na, kwa makundi mengine, zaidi ya kuhani”. “Katika enzi hiyo, hii ilionekana kama Uprotestanti. Alikuwa jasiri. Alikuwa mtu wa Mungu mwenye akili na muwazi!Kwa hiyo Papa ameombwa wakuze shauku yake sawa na ujasiri wake sawa: pamoja, walei, wanaume na wanawake watawa, kwenye njia za pamoja za sala, utambuzi na kazi, kuwa mafundi wa haki na ushirika. Katika suala hilo Papa amependa kurejea thamani moja muhimu ya mwisho ya karama yao: utamu wa baba wa upendo. Na ili waweze kuutafuta na kuuishi kati yao, katika roho ya udugu, na kuutumia kwa kila mtu. Papa amewaomba wawe kama Maria Mama yetu: wakati huo huo nguvu katika ushuhuda na utamu katika upendo. Mtakatifu Leonard alisema: “Upendo hutazama na kudhihirisha uzuri wa kila mmoja, kusamehe kutoka moyoni, kuwa na uso wa mtulivu, mkarimu na upole”. “Na kwa kufanya hivyo tunahitaji msalaba, tunahitaji kujua jinsi ya kubeba msalaba. Inahitajika maombi, inahitaji sadaka! Na tena, alisema: “Kama vile pasipo imani mtu hampendezi Mungu, vivyo hivyo pasipo utamu mtu hampendezi jirani yake”. Haya ni maneno yake: mpango rahisi na wenye nguvu wa maisha na utume.
Papa ameongeza kusema kuwa hata yeye angependa kutoa ushuhuda wa wanafunzi wao, alipokuwa profesa huko Mtakatifu Miguel, wao walikuwa wanasomea huko na walikuwa na Msimamizi mzuri sana. “Tulikuwa tukisema kwamba yule mdogo Joseph, Mkuu, alikuwa na Tuzo ya Nobel ya werevu! Kwa sababu alikuwa mtu wa Mungu, lakini mwerevu! Ilihamia vizuri! Nakumbuka vizuri… kundi zuri la wanafunzi”. Papa Francisko kwa hiyo kwa kuhitimisha ametaka kukumbusha mwaliko wake wa utakatifu kwamba: “Jifanyeni watakatifu na upesi ... Kwa sababu mtakatifu ana mtazamo wa mbali, hufanya maisha kuwa ya kibinadamu zaidi, huwasilisha matumaini na uaminifu na anajua jinsi ya kushiriki uzoefu wake kwamba Mungu ni Upendo”. Kwa hiyo Papa Francisko amewashukuru kwa kile walicho wa ona kile wanachofanya katika Kanisa, katika nyayo za Mtakatifu Leondard kwa kuiga mfano wa Mtakatifu Yosefu. Amewabariki kwa moyo na kuwaomba lakini wasisahau kusali kwa ajili yake.