Baba Mtakatifu Francisko katika Barua binafsi: “Motu proprio” ya tarehe 2 Aprili 2023, amefanya mabadiliko makubwa kwenye Sheria za Kanisa kwa ajili ya haki za watawa. Baba Mtakatifu Francisko katika Barua binafsi: “Motu proprio” ya tarehe 2 Aprili 2023, amefanya mabadiliko makubwa kwenye Sheria za Kanisa kwa ajili ya haki za watawa.  (Vatican Media)

Barua Binafsi ya Papa Francisko: Mabadiliko ya Sheria Kuhusu Haki za Watawa Wanaofukuzwa!

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume uliowekwa kwenye mfumo wa Barua binafsi: “Motu proprio” wa tarehe 2 Aprili 2023, amefanya mabadiliko makubwa kwenye Sheria za Kanisa kwa ajili ya watawa ambao watafukuzwa au kuachishwa maisha ya kitawa kwa mashirika husika, kwa kuongeza idadi ya siku thelathini ili kuweza kuwasilisha rufaa kwa viongozi wanaohusika, lengo ni kulinda haki msingi za mtawa husika! Haki za Mtawa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika Waraka wake wa Kitume uliowekwa kwenye mfumo wa Barua binafsi: “Motu proprio” wa tarehe 2 Aprili 2023, amefanya mabadiliko makubwa kwenye Sheria za Kanisa kwa ajili ya watawa ambao watafukuzwa au kuachishwa maisha ya kitawa kwa mashirika husika, kwa kuongeza idadi ya siku thelathini ili kuweza kuwasilisha rufaa kwa viongozi wanaohusika. Lengo ni kulinda utu, heshima na haki za watawa watakaokuwa wamefukuzwa kutoka utawani. Haya ni mabadiliko kutoka siku kumi za hapo awali hadi siku thelathini, kwa kutambua kwamba, mara nyingi hiki ni kipindi kigumu na chenye changamoto nyingi.

Haki za watawa wabaifukuzwa kwenye maaisha ya wakfu
Haki za watawa wabaifukuzwa kwenye maaisha ya wakfu

Ni katika muktadha huu, Baba Mtakatifu anafanya mabadiliko kwenye Sheria namba 700 CIC kwa Makanisa ya Magharibi, na Sheria Namba 501, CCEO kwa Makanisa ya Mashariki. Baba Mtakatifu anakaza kusema, mabadiliko haya ni kwa ajili ya kulinda, kuheshimu na kudumisha haki msingi za mtawa aliyefukuzwa au kuacha maisha ya kitawa mintarafu Sheria za Kanisa. Itakumbukwa kwamba Kanuni namba 697-699 ya Sheria za Kanisa kwa Makanissa ya Magharibi na Kanuni namba 497-4999 za Makanisa ya Mashariki, mara nyingi hazikuheshimiwa wala kuzingatiwa na viongozi wakuu wa Mashirika, kiasi cha wahusika wakuu kushindwa kujitetea kwenye vyombo husika.

Mchakato wa kumfukuza mtawa unapaswa kuzingatiwa kikamilifu.
Mchakato wa kumfukuza mtawa unapaswa kuzingatiwa kikamilifu.

Mabadiliko haya mapya pamoja na mambo mengine, yanaonesha mchakato unaopaswa kuheshimiwa: kwanza kabisa kabla ya mtawa kufukuzwa au kuachishwa Shirika anapaswa kuonywa kwa maandishi, au kuonywa mbele ya mashuhuda wawili kwa kumjulisha mtuhumiwa sababu ambazo zimewapelekea kuchukua maamuzi haya mazito sanjari na kutoa fursa ya mtuhumiwa kuweza kujitetea. Kama hatua hizi msingi hazitazingatiwa, uamuzi utakatolewa na viongozi wa Shirika unaweza kuwa ni batili, kwa kushindwa kuzingatia haki msingi za mtuhumiwa. Mabadiliko ya Sheria hizi za Kanisa yataanza kutumika rasmi Dominika tarehe 7 Mei 2023.

Papa Haki ya Mtawa

 

04 April 2023, 15:29