Papa akibariki mtoto wakati anazunguka kusalimia mahujaji na waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Papa akibariki mtoto wakati anazunguka kusalimia mahujaji na waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Hati ya Pacem in Terris inahamasisha maamuzi na mipango ya wakuu wa mataifa

Mwishoni mwa katekesi,Papa alikumbuka waraka wa amani wa Yohane XXIII uliochapishwa miaka 60 iliyopita katikati ya mvutano wa Vita Baridi: Ulikuwa ni taswira ya utulivu katikati ya mawingu meusi.Ujumbe wake unafaa sana.Papa ameomba kwa ajili ya Ukraine inayoteswa na kuomba huruma ya Mungu kwa kuzingatia Dominika ya Huruma ijayo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mtazamo wa utulivu katikati ya mawingu meusi. Kielelezo cha uwazi kilikuwa cha  Pacem in Terris,  ambao ni waraka wa amani wa  Papa Yohana XXIII, katika siku zake za mwisho wa upapa wake, uliochapishwa tarehe 11 Aprili 1963. Kwa hiyo mawingu meusi yalikuwa ni makabiliano ya kisiasa na kijeshi kati ya mataifa mawili makubwa yaliyoshinda Vita vya Pili vya Dunia ambayo yaliiweka dunia katika mashaka kutokana na hatari ya tishio la nyuklia. Papa Francisko Jumatano tarehe 12 Aprili 2023 mara baada ya Katekesi yake   amekumbuka hati muhimu ya Papa Roncalli.

Papa amesema kwamba tarehe 11 Aprili ilikuwa ni kumbukumbu ya miaka sitini ya andiko la Pacem in Terris ambalo Mtakatifu Yohane XXIII alielekeza kwa  Kanisa na kwa ulimwengu mzima katikati ya mvutano kati ya kambi mbili zinazopingana katika kile kinachoitwa Vita Baridi. Papa alifungua mbele ya kila mtu upeo mpana wa kuweza kuzungumza juu ya amani na kujenga amani, mpango wa Mungu kwa ulimwengu na familia yake ya kibinadamu.

Ujumbe  wa wakati muafaka

Kwa  upande wa Papa Francisko amebainisha kuwa , andiko hilo lilikuwa baraka ya kweli, kama taswira ya utulivu katikati ya mawingu meusi. Ujumbe wake unafaa sana, alisisitiza Papa huku akinukuu kifungu kizima, cha 62: Mahusiano kati ya jumuiya za kisiasa, kama yale kati ya binadamu binafsi, lazima yadhibitiwe si kwa kutumia nguvu za silaha, bali kwa mwanga wa sababu; yaani, katika ukweli, katika haki, katika mshikamano tendaji”.

Mwaliko kwa viongozi wa mataifa

Baba Mtakatifu amewaalika waamini, wanaume na wanawake wenye mapenzi mema, waraka wa “kusoma Pacem in Terris” kwamba “ Ninaomba viongozi wa mataifa wajiachie wahamasishwa nayo katika mipango na maamuzi yao.

Maombi kwa ajili ya Ukraine iliyopigwa

Papa Francisko aidha  amezingatia mizozo mingi na ya umwagaji damu inayoharibu mabara matano, kuanzia na lile la Ukraine. Kwa taifa lililoshambuliwa, Papa ameomba  kwa mara nyingine tena, kama kawaida katika miito kwa umma tangu mwanzo wa vita, kuomba na kutosahau nchi hiyo kwamba “ Tudumu katika maombi kwa ajili ya Ukraine iliyouawa kishahidi. Tuombe kwa ajili ya kile Ukraine inateseka

Tunahitaji Huruma ya Baba

Papa alikuwa tayari ameeleza hitaji la amani duniani katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland, ambao aliwakumbusha maadhimisho ya karibu ya Dominika ya  Huruma ya Mungu, iliyoanzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kama alivyotaka Bwana Yesu kupitia Mtakatifu Faustina Kowalska karibu karne moja iliyopita. Leo katika ulimwengu unaozidi kujaribiwa na vita na kujitenga na Mungu, tunahitaji hata zaidi Huruma ya Baba. Papa alisisitiza tena juu ya huruma  katika salamu zake kwa lugha ya Kiitaliano, ambayo haikosi kamwe kwa upande wa Mungu: “Bwana hakosi kamwe kuwa na huruma, tufikirie huruma ya Mungu anayetukaribisha daima, inatusindikiza daima. Hatuachi peke yetu kamwe”.

Papa baada ya Katekesi
12 April 2023, 16:10