Papa ameshiriki Mkutano wa kwanza na Baraza la Makardinali washauri
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mkutano umeanza tarehe 24 Aprili 2024 kwa uwepo wa Papa Francisko, katika Baraza la Makardinali. Huu ni mkutano wa kwanza wa Makardinali tisa (C9) washauri wa Papa baada ya upyaisho wa kiungo hicho kwa upande wa Papa mnamo tarehe 7 Machi iliyopita. Wajumbe wa Baraza jipya la makardinali ni Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, Fernando Vérgez Alzaga, Rais wa Serikali ya Mji wa Vatican; presidente del;Fridolin Ambongo Besungu, Askofu Mkuu wa Kinshasa; Oswald Gracias, Askofu Mkuu wa Bombay; Seán Patrick O'Malley, Askofu Mkuu wa Boston; Juan José Omella Omella, Askofu Mkuu wa Barcellona; Gérald Lacroix, Askofu Mkuu wa Québec; Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Lussemburg; Sérgio da Rocha, Askofu Mkuu wa Mtakatifu Salvador de Bahia. Katibu wa Kamati ni Askofu Marco Mellino, wa Cresima.
Baraza la Makardinali washauri 9 lilianzishwa na Papa Franciko na barua ya mkono wake mnamo tarehe 28 Septemba 2013 kwa ajili ya shughuli ya kumsaidia katika kuliongoza Kanisa la Ulimwengu na kujifunza mpango wa kusasisha katiba ya Curia Romana, ambayo hatimaye imeweza kutolewa katiba mpya ya kitume ‘Praedicate Evangelium’ iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi 2022. Mkutano wa kwanza wa makardinali (C9) ulifanyika mnamo Mosi Oktoba 2013 Na wakati huo huo mkutano wa mwisho ulifanyika mnamo Desemba 2022 ambao ulikuwa umejikita na mada ya hatua ya kibara ya mchakato wa Sinodi, iliyohitimishwa hivi karibuni, katika maandlizi ya Instrumentum laborius kwa ajili ya mkutano wa XVI wa Kawaida wa Sinodi, mnamo Oktoba ijayo.