Papa Francisko amewasili Hungaria
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Mji wa Budapest umekaribisha Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya miezi miwili yamaandalizi yasiyokoma, katika mji ulio tayari kuandika kurasa mpya katika historia yake ya miaka 2,000. Ndege ya Ita Airways Airbus A320, iliyopaa saa 02:21 asubuhi Ijumaa tarehe 28 Aprili kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Fiumicino, Roma, ilitua saa 03:53 kwenye uwanja wa ndege wa Ferenc Liszt, dakika chache kabla ya muda uliopangwa. Papa Francisko alishuka kutoka kwenye ndege katika lifti na kwenda kwa miguu, kwa msaada wa fimbo, kuwafikia waliokuwapo. Muda mfupi kabla, aliwasalimiana na Balozi wa Vatican nchini Hungaria Askofu Mkuu Michael Banach, na balozi wa Hungaria katika mji wa Vatican Eduard Habsburg-Lotharingiai.
Vile vile Papa alikaribishwa na naibu waziri mkuu na mvulana na msichana waliovalia mavazi ya kiutamaduni ambao wamempatia mkate na chumvi, ishara ya maisha, baraka na bahati nzuri. Papa Francisko amemega kipande kidogo cha mkate kwa mkono wake wa kula na kuonja, walipiga makofi ya waliohudhuria. Makumi ya watoto wadogo wakiwa wameshikilia bendera za Jiji la Vatican na Hungaria mikononi mwao. Kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa VIP Lounge, uwasilishaji wa wajumbe hulifanyika. Baada ya mkutano huu mfupi, kuhama kwenda Ukumbi wa Sàndor, ambayo ni makazi ya Rais wa Jamhuri ya Hungaria.