Papa Francisko:Hakuna tangazo bila harakati,bila safari!

Katika katekesi yake Jumatano baada ya Pasaka,Papa alizungumzia juu ya bidii ya kiinjili ambayo inaashiria utayari,maandalizi,kwamba mtu hawezi kubaki amefungwa ofisini,kwenye dawati akibishana kama simba wa kibodi na kubadilisha ubunifu wa tangazo na mawazo yaliyochukuliwa hapa na pale.Tunahitaji kuwa huru kutoka katika mipango hadi uwazi wa mshangao wa Mungu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika mwendelezo wa katekesi ya Baba Mtakatifu Francisko kwa mada ya Shauku ya Uinjilishaji:Bidii ya Kitume ya Mwamini, JUmatatno tarehe 12 Aprili 2023, Baba Mtakatifu Francisko, akiwageukia waamini na wamhujaji waliunganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro amesema “Baada ya kuona bidii binafsi ya Mtakatifu Paulo kwa ajili ya Injili majuma mawili yaliyopita, leo tunaweza kutafakari kwa kina zaidi bidii ya kiinjili kwani yeye mwenyewe anaizungumzia na kuielezea katika baadhi ya barua zake. Kwa mujibu wa uzoefu wake mwenyewe, Paulo hakosi kujua hatari ya bidii iliyopotoka, inayoelekezwa katika njia mbaya; yeye mwenyewe alikuwa ameanguka katika hatari hii kabla ya anguko la kimaongozi kwenye barabara ya kwenda Damasko. Wakati fulani tunapaswa kushughulika na shauku isiyoelekezwa, isiyo na kikomo katika kufuata kanuni za kibinadamu na za kizamani kwa jumuiya ya Kikristo. Haya aliandika Mtume  kwamba ni wema kwenu, lakini si kwa uaminifu (Gal 4:17).

Papa alibariki waamini wakati wa katekesi
Papa alibariki waamini wakati wa katekesi

Baba Mtakatifu amesema hatuwezi kupuuza ushawishi ambao wengine hujitolea kufanya kazi mbaya hata katika jumuiya yenyewe ya Kikristo; mtu anaweza kujivunia kuhusu msukumo wa uongo wa kiinjili huku katika hali halisi mtu akifuata ubatili au imani yake mwenyewe au kujipenda kidogo. Kwa sababu hii tujiulize: ni zipi sifa za bidii ya kweli ya kiinjili kulingana na Paulo? Kwa sababu hii, andiko lililosikika  mwanzo linaonekana kuwa la manufaa, orodha ya “silaha” ambazo Mtume anaonesha kwa ajili ya vita vya kiroho. Miongoni mwa haya ni utayari wa kueneza Injili, iliyotafsiriwa na wengine kama bidii ya mtu huyo ni mwenye bidii ya kuleta mawazo hayo, mambo hayo na inajulikana kama kiatu. Kwa nini? Inakuwaje kasi ya Injili inaunganishwa na kile unachoweka katika miguu yako? Fumbo hili linachukua andiko kutoka kwa nabii Isaya, ambalo linasema hivi: Ni jinsi gani ilivyo nzuri milima, miguu ya mjumbe anayetangaza amani,  ya mjumbe wa habari njema anayetangaza wokovu,  anayeambia Sayuni: “Tawala Mungu wako. ” (Is 52,7).

Papa Francisko amesalimia waamini
Papa Francisko amesalimia waamini

Hapa pia tunapata mrejesho wa  miguu ya mtangazaji wa habari njema. Kwa nini? Maana anayekwenda kutangaza lazima ahame, lazima atembee! Lakini pia tunaona kwamba Paulo, katika andiko hilo, anazungumza juu ya kiatu kama sehemu ya silaha, kulingana na mfano wa vifaa vya askari kwenda vitani: katika vita ilikuwa muhimu kuwa na utulivu wa msaada, ili kuepuka hatari ya ardhi ya eneo, kwa sababu mpinzani mara nyingi alitapakaza  katika uwanja wa vita na mitego, na kuwa na nguvu zinazohitajika ili kukimbia na kusonga katika mwelekeo sahihi. Kwa hivyo, kiatu ni kwa ajili ya kukimbia na kuepuka mambo haya yote ya mpinzani.

Mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia
Mahujaji kutoka sehemu mbali mbali za dunia

Bidii ya Kiinjili ni tegemezo ambalo juu yake tangazo limeegemezwa, na watangazaji wanafanana kidogo na miguu ya mwili wa Kristo ambao ni Kanisa. Hakuna tangazo bila harakati, bila kutoka, bila mpango wa kuanzisha. Hii ina maana kwamba hakuna Mkristo ambaye hajiweki  katika safari, au Mkristo ambaye  hatoki nje ya nafsi yake kupeleka tangazo, sio Mkristo. Hakuna tangazo bila harakati, bila safari. Injili haitangazwi ikiwa imesimama, imefungwa ofisini, kwenye dawati au kwenye kompyuta ikibishana kama simba wa kibodi na kubadilisha ubunifu wa tangazo kwa kunakili-na-kubandika mawazo yanayochukuliwa hapa na pale. Injili inatangazwa kwa kutembea, kuondoka na kwenda, Papa amesisitiza. Neno lililotumiwa na Paulo, kuonesha viatu vya wale wanaobeba Injili, ni neno la Kigiriki linaloashiria utayari, maandalizi, uchangamfu. Ni kinyume cha uzembe, usiopatana na upendo. Kiukweli mahali pengine Paulo asema: “Msiwe wavivu katika bidii yenu; badala yake iweni na juhudi katika roho, mkimtumikia Bwana” (Rm12:11). Mtazamo huu ndio uliotakiwa katika Kitabu cha Kutoka ili kuadhimisha sadaka ya ukombozi wa Pasaka: “Hivi ndivyo mtakavyoila: mmejifunga viuno, mmevaa viatu miguuni, fimbo mkononi; utakula haraka. Ni Pasaka ya Bwana! Usiku huo nitapita” (Kut 12:11-12a).

Papa anawaslimia wanandoa wapya
Papa anawaslimia wanandoa wapya

Mtangazaji yuko tayari kuondoka, na anajua kwamba Bwana hupita kwa njia ya kushangaza; kwa hiyo lazima awe huru kutokana na mipango na kutabiriwa kwa hatua isiyotarajiwa na mpya: tayari kwa mshangao. Yeyote anayetangaza Injili hawezi kubakizwa katika vizimba vya kusadikika au katika “imefanywa hivi sikuzote”, bali yuko tayari kufuata hekima ambayo si ya ulimwengu huu, kama vile Paulo asemavyo kujihusu mwenyewe: “Neno langu ni langu na kuhubiri hakutokani na maneno ya hekima yenye kuvutia, bali kwa udhihirisho wa Roho na nguvu zake, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu” (1Kor 2:4-5).

Uwanja wa Mtakatifu Petro umechanua
Uwanja wa Mtakatifu Petro umechanua

Kwa hiyo Papa Francisko amesema hapo ni muhimu kuwa na utayari huu kwa ajili ya upya wa Injili, mtazamo huu ambao ni msukumo, kuchukua hatua, kwenda kwanza. Si kuruhusu fursa kupotea ili kutangaza utangazaji wa Injili ya amani, amani ambayo Kristo anajua jinsi ya kutoa zaidi na bora kuliko ulimwengu. Na kwa hili amewasihi wawe waeneza Injili wanaosonga mbele, bila woga, wanaosonga mbele, kupeleka uzuri wa Yesu, kupeleka upya wa Yesu unaobadilisha kila kitu. Kwa kutoa mfano Papa amesema: “Ndiyo, Baba, hubadilisha kalenda, kwa sababu sasa tunahesabu miaka kabla ya Yesu…” – “Lakini pia, na wewe badili moyo wako: na  je uko tayari kumruhusu Yesu kubadilisha moyo wako? Au wewe ni Mkristo wa vuguvugu ambaye hasogei? Fikiria juu yake na uwe na shauku juu ya Yesu, je, unaendelea? Fikiria kidogo...” Papa amehitimisha.

Katekesi ya Papa
12 April 2023, 16:02