2023.04.28 Papa akiwa amenyanya masalia ya Mtakatifu Stefano katika kanisa Kuu la Mtakatifu huyo huko Budapest. 2023.04.28 Papa akiwa amenyanya masalia ya Mtakatifu Stefano katika kanisa Kuu la Mtakatifu huyo huko Budapest.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amesikiliza shuhuda:Sisi ni vyombo vya Mungu kuonesha watu wetu furaha ya Injili

Wakati wa mkutano katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano,Budapest na maaskofu wa Hungaria,mapadre,mashemasi,watawa kike na kiume,waseminari na wahudumu wa kichungaji.Zimesikika shuhuda kutoka kwa Padre mzee na Kuhani wa Kigiriki-Katoliki na baba wa watoto sita,pamoj,mtawa Mdominika na katekista mlei.

Na angella Rwezaula,- Vatican.

Ni katika Ziara ya Kitume ya 41 ya Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 28 -30 Aprili 2023 ambapo kwa kuhimitisha siku amesikiliza shuhuda za wanaume wawili na wanawake wawili, Padre mzee kaka yake ni mwenyeheri, padre wa Kigiriki-Katoliki na baba wa watoto sita, ambaye ni msemaji wa radio, mtawa kijana wa shirika la Domenikani pamoja na  Katekista mlei anayeshirikiana na Baraza la Maaskofu wa Hungaria. Kwa hiyo hawa ndio mashuhuda waliochaguliwa na Kanisa la Hungaria kwa ajili ya mkutano hu una Papa  katika Kanisa kuu la Mtakatifu  Stefano mjini Budapest, ambalo limekuwa ni tukio la pili la hadhara la safari yake ya kitume nchini Hungaria.  Ikumbukwe hotuba ya Kwanza ilikuwa ni kwa Mamlaka ya Taifa zima, mara tu alipwasili nchini humo. Katika Kanisa lililopewa jina la mfalme wa kwanza wa Hungaria na kuwekwa wakfu mbele ya mfalme Franz Joseph wa Austria-Hungaria, walizungumza baada ya salamu za rais wa Baraza la Maaskofu, Askofu  András Veres, na mbele ya Papa. Hawa walitoa sauti kwa hisia za mapadre zaidi ya elfu moja wa Hungaria, mashemasi, wanaume na wanawake waliowekwa wakfu, waseminari na wachungaji waliojaza hekalu la karne ya kumi na tisa, kati ya elfu 4 waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu ambao walikuwa wakifuatilia mkutano  wa Francisko kupitia vyombo vya Habari na Skrini.

Papa Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano
Papa Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano

Wa kwanza kuzungumza alikuwa Padre József Brenner, msimamizi wa Jimbo  la Szombathely, kaka yake ni Mwenyeheri János Brenner, aliyeuawa kikatili - akiwa na umri wa miaka 26 na serikali ya wasioamini uwepo wa Mungu" huko  Hungaria chini ya nira ya ukomunisti wa kisoviet. Papa  alisema kuwa  kaka yake, alimjumuisha katika safu ya wenyeheri mnamo 2018.  Kwa hiyo József, kuhani mwenye umri wa miaka 66, ni mtoto wa tatu kuzaliwa, János alikuwa mzaliwa wa pili, lakini kaka yake  wa kwanza pia alikuwa padre. Shukrani kwa wazazi wawili ambao walikuwa wameishi maisha matakatifu alisisitiza kuhani mzee wa Hungari - baba aliyejitolea kwa sala na mama ambaye alisaidia maskini. Na amesimulia juu ya baba ambaye alikwenda  misa kila asubuhi na kwenye dawati la ofisi yake aliweka misa ya Kilatini na Kihungariani. Kwa wale waliompendekeza asimpeleke kazini, aliwajibu “Kwanini? Mtu huyu hakuumiza mtu yeyote! Kwa meneja wa ofisi aliyemwita asiyeaminika, kwa sababu anasomesha watoto wake  wawili kuwa mapadri, alijibu huku akicheka: “Ninaomba msamaha: watatu, sio wawili!” Padre  József alisisitiza kwamba mapadre wa Magyar ambao waliishi wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu kama yeye wamekuwa waaminifu kwa Kanisa kila wakati. Ilitubidi kukimbia na hatimaye wakateseka na mateso ya ukomunisti kwa miongo kadhaa. Alimkumbusha Baba Mtakatifu Francisko kauli mbiu ya kipadre ya ndugu yake mfiadini na mwenyeheri: “Kila kitu huchangia katika wema kwa wampendao Mungu” na maneno ya Mtakatifu Petro: “Bwana, twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Mwishoni mwa ushuhuda wake, baada ya kumkumbatia, Papa alibusu mikono ya Padre Brenner.

Maaskofu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano na Papa
Maaskofu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano na Papa

Akiyefuata ni kuhani Sándor Kondás, padre Mgiriki-Mkatoliki ya Upatriaki wa Miskolc, anayehusika na studio ya Kituo cha Vyombo vya Habari  Kikatoliki cha Ugiriki. Alinza na  salamu ile ile aitumiayo kwa wasikilizaji wake wa radio kwa miaka 30: “Kristo yuko katikati yetu!” “Ni, na itakuwa!”. Katikaushuhuda wake amesema kuwa wito wake wa ukuhani unahusishwa na kanisa la kijiji chake cha asili, kwenye kilima kinachotazamana na nyumba zote, “kwangu mimi ni mahali pa mwaliko na mahali pa kumbukumbu”. Amekumbuka kuwa katika kanisa hilo alipewa daraja la upadri, “juu ya kaburi la mchungaji aliyenibatiza”. Kisha alizungumza kuhusu ndoa na “msichana yule tuliyekutana naye mara nyingi sana, kufikia hatua ya kutambua kwamba tulikuwa tumekusudiwa kwa ajili ya kila mmoja wetu na Mungu” kuwa zawadi kutoka kwa Bwana, jambo ambalo lilifanya wote wawili waseme: “Na tujitoe sisi kwa sisi na maisha yetu yote kwa Kristo Mungu wetu”. Wakati huo, alikumbuka, kuwa “tulipanga kujenga kanisa kuu la kanisa kuu pamoja na ndoa yetu.” Miaka mingi imepita, “tunaona kwamba, kama sio kanisa kuu, angalau tumejenga 'kikanisa kidogo cha   dharura' ambapo mtu yeyote anaweza kuingia wakati wowote”.

Watoa ushuhuda mbele ya Papa
Watoa ushuhuda mbele ya Papa

Kuhani wa Kigiriki Kondas na mke wake, baada ya kuzaa  mtoto, waliendelea kuwa  watoto wengine wanne, na wa tano akiwa ni mgonjwa wa utindi wa ubongo. “Bwana pia alitusaidia kukubali uwezo wao na hali zao za afya kama zilivyokuwa katika hali yake ya kimungu”. Amemshukuru Mungu ambaye, “tangu mwanzo wa wito wangu wa kikuhani, ameniweka huru kutoka katika kushindwa na ameniruhusu kukubali hali zisizowezekana, kwa sababu ni kutoka kwao kwamba mtu anaweza kuteka ubora zaidi”. Kwa hiyo  alielewa, shukrani kwa Bwana, kwamba ufanisi wa huduma ya ukuhani haupimwi kwa kile anachoweza kufanya, lakini kwa kiasi gani anaweza kujiondoa mwenyewe, kujiacha kwake. Naye alihitimisha kwa kueleza kwamba yeye ni mwenye furaha anapofanikiwa katika makanisa kuwa na uthibitisho wa kuwapo halisi kwa Bwana, “huko, ambapo macho yake yang’aa kupitia sanamu, nyuso za watakatifu wanaong’aa milele. Ambapo, pamoja na moshi wa uvumba, na nyimbo za fahari, na sala za mara kwa mara, roho yangu hupanda kwa Mungu”.

Uzuri wa Kanisa Kuu Budapest Hungaria
Uzuri wa Kanisa Kuu Budapest Hungaria

Baada ya kuimba kwa kwaya ya Kanisa kuu shirikishi, Sista Krisztina Hernády, mtawa kijana wa Shirika la Wadominikani , alizungumza kwa uwazi kuhusu kwa nini aliamua kuwa mtawa katika karne ya 21. Alikumbuka kwamba alipokuwa mtoto, alimsikiliza nyanya yake akizungumzia watakatifu wa nasaba ya Arpadi ya Hungaria,kwa hiyo shauku kuwa mtakatifu ilizaliwa moyoni mwake. Sio thamani ya kuishi kwa chini. Lakini, alipoanza kuelewa kwamba Mungu alikuwa akimwita kwenye njia thabiti sana, alianz "kujadiliana na Yesu kwa nini alikuwa ana mwiita wakati ana kaka na dada watano, na angeweza kuchagua mtu mwingine. Na alishangaa kwa nini Mungu alitaka msichana wa miaka ishirini apitie maisha akiwa amevaa 'nguo nyesui kama mjane. Inaweza kuonekana kwamba “Sikuwa na shauku hasa kuhusu wito wa Yesu kwa utawa, angalau mwanzoni”. Lakini wakati wa mafungo na Wajesuiti, kwa msaada wa mtawa wa Kifransisko na mmoja wa baba wa Piarist aligundua furaha ya kuwa katika uhusiano wa moja kwa moja na wa kibinafsi na Mungu. Na alijihakikishia kwamba kila mtu ulimwenguni anapaswa kujua kuhusu furaha hiyo, na akakuza hamu ya kuifanyia kazi.

Siku 3 za Ziara ya kitume huko Budapest

Kwa kuhitimisha Sr. Krisztina, alisema “Ninaishi na kufundisha katika Hódmezővásárhely, jiji lililo kusini-mashariki mwa Hungaria, pamoja na wtawa wengine sita wa Kidominikani”. Katika eneo hilo, anaeleza, “sura ya Mungu anayetupenda kibinafsi na kututunza imefifia katika akili za watu wakati wa majaribu ya karne chache zilizopita”. Kwa hiyo yeye na watawa wenzake wanakabiliwa kila siku na umaskini wa kimwili na kiroho wa watu, lakini  ni ukweli kwamba katika mioyo ya watu kuna uwazi wa mema na utafutaji wa majibu safi kweli wa kupatiwa matumaini. Hivyo Wadominikani wanajaribu kuwa vyombo vya Mungu ambavyo kupitia hivyo wanaweza kuwaonesha watu wao furaha ya Injili.

Katekista aliyetoa ushuhuda mbele ya Papa
Katekista aliyetoa ushuhuda mbele ya Papa

Kwa upande wake Dorina Pavelczak-Major, mshiriki mkuu katika Tume ya Katekesi ya Baraza la Maaskofu wa Hungaria, ambayo inawakilisha jumuiya kubwa ya wachungaji walei, wahudumu wa liturujia ya Neno, wahudumu wa ajabu wa Umoja wa Ekaristi, wasomaji, wakoliti,  na makatekista. Kwa hiyo Walei ambao wanatekeleza taaluma yao katika nyanja za elimu ya Kikatoliki, huduma za kijamii na afya, na wakati huo huo, bila shaka, wanatilia maanani sana katekesi katika taasisi za elimu za umma, pia kwa sababu wengi wanasubiri Injili ya Yesu Kristo, amefafanua. Huduma ya kweli ya uinjilishaji, kwa mujibu wa  Dorina, “kwetu sisi pia inaoneshwa kwa uwepo katika maisha ya familia za Kikristo, katika mazungumzo nao. Na alikumbuka kwamba vifungu ambavyo Baba Mtakatifu amewatolea vina msaada mkubwa kuhusiana na uinjilishaji, katekesi, maswali ya kijamii na yale yanayohusu jamii. Na kwa kuhitimisha ametoa shukrani kwa sababu, kama mitume, amesema “sisi pia tunaweza kuishi na kusema kwa uhakika kwamba Yesu Kristo ndiye wakati wetu ujao, yaani, Yeye ndiye njia, kweli na uzima”.

Yaliyojiri yakisimuliwa na Mwandishi wetu wa Habari Vatican News
28 April 2023, 18:44