Papa Francisko,Mkutano kwa waliowekwa wakfu:Muwe wakarimu wa kinabii

Katika kukutana na mapadre,mashemasi,watu waliowekwa wakfu,waseminari na wahudumu wa kichungaji,katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano,Budapet,Papa amesikiliza shuhuda nne zilizotolewa.Na katika hotuba amesema mahekalu ya wanadamu yanapoanguka mambo ya kutisha yanatokea.

Na Angella Rwezaula; -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 28 Aprili jioni  katika kukutana na mapadre, mashemasi  watawa wa kike na kiume na waseminari, wahudumu wa kichungaji, Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano huko Budapest kwanza kabisa amesikiliza baadhi ya shuhuda mbali mbali kabla ya kutoa hotuba yake. Katika hotuba hiyo ameanza kwa salamu ya “Tumsifu Yesu Kristo (dicsértessék a Jézus Krisztus!, laudetur Jesus Christus!) Papa ameonesha furaha ya kuwepo kwake mara baada ya kushikirishana furaha ya Kongamano la Ekaristi kimataifa. Ilikuwa wakati muafaka wa neema na anao uhakika kuwa matunda yake ya  ya kiroho yapo yanawasindikiza. “Katika ulimwengu huu unaobadilika tunataka kushuhudia kwamba Kristo ndiye maisha yetu ya baadaye”. Ni moja ya mahitaji muhimu sana kwetu: kutafsiri mabadiliko na hasa mabadiliko ya zama zetu, kujaribu kukabiliana vyema na changamoto za kichungaji. Lakini hicho kinawezekana kwa kutazama Kristo kama wakati wetu ujao. "Yeye ni Alfa na Omega, Mimi ndiye niliyepo, aliyekuwepo na anayekuja. Mimi ni Mwenye Uwezo Wote.” Mwanzo na mwisho, msingi na nusu ya mwisho wa historia ya Ubinadamu."

Papa akibariki waamini
Papa akibariki waamini

Kwa kutafakari katika kipindi hiki cha Pasaka utukufa wake. Ambaye ni Mwanzo na Mwisho. (1,17, Papa amesema tunaweza kutazama dhoruba ambazo wakati mwinginei zinapiga ulimwengu wetu, mapigano ya haraka na jamii inayonea na migogoro ya imani Mashariki kwa mtazamo ambao hauangukii na kukata tamaa na ambao haupotezi mtazamo wa kiini cha Pasaka: Kristo mfufuka, kitovu cha Historia, ni wakati ujao. “Maisha yetu, ingawa yanaoneshwa na udhaifu, yamewekwa katika nguvu mikononi mwake. Tukisahau hili, sisi pia, wachungaji na walei, tutatafuta njia za kibinadamu na vyombo vya kujilinda na ulimwengu, tukijifungia katika maeneo yetu ya kidini yenye starehe na amani; au, kinyume chake, tutakabiliana na pepo zinazobadilika za ulimwengu na, basi, Ukristo wetu utapoteza nguvu na tutakoma kuwa chumvi ya dunia.”

Picha ya Pamoja  na maaskofu baada ya hotuba yake
Picha ya Pamoja na maaskofu baada ya hotuba yake

Kristo Mfufuka ni kitovu cha Hisotria na ni wakati ujao. Kwa hivyo, hizi ndizo tafsiri mbili ambapo Papa alipenda kusema majaribu mawili ambayo lazima kujilinda  kama Kanisa kila wakati: usomaji wa majanga ya historia ya sasa, ambayo inaonesha kushindwa kwa wale wanaorudia kwamba yote yamepotea, kwamba hakuna zaidi ya mara moja, ambayo hatujui tutaishia wapi. Ni vizuri kwamba Mchungaji Sándor alionesha shukrani zake kwa Mungu ambaye “alimkomboa kutoka katika kushindwa.” Vile vile kuna hatari nyingine, ile ya kusoma kwa ujinga wakati wa mtu mwenyewe, ambayo badala yake inategemea urahisi wa kufuata na inatufanya tuamini kwamba mwishowe kila kitu kiko sawa, kwamba ulimwengu umebadilika kwa sasa na tunahitaji kuzoea. Hapa, dhidi ya kushindwa kwa janga na ulinganifu wa kidunia, Injili inatupatia mapya, inatupatia neema ya utambuzi wa kuingia wakati wetu kwa mtazamo wa kukaribisha, lakini pia kwa roho ya kinabii.

Katika hili Papa ampenda kusema kwa  ufupi juu ya picha nzuri iliyotumiwa na Yesu: ile ya mtini (Mk 13:28-29). Kwa hiyo ni kuelezea  sisi katika muktadha wa Hekalu la Yerusalemu. Kwa wale waliostaajabia mawe yake mazuri na hivyo wakaishi aina fulani ya upatano wa kilimwengu, wakiweka usalama katika nafasi takatifu na katika fahari yake kuu, Yesu alisema kwamba hakuna kitu chochote duniani ambacho kinapaswa kufutwa, kwa sababu kila kitu ni hatari na hakuna jiwe litakalobaki juu ya jiwe; lakini, wakati huo huo, Bwana hakutaka kusababisha kuvunjika moyo au hofu. Na kwa hiyo aliongeza: wakati kila kitu kinapopita, wakati mahekalu ya wanadamu yanapoanguka, mambo ya kutisha yanatokea na kutakuwa na mateso makali, ndipo “watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu akiwa na nguvu nyingi na utukufu”.

Kwa ufupi yaliyojiri katika mkutano

Na hapo ndipo anatualika kuwa: “Jifunzeni mfano kutoka katika mtini: tawi lake likianza kuwa laini na majani kuchipua, mwajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia. Vivyo hivyo na ninyi: mwonapo mambo hayo yakitendeka, jueni ya kuwa yu karibu, yu karibu na malango” (Mk 13, 28-29). Kwa hiyo tunaitwa kukaribisha nyakati tunazoishi kama mmea wenye kuzaa matunda, pamoja na mabadiliko na changamoto zake, kwa sababu kwa hakika katika haya yote - Injili inasema - Bwana anakaribia. Na wakati huo huo tunaitwa kulima msimu wetu huu, kwa kuusoma, kupanda Injili huko, kukata matawi kavu ya uovu, ili  kuzaa matunda. Tumeitwa kwa makaribisho ya kinabii.

Papa anambariki mtoto aliyemkabidhi zawadi ya maua alipingia Kanisani
Papa anambariki mtoto aliyemkabidhi zawadi ya maua alipingia Kanisani

Makaribisho ya kinabii: Ni suala la kujifunza kutambua ishara za uwepo wa Mungu katika uhalisia, hata pale ambapo haionekani kuwa na alama ya wazi ya roho ya Kikristo na kuja kukutana nasi na tabia yake ya changamoto au maswali. Na, wakati huo huo, ni suala la kufasiri kila kitu katika mwanga wa Injili bila kuwa wa kidunia, lakini kama watangazaji na mashuhuda  wa unabii wa Kikristo.  Baba Mtakatifu amesema “Tunaona kwamba hata katika nchi hii, ambapo mapokeo ya imani yamekita mizizi sana, tunashuhudia kuenea kwa usekula na mambo yanayoambatana nao, ambayo mara nyingi huhatarisha kutishia uadilifu na uzuri wa familia, kuwaangazia vijana kwa mifano ya kupenda mali na ili kugawanya mjadala juu ya masuala mapya na changamoto.

Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa, jaribu linaweza kuwa ngumu, kujiondoa na kupitisha tabia ya kuwa ‘mpiganaji’. Lakini mambo haya halisi yanaweza kuwakilisha fursa kwetu sisi Wakristo, kwa sababu yanachochea imani na kuzamishwa kwa baadhi ya dhamira, yanatualika kujiuliza jinsi gani changamoto hizi zinavyoweza kuingia katika mazungumzo na Injili, kutafuta njia, zana na lugha mpya. Kwa maana hiyo, Papa Benedikto wa kumi na sita alithibitisha kwamba enzi tofauti za utengano wa kidini huja kusaidia Kanisa kwa sababu “zimechangia kwa njia muhimu katika utakaso wake na mageuzi ya mambo ya ndani. Kwa hakika, kujitenga [...] kila wakati kulimaanisha ukombozi wa kina wa Kanisa kutoka kwa aina za ulimwengu" (Mkutano na Wakatoliki wanaojishughulisha na Kanisa na katika jamii, Freiburg im Breisgau, 25 Septemba 2011).

Papa akitazama na kusali mbele ya Picha ya Bikira Maria Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano
Papa akitazama na kusali mbele ya Picha ya Bikira Maria Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano

Jitihada ya kuingia katika mazungumzo na hali  leo hii inaitaka Jumuiya ya Kikristo kuwepo na kushuhudia, ili kujua namna ya kusikiliza maswali na changamoto bila woga wala ukakamavu. Hii si rahisi katika hali ya sasa, kwa sababu hakuna ugumu wa shida hata ndani.  Hasa, Papa amependa kumlika mzigo wa kazi kwa makuhani. Kwa upande mmoja, mahitaji ya maisha ya parokia na ya kichungaji ni mengi lakini, kwa upande mwingine, miito inapungua na mapadre ni wachache, mara nyingi wamezeeka na kuna dalili za uchovu". Hii ni hali ya kawaida kwa mambo mengi ya Ulaya, ambayo ni muhimu kwamba kila mtu wachungaji na walei, kujisikia kuwajibika kwa ushirikiano: juu ya yote katika maombi, kwa sababu majibu hutoka kwa Bwana na si kutoka kwa ulimwengu, ni kutoka katika hema na sio kutoka katika  kompyuta. Na baadaye  katika shauku ya huduma ya wito, kutafuta njia za kuwapa vijana kwa shauku shauku ya kumfuata Yesu hata  kwa njia ile ya kipekee ya kuwekwa wakfu.

Kile ambacho amesimulia Sr Krisztina kuhusu “kubishana na Yesu,  kwamba ni kwa nini alimwita ni nzuri: kuna haja ya mtu anayesikiliza na kusaidia kujadili vizuri na Bwana! Na, kwa ujumla zaidi, kuna haja ya kuanza tafakari ya kikanisa, sinodi, ifanywe wote kwa pamoja  kusasisha maisha ya kichungaji, bila kuridhika na kurudia yaliyopita na bila woga wa mapya ya  parokia katika eneo, lakini kuiweka kama kanisa, kipaumbele cha uinjilishaji na kuanzisha ushirikiano kati ya mapadre, makatekista, wachungaji na walimu. Papa amesema wao wako katika njia hiyo na hivyo wasisimame. Watafuta njia iwezekanavyo kwa ajili ya kushirikiana kwa furaha ya sababu ya Injili na kupeleka mbele pamoja, kwa kila mmoja ya karama, uchungaji kama tangazo la Kerigima. Ni vizuri kwa maana ambayo mafundisho yalisukuma kuwa na hitaji ya kufikia jirani kupitia kusimulia, kuwasiliana na kugusa maisha ya kila siku. Papa amewashukuru mashemasi na makatekesita ambao walitoa nafasi muhimu kueneza imani kwa kizazi cha vijana, na walimu  na wafundaji ambao wanajitahidi kwa ukarimu katika nyanja hiyo ya kielimu. Papa amethibitisha kuwa uchungaji mwema unawezekana ikiwa kuna uwezo wa kuishi upendo ambao Bwana aliagiza na ambao ni zawadi ya Roho wake.

Papa akisalimiana na waamini huko Hungaria
Papa akisalimiana na waamini huko Hungaria

Hii inafundisha kukaribisha kinabii,  katika kupeleka faraja ya Bwana kwenye hali za uchungu na umaskini duniani, kukaa karibu na Wakristo wanaoteswa, wahamiaji wanaotafuta ukarimu, watu wa makabila mengine, mtu yeyote anayehitaji. Kwa maana hiyo, wao wana mifano mizuri ya utakatifu, kama Mtakatifu Martino. Kitendo chake cha kuwagawia maskini joho ni zaidi ya kazi ya hisani: ni taswira ya Kanisa ambalo linapaswa kulisimamia, ndilo ambalo Kanisa la Hungaria linaweza kuleta kama unabii katika moyo wa Ulaya: huruma, upole na ukaribu. Lakini pia Papa amekumbusha Mtakatifu Stefano, ambaye masalio yake yake yalikuwa kandoni mwake wakati anatoa hotuba yake: Yeye, ambaye alikuwa wa kwanza kulikabidhi taifa kwa Mama wa Mungu, ambaye alikuwa mwinjili shupavu na mwanzilishi wa monasteri na abasia, pia alijua jinsi ya kusikiliza na mazungumzo na kila mtu na kushughulika na maskini: aliwapunguzia kodi na akaenda kutoa sadaka kwa kujibadilisha ili asitambulike. Hili ndilo Kanisa tunalopaswa kuota Papa amehimiza kwamba , Kanisa  lenye uwezo wa kusikilizana, mazungumzo, makini na wanyonge; kuwakaribisha wote na kwa ujasiri katika kuleta unabii wa Injili kwa kila mmoja.

Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano ulijaa waamini
Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Stefano ulijaa waamini

Kristo ni wakati wetu ujao, kwa sababu ni Yeye anayeongoza historia. Walikuwa wanaamini kwa dhati waungamishi wao wa imani: maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume walifia dini wakati wa mateso ya ukana Mungu; wao wanashuhuda imani sahihi ya watu wa Hungaria. Papa amekumbuka tena Kardinali Mindszenty, ambao waliamini katika nguvu ya maombi, hadi leo, karibu kama msemo maarufu, unarudiwa hapo kwamba: “Ikiwa kuna Wahungaria milioni katika sala, sitaogopa wakati ujao.” Baba Mtakatifu kwa hiyo amewashauri wawe wakaribishaji, wawe mashuhuda  wa unabii wa Injili, lakini juu ya yote wawe wanawake na wanaume wa sala, kwa sababu historia na siku zijazo inategemea hilo. Kwa kuhitimisha amewashukuru kwa imani yao na uaminifu wao, kwa mema yote waliyo nayo na wanayofanya. Papa hakuweza  kusahau ushuhuda wa ujasiri na subira wa Masista wa Hungaria wa Shirika la Yesu aliokutana nao huko Argentina baada ya kuondoka Hungaria wakati wa manyanyaso ya kidini. Amethibitisha kwamba walimtendea mema sana. Anawaombea, kwamba kwa kufuata mfano wa mashahidi wao wakuu wa imani, wasishikwe na uchovu wa ndani na waweze kwenda mbele kwa furaha.

Umati wa waamini waliokuwa wakimsubiri Papa nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Sefano
Umati wa waamini waliokuwa wakimsubiri Papa nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Sefano

Baada ya hotuba yake, Papa Francisko ameongoza sala ya Baba Yetu... amewabariki wote na hatimaye picha ya Pamoja na Maaskofu na kuondoka kurudi katika Makao ya Ubalozi wa Vatican nchini Hungaria. Katika Uwaja wa Kanisa Kuu, umati ulifuatilia na pia kumsalimia Papa wakati alipotoka nje ya Kanisa Kuu.

28 April 2023, 18:47