2023.04.13 Papa amekutana na wajumbe wa Chama cha kidini cha Taasisi za kijamii kiafya (ARIS). 2023.04.13 Papa amekutana na wajumbe wa Chama cha kidini cha Taasisi za kijamii kiafya (ARIS).  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:kuheshimu hadhi ya wazee&kuwanyima dawa ni euthanasia iliyofichika

Akikutana na wanachama wa Jumuiya ya Kidini ya Taasisi za Afya ya Jamii(ARIS) Papa 13 amezungumzia utamaduni wa kutupa ambao katika sekta ya afya unaweza kuonesha matokeo ya chungu zaidi.Ametoa wito wa kuangalia hatari ya kujua mikasa ya wengine hasa wanyonge.Lazima kuheshimu hadhi ya wazeena kuwanyima dawa ni euthanasia iliyofichika.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Alhamisi tarehe 13 Aprili 2023, amekutana na Chama cha Kidini cha Kiafya ARIS ambapo amemshuru Rais wake Padre Virginio Bebber, kwa maneno ya hotuba yake , na kuwakaribisha wote, wakati huo huo akimsalimia Mkurugenzi Ofisi ya Kichungaji ya Afya ya Baraza la Maaskofu wa Italia. Chama  hiki kinaleta pamoja wawakilishi wa Taasisi za Kikanisa (za kidini na za kiulimwengu) au zilizounganishwa nazo, ambazo hutoa huduma za afya au kazi za kibinafsi ambazo zimegawanywa, zinazofanya kazi katika eneo la kitaifa. Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amebaonisha kwamba katika muundano wao wa kiafya kidini, unafafanishwa na nyumba ya Msamaria mwema (Lk 10,25-37), mahali ambapo wagonjwa wanaweza kupokea “mafuta ya faraja na divai ya matumaini”.

Papa amekutana na wajumbe wa ARIS
Papa amekutana na wajumbe wa ARIS

Katika hotuba yake, Papa Francisko amekumbusha jinsi huduma ya afya ya kidini nchini Italia ilivyo na historia nzuri na ya karne nyingi na mengi ambayo Kanisa limeweza kufanya, kwa njia ya huduma ya afya, kusikiliza na kulipa kipaumbele kwa maskini, sehemu dhaifu na zilizotelekezwa ya jamii. Na baadaye alizingatia hatari kadhaa kwamba “Katika sekta ya afya, utamaduni wa taka unaweza kuonyesha matokeo yake chungu zaidi kuliko mahali pengine, wakati mwingine kwa uwazi. Kwa hakika, mgonjwa asipowekwa kituoni na kuzingatiwa katika hadhi yake, mitazamo huzalishwa ambayo inaweza hata kusababisha kukisia juu ya masaibu ya wengine, na hii lazima itufanye tuwe macho”.

Mmoja wa mgonjwa anayehudumia na ARIS
Mmoja wa mgonjwa anayehudumia na ARIS

Baba Mtakatifu Francisko a amesisitiza upendo wa waanzilishi wa huduma ya afya ya Kikatoliki, katika ufahamu kwamba leo hii, kwa sababu mbalimbali, inazidi kuwa vigumu kudumisha miundo iliyopo. Kwa hiyo amesema “ni muhimu kuchukua njia za utambuzi na kufanya maamuzi ya ujasiri, tukijikumbusha kwamba wito wetu ni kusimama kwenye mpaka wa hitaji: wito wetu ni kwamba, kwenye mpaka wa hitaji. Kama Kanisa, tunaitwa kujibu zaidi ya yote mahitaji ya huduma ya afya ya maskini zaidi, waliotengwa na wale ambao, kwa sababu za kiuchumi au kitamaduni, wanaona mahitaji yao hayatimiziwi. Hizi ndizo muhimu zaidi kwetu, zile ambazo ziko juu ya foleni”.

Salumu za Papa kwa wajumbe wa ARIS
Salumu za Papa kwa wajumbe wa ARIS

Papa amezungumzia kile anachokifafanua kama “kurudi kwa 'umaskini wa kiafya ambapo, ametazama uwiano muhimu nchini Italia, zaidi ya yote katika Mikoa yenye hali ngumu zaidi ya kijamii na kiuchumi.  Papa amesema “Kuna watu wanashindwa kupata matibabu kwa kukosa njia, hata kulipia tiketi ni shida”. Vile vile amekumbusha orodha ndefu sana za kungojea tiba, hata kwa ziara za haraka na za lazima na kusisitiza juu ya hitaji kubwa la utunzaji wa kati. Mtazmo wake kwa mara nyingine tena umeelekezwa kwa hiyo kwa hali ya wazee: “Mtu mzee lazima achukue dawa hizi, na ikiwa kuokoa pesa au kwa sababu hii au ni nini hawampe dawa hizi, hii ni euthanasia iliyofichwa na inayoendelea. Tunapaswa kusema hivi. Kila mtu ana haki ya kupata dawa. Na mara nyingi, ninafikiria nchi zingine, ila  Italia sijui mengi juu ya hili, katika nchi zingine ndio, ninajua, wazee ambao wanapaswa kuchukua dawa kama nne-tano na wanaweza kupata mbili tu: hii ni maendeleo ya  euthanasia, kwa sababu mtu hapewi  kile ambacho tiba inapaswa”

13 April 2023, 17:13