2023.04.11  Katika maduka ya vitabu kitabu cha Fabio Marchese Ragona kipo chenye kichwa"Watoa Pepo dhidi ya Shetani" na mahojiano ya kipekee ya Papa. 2023.04.11 Katika maduka ya vitabu kitabu cha Fabio Marchese Ragona kipo chenye kichwa"Watoa Pepo dhidi ya Shetani" na mahojiano ya kipekee ya Papa. 

Papa:shetani anatafuta kushindwa kwa mwanadamu na hawezi kufanya

Katika mahojiano maalum,yaliyomo katika kitabu “Watoa Pepo dhidi ya Shetani” cha Fabio Marchese Ragona,kipo katika maduka ya vitabu tangu 11 Aprili 2023,ambapo Papa Francisko anasisitiza: shetani daima anajaribu kushambulia kila mtu na hupanda mifarakano,hata katika Kanisa,hujaribu kugombanisha.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika mahojiano ya kipekee yaliyomo katika kitabu  chenye kichwa “Watoa Pepo dhidi ya Shetani” cha Fabio Marchese Ragona, kipo katika maduka ya vitabu tangu 11 Aprili 2023. Katika mahojiano hayo mwandishi anaanza na swali: Baba Mtakatifu, katika ushuhuda wa yule mtawa aliyepagawa, tunasoma kwamba shetani akizungumza juu yake alisema: “Ninamchukia, yeye hunisema vibaya kila wakati. Umeona ni shida ngapi ninazomletea?” Jinsi gani ya kuchukulia uthibitisho huo?

Mimi binafsi siifahamu kesi hiyo na kwa hivyo siwezi kutoa tathmini. Lakini inawezekana kabisa kwamba ninamkasirisha shetani, kwa sababu ninajaribu kumfuata Bwana na kufanya kile ambacho Injili inasema. Na hilo linamkera. Wakati huo huo hakika anafurahi ninapofanya dhambi fulani. Anatafuta kushindwa kwa mwanadamu lakini hana matumaini ikiwa kuna maombi.

Je, umewahi kushughulika moja kwa moja na watu wenye mapepo?

Nilipokuwa Askofu Mkuu huko Buonos Aires, nilipata kesi kadhaa za watu ambao walikuwa wanakuja kwangu wakisema wamepagawa. Niliwatuma kushauriana na makuhani wawili wazuri "wataalamu": sio waganga, lakini watoa pepo. Mmoja anaitwa Carlos Alberto Mancuso na alikuwa mtoa pepo katika Jimbo  La Plata. Mwingine alikuwa muungaminishi wangu, Padre Nicolas Mihaljevic, Mjesuit aliyezaliwa Kroatia. Wote wawili baadaye waliniambia kwamba kati ya watu hawa ni wawili au watatu tu ambao walikuwa waathirika wa milki ya kishetani. Wale wengine waliteseka kutokana na mkazo wa kishetani, ambao ni tofauti kabisa kwa sababu hawakuwa na shetani katika miili yao. Hii inapaswa kubainishwa.

Na kama papa, umewahi kutoa pepo?

Hapana, hilo halijawahi kutokea. Ikiwa ingetokea, ningeomba msaada wa mtoaji mzuri wa pepo, kama nilivyofanya kama askofu mkuu.

Watu kadhaa wamesema kuhusu Papa Benedikto XVI kwamba wakati wa kiti chake cha papa alipatwa na mashambulizi ya shetani,  ambaye hutujaribu kila mara,  lakini kwamba, licha ya kuteseka kutokana na hilo, alipinga vyema. Paulo VI mnamo mwaka 1972 alisema kwamba moshi wa Shetani ulikuwa umeingia katika hekalu la Mungu kupitia mpasuko fulani.  Je, kwa hiyo shetani pia anaweza kuchukua hatua  Vatican na kumshambulia papa?

Hakika shetani anajaribu kushambulia kila mtu, bila ubaguzi, na anajaribu zaidi ya yote kuwapiga wale walio na majukumu zaidi katika Kanisa au katika jamii. Hata Yesu alipatwa na majaribu kutoka kwa shetani na mtu anafikiria pia yale ya Simoni Petro ambaye Yesu alimwambia: “Ondoka kwangu, Shetani”. Kwa hiyo hata papa anashambuliwa na yule mwovu. Sisi ni wanaume na huwa anajaribu kutushambulia. Inauma, lakini mbele ya maombi hana matumaini! Na kisha ni kweli, kama Mtakatifu Paulo VI alivyosema, kwamba shetani pia anaweza kuingia katika hekalu la Mungu, ili kupanda mafarakano na kugeuza moja dhidi ya mwingine: migawanyiko na mashambulizi daima ni kazi ya shetani. Daima hujaribu kujidhoofisha ili kupotosha moyo na akili ya mwanadamu. Wokovu pekee ni kufuata njia iliyooneshwa na Kristo.

Je, tunapaswa kumwogopa shetani?

Ninadhani kuna mapepo hatari sana na ninazungumza juu ya mashetani “walioelimika”. Yesu pia anazungumza juu yao, tunasoma katika Injili ya Luka: anasema kwamba wakati roho mbaya inapofukuzwa, inazunguka jangwani kutafuta kitulizo. Lakini wakati fulani anapochoka na hivyo anarudi “nyumbani”, mahali alipokuwa amefukuzwa nje, na anaona kwamba nyumba imepangwa, ni nzuri, kama alivyokuwa ndani.

Je nini kinatokea wakati huo?

Anakwenda kutafuta pepo wengine wabaya kuliko yeye, anawaleta, wanaingia ndani ya nyumba hiyo, kwa adabu, wanapiga kengele, wanamiliki kwa njia ya adabu. Nafsi, bila kujali kuchunguza dhamiri, haioni. Au kutokana na uvuguvugu wa kiroho anawaruhusu waingie. Haya ni mabaya. Kwa sababu wanakuua. Ni milki mbaya zaidi. Roho ya Ulimwengu hufunika mambo haya yote. Hakuna kutoroka: shetani aidha anaharibu moja kwa moja kwa vita na ukosefu wa haki au anafanya hivyo kwa adabu, kwa njia ya kidiplomasia sana, kama Yesu anavyosimulia. Utambuzi unahitajika.

Papa:Shinda shetani kwa njia ya sala
11 April 2023, 14:19