Papa:ukoloni mamboleo ni mjanja,ni uhalifu na kikwazo cha amani!
Na Angella Rwezaula, -Vatican.
Ukandamizaji na unyonyaji wa watu kwa kutumia nguvu au kupenya kwa kiutamaduni na kisiasa ni uhalifu, kwa sababu hakuna uwezekano wa amani katika ulimwengu ambao unatupa idadi ya watu ili kuwakandamiza. Hii kiukweli hatakuwa kamwe na uwezekano ikiwa katika mifumo ya kisiasa ya uwakilishi haiwezea kuwa fungamani halisi ya watu waliobaguliwa, kwa njia ya mfumo sawa na na ikiwa tu nguvu za kifalme zinachukua nafasi ya kisiasa. Ameandika hayo Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake uliotolewa tarehe Mosi Aprili ambao ulielekeza kwa washiriki wa Warsha kuhusu mada ya “Ukoloni, kukomesha ukoloni na ukolonimamboleo:matazamio ya haki kijamii na wema wa pamoja” ambalo lilifanyika kwa siku mbili tarehe 30 na 31 Machi 2023 huko Casina Pio IV mjini Vatican na ambao uliandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Sayansi Jamii, Tume ya Mahakimu wa Amerika na Afrika kwa ajili ya haki kijamii na Mafundisho ya kifransiskani na Tume ya Massachusetts.
Ukoloni wa kiuchumi na kiitikadi
Katika tafakari yake Baba Mtakatifu anabainisha kuwa ingawa katika karne ya 21 hatuwezi tena kusema kitaalamu kuhusu nchi "zilizokoloniwa" kwa mtazamo wa kijiografia, hiyo haiwezi kusemwa kwa nyanja za kiuchumi na kiitikadi. Ukoloni umebadilika katika sura zake, mbinu zake, uhalali wake. Kama matukio mengine mengi ya kisiasa na kiuchumi, ni ya kweli, yanafichwa na kufanya iwe vigumu kutambua na kuondoa. Mfano hai anauchukua lakini ni kwa ajili ya nchi nyingi dunia ambapo ni kama ile ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliyoitembelea hivi karibuni. Nchi ambayo imekuwa huru kwa miaka sabini, lakini ambayo bila shaka iko chini ya hatua ambazo, wakati zinaihakikishia faida fulani, kwa upande mwingine zinahusisha unyonyaji wa rasilimali zake na athari kwa eneo, idadi ya watu na manufaa ya wote.
Wasi wasi wa Papa kuhusu ukoloni wa kiitikadi
Na kwa wasi wasi wake Papa Francisko, basi ni ukoloni wa kiitikadi, ambao unaelekea kusanifisha kila kitu kwa kufifisha mafungamano ya asili ya watu na maadili yao, kung'oa mila, historia na mafungamano ya kidini. Ni mawazo ambayo hayavumilii tofauti na yanazingatia mambo ya sasa, juu ya haki za mtu binafsi, na kupuuza wajibu kwa wale walio dhaifu na wanyonge zaidi. Ndizo tabia hizi za ukolioni mamboleo. Baba Mtakatifu anasisitiza kuwa kama ilivyo kuwa karne kadhaa za matukio ya kihistoria ya umwagaji damu na yasiyo ya kibinadamu hayajasaidia kukuza wazo la kimataifa la ukombozi, kujitawala na mshikamano kati ya mataifa na kati ya wanadamu. Sasa kila kitu ni hila zaidi na kuna hatari kwamba sababu za kweli zilizosababisha ukoloni kubadilishwa na usomaji wa kihistoria ambao unahalalisha kutawaliwa na mapungufu ya asili ya wakoloni.
Umuhimu wa sayansi na warsha ya mafunzo ya uelewa wa ukoloni mamboleo
Kwa hiyo hatupaswi kusahau kwamba maonesho madhubuti ya haki na wema wa wote hukomaa kwa watu na lazima yaheshimiwe hivyo. Historia, asili, mila, dini zote zina matokeo kwenye mantiki zinazotoa maana kwa uamuzi wa kile kilicho sawa na kizuri. Ndiyo maana hakuna mamlaka yoyote ya kisiasa, kiuchumi, kiitikadi yenye uhalali wa kuamua kwa upande mmoja utambulisho wa taifa au kikundi cha kijamii, amefafanua Baba Mtakatifu. Baba Mtakatifu baada ya kueleza umuhimu wa sayansi, taaluma na warsha ya mafunzo kwa ajili ya kuhamasisha ulewa na kupina mazoezi ya koloni mpya, ubaguzi wa rangi na kutengwa, vile vile ameomba radhi kwa matendo ya baadhi ya waamini ambao wamechangia moja kwa moja au kwa namna isiyo ya moja kwa moja michakato ya utawala wa kisiasa na kimaeneo wa watu mbalimbali wa Marekani na Afrika. Baba Mtakatifu pia ameomba msamaha wa makosa au makosa yoyote ambayo yametokea au yanayotokea kwa sasa. Kwa mujibu, wa Papa Fransisko anathibitisha tena nia yake thabiti ya kutenda, kwa mujibu wa mafundisho ya kijamii ya Kanisa, na kufanya kazi kwa ajili ya kubatilisha mchakato wa ukoloni mamboleo unaotesa ubinadamu.