Tafuta

Pasaka 2023,Papa:Rudi Galilaya mahali ulipoanzia

Fuata Yesu huko Galilaya ili ukutane naye na kumuabudu pale ambapo Yeye anasubiri kila mmoja wetu.Tuishi tena uzuri ambao mara baada ya kumgundua mzima,tulimtangaza kuwa Bwana wa maisha yetu.Turudi huko Galilaya,kila mmoja arudi katika Galilaya yake,ile ya mkutano wa kwanza na tufufuke maisha mapya!

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Usiku unataka kuisha na taa za kwanza za machweo zinatawala, wakati wanawake walikuwa njiani kuelekea katika kaburi la Yesu. Wana mashaka, wanahangaika, kwa moyo uliochanika kwa huzuni kwa sababu ya kifo kilichomchukua mpendwa. Lakini kufika mahali pale na kuona kaburi tupu, walihisi kuvunjika, walibadilisha njia; walilikimbia kaburi na kukimbia kwenda kuwatangazia wafuasi mchakato mpya: kuwa “Yesu amefufuka na anawasubiri huko Galilaya.” Ndiyo mwanzo wa maburi ya Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mkesha wa Pasaka, Jumamosi Usiku tarehe 8 Aprili 2023, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa kuudhuriwa wa waamini watakatifu wa Mungu wa ndani na nje ya nchi kwa hiyo wanaowakilisha ulimwengu wote.  Hata hivyo katika mkesha huo, Baba Mtakatifu Francisko amewabatiza wakatekumeni 8 ambao ni watu wazima na kisha kipaimara,  sakramenti ambazo ni za kwanza kuanzishwa kwa Kikristo. Hawa walikuwa watatu kutoka Albania, wawili kutoka Marekani na wengine kutoka Italia, Nigeria na Venezuela.

Papa akimbariki Shemasi ili asome Injil
Papa akimbariki Shemasi ili asome Injil

Baba Mtakatifu akiendelea na tafakari alisema: Katika maisha ya wanawake hawa Pasaka ilitokea, ambayo ina maana ya mchakato: kwani kwao kiukweli walipitia safari ya wasiwasi kuelekea kaburi la furaha, walikimbia kuelekea kwa wanafunzi ili kuwaeleza wao, si kwamba Bwana amefufuka, lakini pia kwamba kuna hatima ya kufikia haraka huko Galilaya. Mpango na Mfufuko huko pale na unapelekea Ufufuko. Kuzaliwa kwa upya kwa wanafunzi, ufufuko wao moyoni unatokea huko Galilaya. Kwa hiyo Papa ametoa mwaliko kwamba “ Tuingie hata sisi katika mchakato huu wa wanafunzi ambao walikwenda katika kaburi huko Galilaya.

Wakati wa kusoma Injili
Wakati wa kusoma Injili

Wanawake kwa mujibu wa Injili walikwenda kutembelea kaburi (Mt 28,1). Walikuwa wanafikiri kuwa Yesu anapatikana mahali pa kifo na kwamba kila kitu kilikuwa kimekwisha daima. Wakati mwingine inatokea hata sisi kufikiria kuwa furaha ya kukutana na Yesu ni ya wakati uliopita, na wakati katika wakati uliopo tunajua hasa kaburi zilizowekwa muhuri: zile za kukata tamaa, za uchungu wetu na kukosa imani, zile za kusema hakuna cha kufanya, za mambo ambayo hayabadiliki kamwe na hivyo ni bora kuishi kwa siku, kwa sababu kesho haina uhakika”. “Hata sisi ikiwa tuliguswa na uchungu, kukandamizwa na huzuni, kunyenyekezwa na dhambi, uchungu kwa sababu ya kushindwa au kuwa na wasiwasi fulani, tumefanya uzoefu wa ladha chungu ya kuchoka na tumeona furaha ya moyo ikizimika”.

Misa ya Pasaka
Misa ya Pasaka

Wakati mwingine kwa urahisi tulihisi uzito wa kupeleka mbele kila siku na kuchoka kuthubutu nafsi ya kwanza mbele ya ukuta kama wa mpira wa ulimwengu mahali ambamo utafikiri sheria daima zinazidi kuwa za kijanja na zenye nguvu zaidi. Wakati mwingine, kuwa tumehisi wasio na la kufanya na tuliokata tamaa mbele ya nguvu ya ubaya, mbele ya migogoro inayokatisha uhusiano, matinki za hesabu na kutokujali ambako utafikiri unatawala jamii, saratani ya ufisadi, kupanuka kwa ukosefu wa haki na upepo wa baridi wa vita. Na bado labda tumejikuta tunakabiliana uso kwa uso na kifo, kwa sababu tumeondolewa uwepo mtamu wa wapendwa wetu au tumejikuta katika magonjwa au katika mateso  na kwa urahisi tumebaki kulilia na kisima cha tumaini kimenyauka.  Kwa hiyo kwa hizi au hali nyingine, michakato yetu ya safari inasimama mbele ya makaburi na tunabaki tumeganda na kulia, kujililia, peke yetu na wasio na la kufanya huku tukirudia kusema, “kwa nini”.

Papa akitoa mahubiri
Papa akitoa mahubiri

Kinyume chake, wanawake wakati wa Pasaka hawakubaki wameganda mbele ya kaburi, badala yake Injili inasema: “waliliacha kaburi kwa haraka na kwa furaha kubwa, wakakimbia kutoa tangazo kwa wanafunzi wake(8). Walipeleka habari ambayo itawabadilisha maisha daima na historia: ‘Kristo amefufuka’ (6). Na wakati huo huo wanahifadhi na kuonesha taadhari ya Bwana na mwaliko wake kwa mitume kwamba: “waende huko Galilaya, kwa sababu kule watamwona”(7). Lakini ina maana gani kwenda Galilaya? Ni Mambo mawili. Kwa upande mmoja kutoka ndani ya kujifungia katika chumba cha karamu kuu ili kwenda katika mkoa wanakoishi watu (Mt 4,15), kuondoka katika kujificha ili kujifungulia utume, kundokana na woga ili kutembea kuelekea wakati ujao. Kwa upande mwingine, maana yake ni kurudi katika asili, kwa sababu ni hapo Galilaya kwamba kila kitu kilianzia. Pale Bwana alikuwa amekutana na kuwaita mitume kwa mara ya kwanza. Kwa hiyo kwenda Galilaya ni kurudi katika neema ya asili, ni kupata tena kumbukumbu ambayo inazaa tena tumaini, kumbukumbu ya wakati ujao ambao sisi tumeahidiwa na Mfufuka.

Misa ya Mkesha wa Pasaka 8 Aprili 2023
Misa ya Mkesha wa Pasaka 8 Aprili 2023

Baba Mtakatifu amesema kwamba ndiyo maana Pasaka ya Bwana inafanya hivyo: inatusukuma kwenda mbele kuondokana na maana ya kushindwa, kuviringisha jiwe mbali la kaburi ambalo mara nyingi tunapoteza tumaini, kutazama kwa imani wakati ujao, kwa sababu Kristo amefufuka na amebadili dira ya historia; lakini kwa kufanya hivyo, Pasaka ya Bwana inatupeleka katika wakati uliopita wa neema na kutufanya kwenda huko Galilaya, pale ambapo ilianza historia yetu ya upendo kwa Yesu. Anatuomba yaani kuishi tena kipindi kile, hali ile, uzoefu ule ambao tulikutana na Bwana, tumefanya uzoefu wa upendo wake na tulipokea mtazamo mmoja mpya na angavu juu yetu, juu ya hali halisi, na juu ya fumbo la maisha.

Misa ya Mkesha wa Pasaka katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Vatican.
Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro
Waamini katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba "Ili kuweza kufufuka, yaani kwa kuanza upya,  kuanza safari mpya, tunahitaji daima kurudi Galilaya yaani kwenda sio kwa Yesu wa kijujuu, wa wazo, lakini kwa kumbu kumbu hai, dhati na inayodunda mkutano wa kwanza na Yeye. Baba Mtakatifu amesema ili kutembea pamoja lazima kukumbuka; kwa kuwa na tumaini lazima kumwilishwa na kumbu kumbu. Mwaliko huo ni kukumbuka na kutembea! Ikiwa tutaweza kurudisha upendo wa kwanza, mshangao na furaha kukutana na Mungu, utakwenda mbele. Kumbuka na tembea. Kumbuka Galilaya na tambea kuelekea Galilaya. Ni mahali ambapo ulimtambua Yesu binafsi, mahali ambapo Yeye kwako hakubaki mtu wa kihistoria kama wengine, lakini amekuwa mtu wa maisha: sio Mungu wa mbali, lakini Mungu wa karibu, ambaye anakufahamu zaidi ya yeyote yule na anakupenda zaidi ya mwingine yeyote.  

Ubatizo wa wakatekumeni
Ubatizo wa wakatekumeni

Baba Mtakatifu ameomba waamini wafanye kumbu kumbu ya Galilaya, Galiya yako; ya wito wako, Neno lile la Mungu ambalo kwa wakati sahihi alizungumza na wewe hasa: uzoefu ule wa nguvu katika Roho, wa furaha kubwa ya msamaha iliyohisiwa baada ya kutubu, ya wakati ule wa kina na usiosahulika wa sala, ule wa mwanga ambao uliwaka ndani na ukakubadilisha maisha yako, mkutano ule, na hija ile". Kila mmoja wetu anajua eneo lake ndani la ufufuko, lile la kwanza, lile la kina na lile ambalo lilikubadilisha maisha. Rudi katika mkutano ule wa kwanza. Jiulize jinsi gani unauhisha leo hii. Rudi katika wakati ule wa kwanza wa mkutano. Jiulize jinsi gani ilikuwa na wakati ulikuwa namna ya kukarabati katika muktadha huo, muda na mahali, jaribu kuhisi hisia zile na kuziishi rangi na ladha. Kwa sababu ni pale unaposahau upendo ule wa kwanza ni pale unaposahau mkutano wa kwanza na ambao ulianza kuingiza vumbi ndani ya moyo wako.

Ubatizo wa wakatekumeni
Ubatizo wa wakatekumeni

Na ulifanya uzoefu wa huzuni na kama ilivyo kwa wanafunzi kila kitu kilikuwa bila matarajio, kwa kuziba matumaini. Lakini leo hii nguvu ya ufufuko anakualika kuviringisha kutoa uzito wa kukata tamaa na imani; Bwana, mtaalamu wa kuondoa jiwe kubwa la dhambi na hofu, anataka kumulika kumbu kumbu yako takatifu, kumbu kumbu yako nzuri zaidi, kuifanya sasa ya mkutano wa kwanza na Yeye. Kumbuka na kutembea: rudi Kwake, upate neema ya ufufuko wa Mungu ndani mwako! Baba Mtakatifu ameomba "kufuata Yesu huko Galilaya ili ukutane naye na kumuabudu pale ambapo Yeye anasubiri kila mmoja wetu, Tuishi tena uzuri wa ambao mara baada ya kumgundua mzima, tulimtangaza kuwa Bwana wa maisha yetu. Turudi huko Galilaya, kila mmoja arudi katika Galilaya yake, pale pa mkutano wa kwanza na tufufuke maisha mapya!

Tafakari ya Papa katika Mkesha wa Pasaka
08 April 2023, 21:30