Ujumbe wa Papa wa Pasaka 2023 kwa Urbi Et Orbi:migogoro bado inashamiri

Katika ujumbe wake Papa Francisko ambao kiutamaduni hutolewa kwa ulimwengu,amegusia uharaka wakukutana na Bwana,hasa watu wenye shida,ili kushinda migawanyiko na migororo,kuanzia vita nchini Ukraine na Urussi.Siria,DRC,Sudan Kusini,Ethiopia,Eritrea,Haiti,Bukrina Faso,Mali, Msumbiji,Nigieria,Nicaragua na Myanmar.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Leo tunatangaza kuwa Yeye, Bwana wa maisha yetu ni “ufufuko na uzima” wa ulimwengu(Yh11,25). Ni Pasaka ambayo ina maana ya “mapito”, kwa sababu katika Yesu ilitimizwa hatua stahiki ya ubinadamu, ile ya kutoka katika kifo hadi uzima, kutoka katika dhambi hadi neema, kutoka katoka hofu, hadi imani, upweke hadi muungano. Katika Yeye, Bwana wa wakati  na wa historia ndiye ninataka kuwambia wote kwa furaha ya mouo: Pasaka Njema. Ndivyo Baba Mtakatifu alianza ujumbe wake wa  Urbi et Orbi kwa mwaka 2023, kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika ya Pasaka tarehe 9 Aprili 2023.

Kilichojiri wakati wa misa ya Pasaka 9 Aprili 2023

Baba Mtakatifu amesema iwe kwa kaka na dada wote kwa namna ya pekee kwa ajili ya wagonjwa, na maskini, kwa ajili ya wazee na kwa yule ambaye anapitia wakati wa majaribu na ugumu, mapito kutoka katika mahangaiko hadi faraja. Hatuko peke yetu: Yesu, aliye mzima yuko nasi daima. Kanisa lifurahi na ulimwengu, kwa sababu leo hii matumaini yetu yasibamizwe tena dhidi ya ukuta wa kifo, lakini Bwana ametufungulia daraja kuelekea maisha. Baba Mtakatifu amesema kuwa wakati wa Pasaka, hatima ya ulimwengu imebadilika na leo hii ni sambamba hata na tarehe ambayo inasadikika ilikuwa ya Ufufuko wa Kristo, kwa hiyo tunaweza kufurahi kusherehekea neema, siku muhimu zaidi na nzuri ya historia.

Wakati wa Baraka ya Urbi et Orbi 9 Aprili 2023
Wakati wa Baraka ya Urbi et Orbi 9 Aprili 2023

Kristo amefufuka, ni kweli amefufuka, kama wanavyotangaza katika Makanisa ya Mashariki. Kweli ile ambayo wanasema kuwa tumaini sio udanganyifu ni ukweli! Na kwamba safari ya ubinadamu kuanzia Pasaka na kuendelea imepitiwa na tumaini na kuendelea zaidi kwa haraka. Mashuhuda wa kwanza wa ufufuko  wanatuonesha  mfano wao. Injili zinasimulia haraka nzuri iliyokuwa ya siku ya Pasaka, wanawake walikimbia kwenda kutoa tangazo kwa wanafunzi (Mt 28,8). Na baadaye hata Maria Magdalena alikimbea kwa Simoni Petro (Yh 20,2). Yohane na pia Petro walikimbia pamoja wote wawili ili kufika mahali ambapo Yesu alikuwa amezikwa. Na baadaye kuna usiku wa Pasaka,, kukutana na Mfufuka juu ya Njia ya Emmaus, wote wawili walikimbia bila kusita (Lk 24,33) na waliharakishi kukimbia kwa kilometa katia mpando na giza wakiwa na furaha isiyoisha ya Pasaka ambayo ilikuwa inawaka katika mioyo yao (Lk 24,32).

Papa akiwa kwenye Balkoni ya kutolea Baraka ya Urubi Et Orbi 2023
Papa akiwa kwenye Balkoni ya kutolea Baraka ya Urubi Et Orbi 2023

Ni furaha hiyo hiyo ambayo Petro wakati yuko kwenye ziwa la Galilaya baada ya kumwona Yesu Mfufuka hasingeweza kuitunza katika mtumbwi na wengine, lakini alijitupa haraka katika maji ili kuogelea kwa haraka akutane naye (Lk Gv 21,7). Kwa hiyo wakati wa Pasaka, mchakato wa safari unaendelea na kugeuka kuwa mbio kwa sababu ubinadamu unatazama hatma ya mchakato wake,  kwa maana ya hatma ya Yesu Kristo na anayeita kuharakisha kukutana na Yeye  tumaini la Ulimwengu.

Papa kibariki waamini
Papa kibariki waamini

Tuharakishe hata sisi kukuta katika safari ya imani ya pamoja: imani kati mtu, kati ya watu na mataifa. Tuache tushangazwe tangazo jema la Pasaka , kutoka katika mwanga unaoangaza usiki na giza ambamo mara nyingi dunia inajikuta imegubikwa humo. Tuharakisha kushinda migogoro na migawanyiko na kufungua mioyo yetu kwa wale wenye shida zaidi. Tuharakishe kupitia nyayo za amani na za udugu. Tufurahie kwa  ishara za dhati za tumaini ambazo zinatufikia kutoka kwenye nchi nyingi, kuanzia na wale ambao wanateseka katika maisha na kukarimu wale wanaokimbia vita na umaskini. Lakini katika safari ndefu kuna mawe mengi ya kujigonga ambayo yanafanya kuwa ngumu na kuzuia kukimbilia kuelekea Mfufuka.

Baraka ya Papa Francisko
Baraka ya Papa Francisko

Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba “Kwake yeye tumwelekeze maombi kwamba tusaidie kukumbilia kukutana na wewe! Tusaidie kufungua mioyo yetu! Wasaidie watu wapendwa wa Ukraine katika mchakato wa safari kuekelea amani, na ulete mwanga wa Pasaka juu ya watu wa Urussi. Wafariji waliojeruhiwa na wale ambao wamepoteza wapedwa wao kwa sababu ya vita na ufanye kwamba wafungwa waweze kurudi na afya na salama katika familia zao. Fungua mioyo ya jumuiya nzima ya Kimataifa ili waweza kufanya kufikia mwisho wa vita hivi na migogoro yote ambayo inatoa damu ulimwenguni kuanzia na Siria, ambao bado wanasubiri amani. Wasaidie ambao wamekumbwa na tetemeko la nguvu huko Uturuki na vile vile Siria. Tusali kwa ajili ya wale waliopoteza familia na marafiki na wale wasio na nyumba, ili waweze kupata faraja kutoka kwa Mungu na kutoka kwa msaada za mataifa.

Uwanja ulivyopambwa maua ya Pasaka
Uwanja ulivyopambwa maua ya Pasaka

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba: Katika siku hii tunakukabidhi Bwana, mji wa Yerusalemu, shuhuda wa kwanza wa ufufuko wako. Maonesho hai ya wasi wasi na mashambulizi ya siku hizi za mwisho ambayo yanahatarisha hali halisi ya imani na heshima ya pamoja, kuna ulazima kwa ajili ya kuanza  kwa upya majadiliano kati ya Israeli na Palestina na hivyo kwamba amani iweze kutawala katika Mji Mtakatifu na katika Kanda nzima.

Papa anavyoonekana katika maua
Papa anavyoonekana katika maua

Baba Mtakatifu Francisko ameendelea na sala kwamba “Bwana saidia Lebanon ambayo bado inatafuta kuwa na msimamo na umoja kwa sababu iweze kushinda migawanyiko na wazalendo wote wafanye kazi pamoja kwa ajili ya wema wa pamoja wa Nchi. Aidha hatuwezi kusahahu watu wapendwa wa Tunisia, kwa namna ya pekee vijana na wale ambao wanateseka kwa sababu ya matatizo ya kijamii na kichumi, ili wasipoteze matumaini na wafanye kazi kwa ajili ya kujenga wakati ujao wa amani na udugu. Inua mtazamo wako kwa ajili ya Haiti, ambayo inateseka kwa miaka mingi katika mgogoro wa kijamii, kisiasa na kibinadamu na usaidie jitihada za wadau wa kisiasa na wa Jumuiya ya Kimataifa katika kutafuta suluhisho la mwisho kwa walio wengi wenye matatizo yanayosumbua watu ambao tayari wameangaika.

Walinzi wa Kipapa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Misa
Walinzi wa Kipapa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Misa

Imarisha michakato ya amani na mapatano yaliyoanzishwa huko Ethiopia na Sudan Kusini na ufanye kwamba vurugu ziishe huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wasaidie Bwana Jumuiya za Kikristo ambazo leo hii zinasheherekea Pasaka katika muktdha maalum kama vile Nicaragua, na Eritrea, na wakumbushe wote ambao wamezuiwa kukiri imani yao kwa uhuru na adharano imani yao. Uwape nguvu waathirika wa shambulizi la kigaidi kimataifa, hasa nchini Burkina Faso, Mali, Msumbiji na Nigeria.

Umati wa waamini wakiwa wamekaa katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati wa waamini wakiwa wamekaa katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Saidia Myanmar ili ipitie njia za amani na angaza mioyo ya wahusika ili huko Rohingya inayoteseka ipate haki. Wape nguvu wakimbizi, waliochukuliwa, wafungwa kisiasia, na wahamiaji hasa wale walio katika mazingira magumu, na zaidi wale wote ambao wanaoteseka na njaa, umaskini na matokeo mabaya ya madawa ya kulevya, biashara haramu ya watu na kila aina ya utumwa. Waongoze Bwana wahusika wa mataifa, kwa sababu pasiwepo mwanamme na mwanamke yoyote anayebaguliwa na kukanyagwa hadhi yake; kwa sababu katika heshima kamili ya haki za binadamu na ya demokrasia , yaponeshwe majeraha ya kijamii, na kutafuta tu daima na wema  wa pamoja wa wazalendo, wawakikishie usalama na hali ya lazima kwa ajili ya majadiliano na kuishi kwa amani kwa pamoja.

Viongozi  mbali mbali wa serikali na kimataifa wameudhuria misa
Viongozi mbali mbali wa serikali na kimataifa wameudhuria misa

Baba Mtakatifu akiendelea amesema “Hata sisi tupatie  safari ya haki, ili kuharakisha mapigo ya tumaini, tutamani uzuri  wa mbingu. Tuchote leo hii nguvu ya kwenda mbele katika wema wa kukutana na wema ambao haukatishi tamaa. Na ikiwa kama alivyo andika Baba wa zamani,kwamba “dhambi kubwa zaidi ni ile ya kutokuamini nguvu ya Ufufuko (Mtakatifu Isack wa Ninawi), Leo hii “Ndio tuna uhakika kwamba: Kristo kweli amefufuka. Tunaamini Kwako Bwana Yesu, tunaamini ya kwamba kuwa  na Wewe Tumaini linazaliwa na safari inaendelea- Wewe Bwana wa uzima, tia moyo safari zetu na rudia hata kwetu, kama ulivyosema kwa wanafunzi katika usiku wa Pasaka “ Amani iwe kwenu (Yh 20,19.21).

Baraka ya Urbi et Orbi ya Papa Francisko, tarehe 9 Aprili 2023
09 April 2023, 12:30