Yohane XXIII alieleza wote kuwa “Pacem in terris”
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Alama bora inahitaji dokezo lake la kwanza ili kuwa kazi bora. Ujumbe wa kwanza wa Pacem in terris Pacem in terris ambao ni kazi nzuri ya Papa Yohane XXIII unasikika katika ujumbe wa radio, usio na urefu wa mistari 20, na usioweza kulinganishwa na waraka ambao utatolewa miezi sita baadaye. Mwandishi wa Vatican News Alessandro De Carolis kuwa bado ujumbe huo unakuwa ujumbe wa kwanza ambao tayari unakuwa ni hati nzima inayoamsha shukrani kubwa ya kimataifa, upinzani na mijadala na ambao inabaki kuwa msingi wa mafundisho ya Papa juu ya amani kwa miaka 60 baada ya uchapishaji wake. Kwa hiyo katika kuadhimisha miaka 60 tangu kuchapishwa kwa Waraka wa Pacem in terris, mnamo tarehe 11 Aprili 1963, tunapendekeza tena maneno ambayo Papa Roncalli alitamka siku ya kutiwa saini kwake na katika uingiliaji kati na mikutano mbalimbali zilizofuata, tukimulika mambo mapya na mambo ya waraka huo ambayo yalikuwa karibu sana moyoni mwake. Ni tarehe 25 Oktoba 1962 siku ya mgogoro wa makombora ya Cuba kati ya Marekani na Urussi …. Siku moja kabla mfumo wa taadhari wa marekani ulikuwa umepita huko DEFCON 2, ambao mara moja chini ya vita vya atomiki, na hivyo wakati ulimwengu unatetemeka, Yohane XXIII aliamua kuelekeza maombi ya kweli kwa wale wahusika wa mamlaka. Alizungumza kwa lugha ya kifaransa, lugha ya kidiplomasia kimataifa, akinukuu wazo ambalo alikuwa ameelekeza katika mantiki nyingine na ambao ulikuwa unasikika hivi:
Mikono juu ya dhamiri…
“Kwa mkono juu ya dhamiri, wasikilize kilio cha huzuni ambacho kila pande ya dunia, kuanzia na watoto wasio na hatia hadi wazee, kuanzia na watu binafsi hadi jumuiya, amani inapaa mbinguni: amani! Amani”.
Baadaye kwa wazo akiwa amepiga magoti alirudia: Tuombee serikali zisibaki viziwi katika kilio cha ubinadamu
Papa Ronacalli: ndio maana ni mpya
Kama wanahistoria walivyopanua hati hiyo, maneno hayo yanaoendana na mchakato bunifu wa haraka sana. Monsinyo Pietro Pavan, mtaalamu wa mafundisho ya kijami ya Kanisa wa Yohane Paulo II aliyemuunda kuwa Kardinali aliandika rasimu ya Waraka wa Papa Roncalli na kuuweka chini ya uangaliz ili andiko hilo liweze kuotolewa tarehe 11 Aprili 1963. Tangu wakati hu ona zaidi tangu saini , Yohane XXIII hakukosa fursa ya kuzunguzia hati, kwa kuweka juu yake baadhi ya mantiki ambayo baada ya miaka 60 ni vizuri kuyasoma na kusikiliza.
Siku mbili kabla tarehe 9 Aprili, Jumanne Takatifu, Papa katika hotuba yake fupi wakati wa kutia saini katika Waraka, alijifanya kama msimuliaji akielekeza kati ya mengine, habari mbya kuu zaidi ya Pacem in Terris na kwa sababu , uchaguzi wa kuelelezea sio tu kwa waamini lakini hata kwa kila mtu, kitu ambacho hakikuwa kimefanyika kwa wakati uliopita: Hii inaelezea uvumbuzi unaofaa kwa hati hii, iliyoshughulikiwana sio tu kwaajili ya uaskofu wa Kanisa la ulimwengu wote, kwa wakleri na waamini wa ulimwengu wote, lakini pia “kwa watu wote wenye mapenzi mema”. Amani ya ulimwengu wote ni nzuri ambayo inavutia kila mtu bila ubaguzi; kwa hivyo tumefungua mioyo yetu kwa wote.
Mkirudi nyumbani pelekeni amani nyumbani
Tarehe 13 Aprili mwaka huo ilikuwa ni Dominika ya Ufufuko na Yohane XXIII alienea ujumbe mrefu kwa njia ya Radio ambo ulipata nafasi ya kufikiria juu ya Waraka ambao ulikuwa umechapishwa. Neno amani liliruda kwa mara therathini , Papa Roncalli alifafanua Pacem in terris “ kama zawadi yetu ya Ufufuko wa mwaka wa Bwana 1963 na kuhitimishwa na sala ambayo ilikuwa kwa upya kama wito wake wa kwanza kwa watawala: Waangazie watawala wa watu, ili, pamoja na kujali kwa haki kwa ustawi wa ndugu zao, wahakikishe na kulinda hazina kuu ya amani; huwashe nia ya kila mtu ili kushinda vikwazo vinavyogawanyika, kuimarisha vifungo vya upendo wa pande zote, ili kuwa tayari kuelewa, kuhurumia na kusamehe.
Ilikuwa imepita karibu majuma mawili, tarehe 24 Aprili, ambayo ilikuwa ni siku ya katekesi ambapo tarehe 9, Aprili, Papa mwema alikuwa amekiri kwa hisia kali, kuhusiana na Waraka, mbele ya watu waliokuwa wanamsikiliza katika Kanisa Kuu, akishirikisha furaha kubwa, kwa mwangwi wa sauti chanya ambazo zilikuwa zikilifika. Alieleza kuwa uchaguzi ambayo ilimfanya kuchapicha Alhamisi Kuu kuwa inaendana na Ujumbe wa Yesu kwa wanafunzi katika karamu kuu. “Ninawaachia amani, ninawapa amani”, kwa hiyo alizindua pendekezo ambalo linasisitiza na maneno yake ambayo tayari yalikuwa yanaelezwa kuwa ni hotuba mnamo tarehe 11 Oktoba 1962, usiku wa ufunguzi wa Mtaguso:
Mkirudi katika nchi zenu, nyumbani kwenu, muwe wachukuaji wa amani kila mahali: amani na Mungu katika patakatifu pa dhamiri; amani katika familia; amani katika taaluma; amani na watu wote, kwa kadiri hivyo inavyowategemea ninyi: kwa njia hii mtahakikishiwa heshima na shukrani ya wote, na neema za Mbingu na nchi. Daima muwe wasafiri wa amani!
Katika akili na katika mioyo ya wote
Yohane XXIII alikuwa na furaha lakini akiwa amejaribiwa sana na ugonjwa na uchovu. Hata hivyo alikuwa na namna ya kurudi kuzungumzia waraka wa Pacem in terris ambao utakuwa wa mwisho wa jitihada zake rasmi, ambapo tarehe 11 Meio katika Ikulu kwa ajili ya kutunukiwa kwa upande wa Rais wa Italia bwana Antonio Segni , tuiz ambayo ilitolewa na Mfuko wa Balzan, “kwa ajili ya ubinadamu , amani na udugu kati ya watu”.
Siku moja kabla katika muktadha huo , kulikuwa kumefanyika matukio mawili, moja katika ukumbi wa Jumba la Kitume na jingine katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, wakiwepo makardinali na watu mashuhuri tofauti katika ulimwengu wa kitaaluma na sayansi. Katika mikuntano miwili ya kwanza, akimshukuru Waziri Mkuu, Papa Roncalli aliweza kuomba kwa imnai kusoma kile ambacho kinatokea: Matarajio ya amani ya haki, ambayo sisi ni mashuhuda wenye furaha leo, yamepenya akili na mioyo ya wote, bila tofauti, lakini kwa msisitizo mkubwa zaidi, utafikiri ndani ya madarasa ya kazi.
Kwa hivyo, amani sio tena haki ya dhamiri ya “watawala wa watu” tu, lakini ufahamu ambao unaonekana kuwa umepanua msingi wake, ambao sasa unahusisha pia watu wa kawaida, kwa hakika shukrani kwa mwangwi ambao waraka ulikuwa nao. Siku ishirini na nne baadaye John XXIII anakufa, lakini alama ya Pacem terris yake inabakia kuwa nota ya ulimwengu wote. Imebaki hivyo tangu ujumbe wa kwanza mfupi wa radio wa 1962, ambao leo hii unarejea kuwa kama mwangwi wa maombi mengi ya Papa Francisko kwa viongozi wa jumuiya ya kimataifa, katika enzi ya vita vya dunia vilivyogawanyika vipande vipande duniani. Tuache tufanye kila tuwezalo kuokoa amani. Kwa hivyo tutaepusha ulimwengu maovu ya vita ambayo matokeo yake ya kutisha hakuna anayeweza kutabiri.