Hotuba ya Papa,Hungaria:Siasa zimesahau ukomavu uliofikiwa

Papa Francisko akiwa na msafara wake baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Budapest alikaribishwa kwa heshima zote kitaifa.Amezungumza na viongozi wa Serikali,vyama vya kiraia pamoja na wanadiplomasia nchini Hungaria ambapo ameuliza:“juhudi za kutafuta amani ziko wapi?

Na Angella Rwezaula;- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 28 Aprili 2023, hatimaye katika ziara yake ya 14 ya Kitue nchini Hungaria mara baada ya kukaribishwa kwa heshima kuu na kutambulisha, Rais wa Jamhuri ya Hungaria Bi Katalin Novak alisalimiana pia na viongozi wake na kutoa hotuba kwa viongozi wa Serikali, vyama vya kiraia pamoja na wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi na mashirika ya Kimataifa katika nchi ya Hungaria. Baba Mtakatifu Francisko ameanza na shukrani kwa Rais kwa makaribisho na maneno ya hotuba yake. Ameanza na: Mji wa historia. Nchi hiyo yenye asili ya kizamani, kama wanavyoushuhudia mambo mengine ya kizamani yanayobaki ya Historia ya Celtic na kirumi.  Hata hivyo, fahari yake Papa amesema inarudisha kwenye hali ya kisasa, ilipokuwa mji mkuu wa Milki ya Austria-Hungaria wakati wa kipindi hicho cha amani kilichojulikana kama uzuri wa kipindi kilichoendelea hadi Vita vya Kwanza vya Dunia. Wakati huo nchi ilijua wakati wa amani, imejua migogoro yenye uchungu: si tu uvamizi wa nyakati za mbali lakini, katika karne iliyopita, jeuri na ukandamizaji uliosababishwa na udikteta wa Kinazi na Kikomunisti na inawezekanaje  kusahau 1956?

Hotuba ya Papa kwa Hungaria
Hotuba ya Papa kwa Hungaria

Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa wakati wa Vita vya Kidunia vya pili, walijuwa kufukuzwa kwa makumi na makumi ya maelfu ya wakaazi, pamoja na idadi iliyobaki ya asili ya Kiyahudi iliyofungwa kwenye ghetto na kukabiliwa na mauaji mengi. Katika muktadha huo kumekuwa na watu wengi waadilifu jasiri – Papa Francisko amemfikiria Balozi Angelo Rotta  ambaye alikuwa na  ujasiri mwingi na dhamira kubwa ya kujenga upya, ili leo hii ya Budapest ni moja ya miji ya Ulaya yenye asilimia kubwa ya Wayahudi, kituo hicho cha nchi inayojua thamani ya uhuru na ambayo, baada ya kulipa gharama kubwa kwa udikteta, inabeba ndani yake dhamira ya kulinda hazina ya demokrasia na ndoto ya amani. Baba Mtakatifu Francisko amekazia kuhusu kuanzishwa kwa mji wa Budapest , ambapo mwaka huu wanasheherekea. Kwa hiyo nchi hiyo inasheherekea miaka 150 yaani mnamo mwaka 1873 kutoka katika miji mitatu ya Buda na Obuda huko Magharibi ya Danubio na Pest, iliyokaribu na mto. Kuzaliwa kwa mji mkuu huo katika moyo wa bara Ulaya unakumbusha safari ya umoja ambao ulifuatwa kutoka Ulaya, katika ule wa Hungaria unapata maisha hai.  Baada ya vita ya Pili, iliwakikisha pamoja katika Umoja wa mataifa, matumaini makubwa katika lengo la pamoja ambalo linahusiana kati ya Mataifa ambayo yalikuwa yamezuka migogoro.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kwamba katika ulimwengu ambamo tunaishi, lakini hamu ya kisiasa ya umoja na kwa ajili ya wingi wa utamaduni utafikiri nikumbu kumbu iliyopita: utafikiri ni kutazama mawio ya huzun katika ishara ya pamoja ya amani, wakati nafasi zinafanyika zile za vita. Kwa ujumla kuna utofauti sana kati ya shauku za kujenga umoja wa mataifa ya amani na thabiti, wakati katika sehemu zinaonesha mateso, uzalendo huvuma tena na hukumu na sauti zinatiwa chumvi kwa wengine. Katika ngazi ya kimataifa hata inaonekana kwamba siasa ina athari za kuchochea roho badala ya kutatua matatizo, na kusahau ukomavu uliofikiwa baada ya vitisho vya vita na kurudi kwenye aina ya watoto wachanga wa vita. Lakini amani kamwe haitatoka kwa kufuata masilahi ya kimkakati wa mtu binafasi, bali kutoka kwa sera zenye uwezo wa kuangalia kwa ujumla, maendeleo ya kila mtu: makini kwa watu, maskini na ya kesho; si tu kwa uwezo, mapato na fursa za sasa.

Papa akihutubia Nchi ya Hungaria
Papa akihutubia Nchi ya Hungaria

Katika wakati huu wa kihistoria, Ulaya ni ya msingi. Kwa sababu, shukrani kwa historia yake, inawakilisha kumbukumbu ya ubinadamu na kwa hivyo inaitwa kuchukua jukumu linalolingana nayo: lile la kuunganisha walio mbali, la kuwakaribisha watu ndani yake na kutomwacha mtu yeyote adui milele. Kwa hivyo ni muhimu kugundua tena roho ya Ulaya: shauku na ndoto ya Mababa waanzilishi, viongozi wa serikali ambao wameweza kutazama zaidi ya wakati wao, nje ya mipaka ya kitaifa na mahitaji ya haraka, na kutengeneza diplomasia zenye uwezo wa kurekebisha umoja, sio kupanua mpasuko.  Baba Mtakatifu amemfikiria De Gasperi aliyesema kwenye meza ya mduara ambayo Schuman na Adenauer pia walishiriki kwamba: “Ni kwa ajili yake yenyewe, sio kupingana na wengine, kwamba tunatetea Ulaya iliyoungana ... tunafanya kazi kwa umoja, si kwa mgawanyiko.”(Hotuba katika kwenye meza ya mduaria Ulaya, Roma, 13 Oktoba 1953). Na tena, kulingana na kile ambacho Schuman alisema: “Mchango ambao Ulaya ilipangwa na muhimu unaweza kutoa  ustaarabu ambao ni muhimu kwa kudumisha uhusiano wa amani”, kwa hiyo haya ni maneno ya kukumbukwa! “Amani ya ulimwengu inaweza kulindwa tu kwa juhudi za ubunifu, sawia na hatari zinazotishia” (Azimio la Schuman, 9 Mei 1950). Baba Mtakatifu amsema “Katika awamu hii ya kihistoria kuna hatari nyingi; lakini, nashangaa, hata kufikiria Ukraine iliyopigwa, ziko wapi juhudi za ubunifu za amani?”

Ziara ya Papa nchini Hungaria 28-30 aprili 2023

Kwa hivyo, Papa amefikiria Ulaya ambayo si mateka wa vyama, ikiangukia katika mawindo ya umaarufu wa watu binafsi, lakini ambayo haijibadili yenyewe kuwa kioevu, ikiwa si gesi, ukweli, katika aina ya udhabiti usio na maana, usiojali maisha ya watu. Hii ni njia chafu ya ‘ukoloni wa kiitikadi’, ambayo huondoa tofauti, kama ilivyo kwa kile kinachojulikana kama tamaduni ya kijinsia, au kuweka dhana za kupunguza uhuru kabla ya ukweli wa maisha, kwa mfano kwa kujivunia kama ushindi "haki ya ya  kutoa mimba”, ambayo huwa ni kushindwa kwa kutisha. Kinyume chake kwa upande mwingine, ni ajabu jinsi gani kujenga Ulaya inayozingatia mtu na watu, ambapo kuna sera madhubuti za kiwango cha kuzaliwa na familia, zinazofuatiliwa kwa uangalifu katika nchi hii, ambapo mataifa tofauti ni familia ambayo ukuaji huo unakua na upekee wa kila mmoja huhifadhiwa. Daraja maarufu zaidi huko Budapest, lile la minyororo, hutusaidia kuwazia Ulaya liyotengenezwa kwa pete nyingi tofauti kubwa, ambazo hupata uimara wao katika kuunda uhusiano thabiti pamoja. Katika hili  Baba Mtakatifu amesema imani ya Kikristo husaidia na Hungaria inaweza kutenda kama ‘daraja’, ikitumia tabia yake maalumu  ya kiekumene: hapo madhehebu mbalimbali yanaishi pamoja bila uadui, yakishirikiana kwa heshima, na roho ya kujenga. Kwa akili na moyo wangu ninaenda kwenye Abasia ya Pannonhalma, mojawapo ya makaburi makubwa ya kiroho ya nchi hiyo, mahali pa sala na daraja la udugu.

Baba Mtakatifu Francisko katika kipengele cha tatu, ameelezea muktadha wa mji wa Budapest kuwa ni wa watakatifu, kama ilivyokuwa inaonesha hata Picha kubwa kwenye ukumbi ule. Wazo la kwanza lilimwendea Mtakatifu Stefano; Mfalme wa Kwanza wa Hungaria, aliyeishi kipindi cha wakristo wa wa Ulaya ambao walikuwa wanaelewana Ulaya; Sanamu yake ndani ya Nyumba ya Kifalme ya Buda, inaendelea na kulinda mji wakati katika Kanisa Kuu lililowekwa wakfu katika Moyo wa Mji mkuu ni pamoja na ule wa Esztergom, Jengo kubwa sana la kidini katika Nchi. Kwa hiyo Historia ya Hungaria inazaliwa na utakatifu, na sio tu mfalme lakini kwa familia nzima; mke wake mwenyeheri Gisella, na mtoto wake Mtakatifu Emerito. Ushauri wa baba yake ambao unaunda kama mirathi ya kiroho kwa watu wa Hungaria ni maneno yanayofaa kwa wakati huu kwamba: Napendekeza kwamba uwe mwema, si kwa jamaa yako tu na jamaa yako, au kwa wenye nguvu na matajiri, au kwa jirani yako na wenyeji wako, lakini pia kwa wageni." Mtakatifu Stefano anahamasisha haya yote kwa roho ya kweli ya Kikristo, akiandika: "Ni mazoezi ya upendo ambayo husababisha furaha kuu". Na anamalizia kwa kusema: “Kuweni wapole ili msije mkapigana na ukweli” (Mawaidha, X).

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amesema, hayo hayawezi kutengenishwa na ukweli na upole. Ni mafundishi makubwa ya imani: thamani za kikristo hawezi kushuhudiwa kwa njia ya ugumu na kujifunga, kwa sababu Ukweli wa Kristo unapelekea upole, ukarimu katika roho za heri. Unasimika mizizi katika wema wa watu wa Hungaria, ulioonesha na aina fulani ya kuzungumza kwa pamoja kwa mfano  “jónak lenni jó” [è bene essere buoni] e “jobb adni mint kapni” [ni vizuri kutoa kuliko kupokea). Kutokana na hilo hung’aa sio tu utajiri wa utambulisho thabiti, bali hitaji la uwazi kwa wengine, kama Katiba inavyosema: “Tunaheshimu uhuru na utamaduni wa watu wengine, tumejitolea kushirikiana na mataifa yote ya dunia". Inasema zaidi: "Watu wachache wa kitaifa wanaoishi nasi ni sehemu ya jumuiya ya kisiasa ya Hungaria na ni sehemu za serikali", na inapendekeza kujitolea "kwa ajili ya utunzaji na ulinzi [...] wa lugha na tamaduni [...] ya watu wachache wa kitaifa nchini Hungaria". Mtazamo huu ni wa kiinjili kweli, ambao unatofautisha mwelekeo fulani, wakati mwingine unaohesabiwa haki kwa jina la mapokeo ya mtu mwenyewe na hata imani, kujiondoa ndani yako mwenyewe.

Papa Francisko huko Hungaria
Papa Francisko huko Hungaria

Baba Mtakatifu Francisko aidha amewashukuru kwa sababu ya kuhamasisha matendo ya upendo na elimu inayotakana na thamani na ile ambayo inajikita katika makampuni ya kikatoliki mahalia na kama ilivyo msaada wa dhati kwa wakristo wengi waliojaribiwa ulimwenguni hasa nchini Siria na Lebanon. Ni matunda ya ushirikiano kati ya Serikali na Kanisa ambayo ili kuwa hivyo, lazima lakini kuwa makini hata hivyo, inahitaji kulinda tofauti zinazofaa. Ni lazima kwamba kila mkristo akumbuke hili, kwa kuzingatia Injili, kuwa na chaguzi huru ambazo zinaokoa za Yesu na kuwa makini juu ya mantiki za madaraka. Itakuwa vizuri kuwa na mtazamo wa uzuri wa kilei ambao auangukii kwenye tabia za ulei ulioibuka, ambao unajionesha  kudharau mantiki ya kitakatifu  na baadaye kuweka dhabihu juu ya altare za faida “Yeyote anayejiita Mkristo akisindikizwa na mashahidi wa imani, kimsingi anaitwa kushuhudia na kutembea na kila mtu, akikuza ubinadamu unaovuviwa na Injili na kuweka njia mbili kuu: kujitambua kuwa watoto wapendwa wa Baba na upendo kila mmoja kama ndugu. 

Ni mada ambayo ya ukarimu ambao umekuwa na madala mkubwa katika siku zetu na ni uhakika mgumu. Licha ya hayo Baba Mtakatifu amesema  Kwa Mkristo, tabia ya kina haiweza kuwa tofauti na ile ambayo Mtakatifu Stefano alionesha baada ya kumtambua Yes una ambayo inajitofautisha na mgeni wa kukaribishwa ( Mt 25,35). Na kwa kufikiria Kristo aliyepo kwa kaka na dada wengi wanaohanika na ambao wanakimbia migogoro, umakini, na mabadiliko ya tabia nchi na ambao unahitaji kubalina na shinda  bila kukweli na shaka. Ni mada ya kukabiliana kwa pamoja, kwa jumuiya hata kwa sababu katika muktadha ambao tunaishi, matukeo ya kwanza ua baadaye yatawagusa wote. Kwa hiyo ni hataka kama Ulaya , kuanya kazi katika njia salama na haliali  katika mfuko shirikisho wa kukabiliana changamoto ya sasa ambaye haiwezekani kuisitisha kwa kuisukuma bali kuipokea na kuandaa wakati ujao ambao ikiwa sio pamoja haiwezekani kuwa.

Hayo yalikuwa mstari wa kwanza kwa yule anayemfuata Yesu na anataka kumuiga kwa mfano wa mashahidi wa Injili. Haiwezekani kutaja wote waungamizi wa kuu wa Imani katika eneo hilo lakini angazo kutaja wamojawapo mtakatifu Ladislao na Mtakatifu Margherita, na pia kukumbua susa za karne iliyopita kama vile Kardinali József Mindszenty, wenyeheri na watakatifu Vilmos Apor na Zoltán Meszlényi, Mwenyeheri László Batthyány-Strattmann. Kuna wengi wenye haki. Na imani , mababa na mama katika Nchi yao. Kwao Papa amependa kuwakabidhi wakati ujia wa Nchi hiyo pendwa kwake. Akiwashukuru kwa kumsikiliza kile alichokuwa nacho rohoni mwakekushirikishana nao, amewahikishia ukaribu wake, na sala zakwa kwa watu wote wa Hungaria akiwa na wazo maalu kwa wale ambao wanaishi nje ya Nchi yao na kwa wale ambao alikutana nao  na amefikiria Jumuiya ya kitwa ya Hungaria aliyowahudumia huko Buenos Aires katika maisha, na walimtendea mema.. I(sten, áldd meg a magyart)! Yaani Mungu abariki wahungaria.

Hotuba ya Papa Francisko nchini Hungaria
28 April 2023, 16:23