Baba Mtakatifu amekutana na Maaskofu wa Tanzania
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ijumaa tarehe 19 Mei 2023, Maaskofu wa Tanzania walikutana na Baba Mtakatifu mjini Vatican. Kabla ya mkutano huo ulitangulia misa Takatifu katika Kaburi la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Misa Takatifu ilioongozwa na Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Mbeya. Maaskofu na maaskofu wakuu wote walikuwapo pia Askofu Mkuu Protase Rugambwa, Askofu Mwandamizi wa jimbo Kuu katoliki la Tabora. Masomo yalisomwa, ambapo Somo la kwanza na Zaburi vimesomwa na Mkuu wa Majeshi Mstaafu nchini Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, ambaye katika muktadha wa hija hii ni Mwakilishi wa Walei Katoliki Tanzania katika Baraza la Maaskofu anayembatana na Maaskofu na vile vile Injili ilisomwa na Padre Cesco Msaga(CPPS), Katibu Msaidizi wa Baraza la Maaskofu Tanzania. Askofu Mkuu Nyaisonga akianza mahubiri yake amesisitizia ushuhuda wa kile ambacho wameshuhudia kwa siku hizi kukipeleka watakaporudi mahalia.
Askofu Mkuu Nyaisonga amesema ni kumkabidhi Mungu ili kuwapa nguvu inayowawezesha kuendelea na “hapa ni mahali pa kujipyaisha,kupata nguvu mpya. Katika masomo yote yalikuwa yanaeeleza kwamba msiongope.” Askofu Mkuu amesema “katika somo la kwanza Mtume Paulo alisema ‘Usiogope,’ nguvu ya Mungu iko na wewe, yeye kweli kabla hajakutetea, haoni sababu ya kukuhukumu. Kwa sababu ananiondolea kesi hiyo, anaifuta hiyo kesi na Paulo mtume anaendelea kutenda utume wake”. Kwa hiyo “Yeye alipata maono, maono yaliyomwambia asiogope Mungu atamkinga. Sisi hapa tuna zaidi ya maono. Sisi sio ndoto, ila tutawaadithia watu hao,na mashujaa wanawambia msiogope, kama sisi tuliweza, nyakati zile ambazo hali ya kumwamini Kristo ilikuwa chini na ishara zile za Kristo hazikuaminika kirahisi, ninyi mnaweza zaidi, kwa sababu alama zake za nyakati na ishara ni nyingi, za nguvu ya Mungu kati watu.”
Askofu Mkuu nyaisonga akiendelea amesisitiza kwamba “hata kupitia Injili ya Bwana, Yesu anasema mnasononeka na kusikitika, lakini hiyo ni ya muda mfupi, kwa sababu kifuatacho ni furaha kubwa kama ilivyo kwa Mama mzazi anavyosahau mara moja mateso ya kabla ya kujifungua. Na anafurahia mtoto, baada ya kujifungua. Kwa hiyo ameongeza “ huu ni mwaliko wa kutokuogopa yale ambayo ni msingi wa imani yetu. Na pole pole, mateso yanapungua na furaha inaongezeka. Kutoogopa haimanisha kukaa tu, badala yake inaaamisha kufanya kazi, Mtume Paulo aliwambiwa asiogope na aliendelea kufanya kazi. Pole pole mateso yake yakapungua na kukawa na furaha hadi leo” amesisitiza Askofu Mkuu Nyaisonga.
Akimgeukia Mtume Petro, amesisitiza kwamba“alijua hapaswi kuogopa na aliendelea na hakutumia muda mwingi wa kufikiria mateso, bali muda mwingi wa kufanya kazi yake; kuwapa watu furaha na hatimaye ikawa furaha yake pia”; kwa namna hiyo Rais wa TEC amethibitisha kuwa: “Hii ndiyo kanuni tunayoichota leo hii hapa, kwa kumtazama Mtume Petro, lakini pia hata mitume wengine, na mapapa watakatifu”. Mateso yeyote ya kichungaji, au ya maisha, ya kila mmoja na majukumu yake ni kama maandalizi tu ya kutupeleka kwenye furaha. Ni kama ngazi za kupandia kuelekea furaha. Kwa hiyo Mateso na mahangaiko yote haya hayatwambii kuwa tukae na kusubiri ili furaha ije yenyewe, kinyume chake lazima kuendelea kufanyia kazi. Askofu Mkuu aliwaomba “kuchota baraka ya pekee na ikolee ndani Roho zetu ili tuwaambukize ndugu zetu na waamini wote, tunaokutana nao, kwa kuwa tunatoka kushuhudia matendo makuu ya Mungu", Alisistiza zaidi Askofu Mkuu.
Rais wa TEC akiendelea na mantiki ya ushuhuda amesema "Nimetoka kati ya mashujaa ambao hawakuogopa moto, silaha, mateso yote na imani ikabaki salama. Na nguvu hiyo ipate kuonekana katika utume wetu ili na wingene waseme kwamba kama huyu aliyetoka huko anadhihirisha, nami nifanye hivyo.” Kwa kuhitimisha ameomba kupitia maombezi ya Mtume Petro kwamba: “sisi sote tuimarike na tutimize kama Mungu anavyotutuma”.
Kabla ya sala ya Mwisho katika Kaburi la Mtakatifu Petro, Padre Cesco Msaga,(CPPS), Katibu Msaidizi wa Baraza la Maaskofu Tanzania, kwa niaba ya wote alitoa shukrani kwa wale wote ambao wamewasindikiza katika siku hizi kufanikisha ziara yao hasa katika ibada za misa takatifu zilizofanyika kila asubuhi kwa kusindikizwa na baadhi ya watazania, Roma.
Na mara baada ya Baraka Takatifu Sala ya Imani kwa kukiri kwa Bwana wetu Yesu Kristo, kama walivyofanya watangulizi wote kuanzia na Mtakatifu Petro, Mtume aliyeitwa kuwahimarisha wana wake ilifuatia na, vile vile kujikabidhi kwa Mama Yetu Bikira Maria na watakatifu wote. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC kwa maana lilianza Hija ya Kitume “Ad Limina Apostolorum Visitatio, mnamo Dominika tarehe 14 Mei 2023 ,” hija ambayo kiutamaduni hufanyika kila baada ya miaka mitano. Kuanzia tarehe 15 Mei walianza na misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu, Roma mbele ya Picha ya Bikira Maria Afya ya Warumi (Salus Populi Romani) huku wakimkabidhi Hija yao kwa mama Maria. Misa hiyo iliongozwa na Askofu Mkuu Paul Ruzoka, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Tabora, Tanzania. Baada ya misa Takatifu Maaskofu hao walianza matembezi katika mabaraza ya Kipapa.
Jumanne, tarehe 16 Mei 2023, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania katika matembezi yao walifika pia katika Baraza la Kipapa la Mawasiliano na kuzungumza na wakuu wake chini ya uongozi wa Dr. Paolo Ruffini, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano. Jumatano tarehe 17 Mei 2023 Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania lilipata bahati ya pia kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Italia mara baada ya ziara nyingine za siku kama ilivyopangwa. Kwa hiyo walikutana na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, kwa kusikiliza historia ya mahusiano kati ya Vatican na Tanzania ambapo Balozi wa Tanzania nchini Italia alielezea ukweli wa mshikamano mkubwa pia kulikuwa na wawakilishi wa diaspora kutoka pande zote za Italia.
Alhamisi tarehe 18 Mei 2023, Maaskofu wa Tanzania walisali Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta. Misa iliongozwa na Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya, wa Jimbo Kuu katoliki la Dodoma Tanzania. Siku hiyo ilikuwa ni Siku Kuu mjini Mjini Vatican ya Kupapa kwa Bwana, na ambayo kiutamaduni,ndiyo mahali pekee au nchi ndogo pekee ulimwenguni inayooadhimisha siku kuu kama hizi katika siku yenyewe, lakini makanisa yote mahalia, siku kuu zinazoangukia katikati ya Juma zinapelekwa Dominika inayofauta.