Papa amekutana na Rais wa Ukraine
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika ugeni uliofika mjini Vatican, yalikuwa ni maneno machache, yaliyosemwa kibinafsi, kwa mara ya kwanza tangu mwanzo wa mzozo wa vita." Ni heshima kubwa kwangu kuwa hapa ....” “Asante kwa ziara hii.” Baadaye walipeana mikono, na rais kwa kuinamisha kichwa chake. Kwa hiyo Rais Volodymyr Zelensky amefika mjini Vatican kukutana na Papa Francisko, Jumamosi tarehe 13 Mei 2023. Alifika muda mfupi baada ya saa kumi jioni, akiwa kwenye gari la kivita, kupitia uwanja wa Ukumbi wa Paulo VI. Alivaa nguo rahisi kama inavyooneshwa kwenye video na picha: suruali ya kijivu, tisheti ya ya rangi ya kijeshi na aliwasalimu waandishi wa habari waliokuwepo kwanza kwa kutikisa kichwa na kisha kwa mkono wake.
Hata hivyo ilikuwa ni dakika chache tu baada ya saa 10 jioni ambapo Rais Zelensky alikuwa ameacha Ikulu ya Chigi, Roma kwa msafara kupitia, katikati ya Roma ambayo tayari ilikuwa ina ulinzi mkali tangu Ijumaa tarehe 12 Mei, kuelekea Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Magari hayo yalivuka uwanja na kisha kuelekea mbele ya Ukumbi wa Paulo VI. Kwa hiyo aliye mkaribisha rais wa Ukraine ni Monsinyo Leonardo Sapienza, mwakilishi wa Nyumba ya Kipapa. Akifuatiwa na balozi wa Ukraine anayewakilisha nchi yake mjini Vatican, Bwana Andrii Yurash na mkuu wa ofisi ya rais, Andriy Yermak.
Papa alimkaribisha kwenye mlango wa Ukumbi huo, ambapo walifanya mkutano huo na sio katika Jumba la kitume. Kwa pamoja walielekea kwenye ofisi iliyoandaliwa kwa tukio hilo. Wakiwa wameketi wakitazamana kwenye meza na msalaba juu yake na upande wa kulia kulikuwa na picha ya Mama Yetu wa Luján, ambapo walianza mazungumzo milango ikiwa imefungwa na ambapo mazungumzo hayo yalichukua kama dakika 40, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican. Mada zilizozungumza ni za hali ya kibinadamu na kisiasa nchini Ukraine iliyosababishwa na vita vinavyoendelea.
Kwa mujibu wa msemaji wa Vyombo vya habari Vatican, Papa amemhakikishia maombi yake ya mara kwa mara, yaliyoshuhudiwa na maombi mengi afanyayo kila wakati wa katekesi na maombi ya kuendelea kwa Bwana kwa ajili ya amani, tangu mwezi Februari mwaka 2022. Wote wawili hata hivyo "walikubaliana juu ya haja ya kuendelea na juhudi za kibinadamu katika kuunga mkono idadi ya watu". Papa alisisitiza "hitaji la dharura la 'ishara za ubinadamu' kwa watu dhaifu zaidi, wahathirika wasio na hatia wa mzozo huo."
Zawadi
Miito hiyo kutoka kwa Papa, inaongeza kwa zile nyingine nyingi zilizotolewa katika miezi hii zaidi ya kumi na tano ya uchokozi dhidi ya watu waliopigwa wa Kiukreni. Maneno ya ukaribu, ya maumivu na pia matumaini katika amani yaliyoombwa mara kadhaa na kwa hiyo yametafsiriwa kuwa zawadi ambayo Papa alimpatia Rais Zelensky. Kwanza ilikuwa ni kazi ya shaba inayoonesha tawi la mzeituni, ishara ya amani. Pamoja na hiyo kuna Ujumbe wa Siku ya Amani Duniani 2023, Hati ya Udugu wa Kibinadamu, kitabu cha Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV, Kitabu cha Waraka wa Amani kwa ajili ya Ukraine ambacho kinaleta pamoja zaidi ya uingiliaji wa hotuba za Papa juu ya vita vya Ukraine.
Zawadi zilizotolewa na Rais Zelensky pia zilikuwa muhimu. Kwa kazi ya sanaa iliyotengenezwa kwa sahani isiyo na risasi na mchoro juu ya mauaji ya watoto wakati wa mzozo ulioitwa Hasara 2022-58, ambapo 58 inawakilisha siku ya hamsini na nane tangu kuanza kwa uvamizi wa Urussi na ambayo, hadi kufikia hatua hiyo, ilisababisha vifo vya watoto 243. Katika kazi hiyo maelezo yanasomeka kuwa: “Hasara kwa siku zijazo na kwa wanadamu wote.”
Mazungumzo na Askofu Mkuu Gallagher
Baada ya mazungumzo ya faragha na Papa Francisko, rais wa Ukraine alikuwa na mkutano na katibu wa Vatican wa Mahusiano na Matifa na Mashirika ya kimataifa, Askofu Mkuu, Paul Gallagher. Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican hakuwepo kuanzia tangu 12 kwa sababu amekwenda mjini Fatima, kuadhimisha Sikukuu ya Bikira Maria katika Madhabahu ya Cova de Iria, Ureno.
Kwa hiyo katika mazungumzo yao na Askofu Mkuu Gallagher yalichukua kama nusu saa. Kama taarifa ya Vyombo vya habari Vatican ilivyofahamisha, kwanza kabisa walijikita katika masuala ya vita vya sasa vya Ukraine na dharura zinazohusiana nayo, hasa zile za kibinadamu na pia hitaji la kuendeleza juhudi za kupata amani. Katika tukio hilo pia ilikuwa vizuri kushughulikia masuala ya pande mbili, hasa hasa yanayohusiana na maisha ya Kanisa Katoliki nchini Ukraine.