Papa Francisko atakutana na rais wa Ukraine Zelensky mjini Vatican!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ni mkutano wa pili ana kwa ana, ambao utafanyik mara baada ya ule wa mnamo 2020; wa kwanza tangu kuzuka kwa mzozo wa vita nchini Ukraine. Kwa hiyo karibu miezi kumi na tano baada ya shambulio la kwanza la Urussi huko Kyiv, Papa Francisko atampokea Rais Volodymir Zelensky wa Ukraine. Mkutano huo utafanyika Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 kama ilivyotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, vikithibitisha habari zilizosambazwa na vyombo vya habari.
Mkutano huo utakuwa alasiri saa 9 mjini Vatican na utafanyika kama sehemu ya safari ya rais wa Ukraine jiji Roma, ambayo pia itajumuisha mkutano na Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, na pamoja na Waziri Mkuu Bi Giorga Meloni. Rais Zelensky mwenyewe alitangaza hayo saa 4.24 katika akaunti yake ya Twitter akizungumzia juu ya ‘ziara muhimu’
Papa na rais wa Ukraine kama ilivyotajwa walikuwa wamekutana ana kwa ana katika Jumba la Kitume Vaticana mnamo tarehe 8 Februari 2020, chini ya mwaka mmoja baada ya uchaguzi ambao ulikuwa umeamuru ushindi wake katika uongozi wa Ukraine. Mazungumzo yao yaliyochukua karibu nusu saa nyuma ya milango iliyofungwa, ambayo mwisho wake Papa Francisko alikuwa ametoa zawadi ya Medali ya Mtakatifu Martino di Tours, kwa matumaini kwamba ingewalinda watu wa Ukraine ambao tayari walikuwa wamekumbwa na vita vya wakati huo katika eneo moya la nchi mashariki mwa nchi. Rais Zelensky pia alikutana na Katibu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa Taarifa za vyombo vya habari Vatican ilibainihs akuwa "Katika mazungumzi yao yalikuwa ni ya ukarimu huku wakibainisha juu ya kujitolea zaidi kwa hali ya kibinadamu na kutafuta amani katika muktadha wa mzozo ambao, tangu 2014, bado umekuwa ukiisumbua Ukraine. Aifha taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ilikuwa imethibitisha matumaini yaliyoelezwa “kwamba Pande zote zinazohusika zioneshe usikivu wa hali ya juu kwa mahitaji ya watu, waathiriwa wa kwanza wa ghasia, pamoja na kujitolea na uwiano katika mazungumzo.”