Tafuta

Papa Francisko:tunapopata ugumu wa maisha tujue mahali pa kwenda

Neno la leo ni kisima cha faraja na matumaini.Yesu hakutengena kamwe na sisi lakini alitufungulia njia,alitanguliza lengo letu la mwisho,la kukutana na Mungu Baba,mahali ambapo katika moyo wake kuna nafasi ya kila mmoja.Kwa hiyo tunapofanya uzoefu wa ugumu,hasara na hata kushindwa,tukumbuke ni wapi maisha yetu yanaelekea.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya V ya Pasaka tarehe 7 Mei 2023 kiini cha Maneno ya Yesu ni  “Mimi ndimi njia, ukweli na uzima: mtu haji kwa Baba ila kwa njia yangu.” (Yh14,1-12), ambapo katika Tafakari ya Baba Mtakatifu Franciso, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu amesema: Injili ya liturujia ya siku kutoka kwa Yohane 14,1-12 imetolewa katika hotuba ya mwisho ya Yesu kabla ya kifo chake. Moyo wa mitume ulikuwa na shaka, lakini Yesu aliwaelekeza maneno ya uwakikisho akiwaalika wasiwe na woga: Kiukweli yeye hawaachi, lakini anakwenda kuwaandalia makao kwa ajili yao na kuwaongoza kuelekea lengo la mwisho. Bwana leo hii anaalika hivyo kwetu sisi sote maajabu ya eneo,  mahali pa kwenda, na wakati huo huo, anatuelekeza jinsi ya kwenda na kutuonesha njia ya kupitia. Anatuambia twende wapi na jinsi ya kwenda huko.

Umati wa waamini na mahujaji kwenye sala ya Malkia wa Mbingu
Umati wa waamini na mahujaji kwenye sala ya Malkia wa Mbingu

Awali ya yote wapi pa kwenda. Baba Mtakatifu ameeleza kuwa “Yesu anaona mashaka ya wanafunzi wake, woga wao wa kuachwa, kama ambavyo inatokea hata sisi tunapolazimika kuachana na mtu ambaye tulikuwa tunampenda. Na kwa hiyo anasema “mimi ninakwenda kuwaandalia makao(…), ili mahali nitakapokuwa nanyi muwepo (rej.Yh 14 2-3).  Yesu alitumia picha halisi ya kifamilia nyumbani, mahali ambapo kuna uhusiano na urafiki wa kina.  “Katika nyumba ya Baba, aliwambia marafiki zake na kwa kila mmoja wetu kuwa “kuna nafasi kwa ajili yako, unakaribishwa, na utaookelewa daima kwa joto na mkumbatio na mimi nitakuwa mbinguni kukuandalia nafasi.” Baba Mtakatifu Francisko akiendelea alisema kuwa Neno hilo ni kisima cha faraja na matumaini. Yesu hakutengena kamwe na sisi lakini alitufungulia njia, alitanguliza lengo letu la mwisho, la kukutana na Mungu Baba, mahali ambapo katika moyo wake kuna nafasi ya kila mmoja. Kwa hiyo tunapofanya uzoefu wa ugumu, hasara na hata kushindwa, tukumbuke ni wapi maisha yetu yanaelekea.

Tafakari ya Papa kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu Mei 7,2023

Papa amesisitiza kwamba “hatupaswi kupoteza mtazamo wa hatma, hata ikiwa leo hii kuna hatati ya kusahamu, ya kusahau maswali ya mwisho yale muhimu: je tunakwenda wapi? Je tunaelekeza wapi mwendo? Kwa sababu gani inatupaswa kuishi? Bila kujiuliza maswali haya, tunasonga maisha ya wakati uliopo tu, tunafikiria kuwa lazima kufurahia kadri tuwezavyo na tunaishia kuishi kwa siku hiyo tu, bila lengo na bila matazamio. Makao yetu kinyume chake ni kule mbinguni (Fil 3,20) na tusisahau kamwe ukuu na uzuri huo wa mwisho! Baba Mtakatifu aidha amebainisha kwamba mara tu unapogundua hatma, hata sisi kama Mtume Thomas, katika Injili ya Siku, tujiulize  swali “ je ni jinsi gani ya kufika? Hii ni kwa sababu hasa wakati kuna matatizo makubwa ya kukabiliana nayo na tuna hisia ambazo ubaya huo una kuwa na nguvu, tunapaswa kujiuliza: je nini ninapaswa kufanya, na ni njia ipi ya kufuata?   Kwa hiyo tusikiliza jibu la Yesu lisemalo “ Mimi ni njia, Ukweli na Maisha (rej Yh 14, 6).

Waamini wakisililiza tafkari ya Papa katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.
Waamini wakisililiza tafkari ya Papa katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican.

Kwa njia hio Yesu ni njia ya kufuata ili kuishi katika ukweli na kuwa na maisha tele. Yeye ni maisha na hivyo imani katika Yeye siyo ‘kifurushi cha mawazo’ ya kuamini, lakini ni njia ya kupitia, mchakato wa safari ya kutumiza, safari na Yeye. Ni kufuata Yesu kwa sababu Yeye ni maisha ambayo yanatufikisha katika furaha isiyozama. Ni kumuihsa , hasa kwa isra za ukaribu na huruma kueleza wengine. Na tazama dira kwa ajili ya kufika mbingu: kupenda Yesu, njia, na kugeuka kuwa ishara kwa njia ya upendo duniani. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro alisema, tuishi wakati uliopo na kushikana mikono katika wakati uliop lakini tusiache tufungwe na wakati uliopo: tutazame juu, mbinguni, tukumbuke lengo la mwisho, tukumbuke kuwa tumeitwa katika umilele, katika mkutano na Mungu. Na kutoka mbinguni hadi moyoni, tupyaishe leo hii chaguzi za Yesu, chaguzi za kumpenda na kutembea nyuma ya nyayo zake. Bikira Maria, aliyemfuata Yesu,na ambaye tayari alifika kwenye lengo, atusaidie matumaini yetu.

Waamini wengi katika sala ya Malkia wa Mbingu
Waamini wengi katika sala ya Malkia wa Mbingu
07 May 2023, 13:26