Papa Francisko amerudi Hospitali ya Gemelli kwa upasuaji mpya
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, Dk. Matteo Bruni Jumatano tarehe 7 Juni 2023, asubuahi amesema kuwa: “Baba Mtakatifu, mara baada ya Katekesi yake, amekwenda Hospitali ya Chuo Kikuu A. Gemelli mahali ambapo alasiri, atafanyiwa Upasuaji wa 'Laparotomia', yaani plastiki ya ukuta wa tumbo na bandia. Upasuaji huo uliopangwa katika siku za hivi karibuni na timu ya matibabu inayomsaidia Baba Mtakatifu, ambao walionelea kuwa ni muhimu kwa sababu ya ugonjwa wa hernia wa ndani ambao unasababisha magonjwa ya mara kwa mara, maumivu na mbaya zaidi." Kwa kuongezea "Kwa kulazwa kwake hospitalini katika kituo cha afya kutachukua siku kadhaa ili kuruhusu mapumziko ya kawaida ya baada ya upasuaji na ahueni kamili ya utendaji," amehitimisha Dk. Bruni.
Kwa mara ya tatu Papa analazwa
Ikumbukwe kuwa huu ni uingiliaji kati wa tatu katika Hospitali hiyo ya Gemelli. Kama inavyokumbukwa, Papa alilazwa hospitalini mnamo tarehe 29 Machi 2023 kwa ugonjwa wa mfumo wa kupumua wa kuambukiza ambao ulikuwa umemsababishia matatizo ya kupumua. Kisha aliachiliwa mnamo Aprili 1 iliyofuata, baada ya ahueni ya haraka na chanya. Mwishoni mwa mwezi Aprili, katika mkutano na waandishi wa habari akiwa kwenye ndege iliyorudi kutoka Hungaria, katika ziara yake ya kitume kwa waandishi wa habari ambao walimuuliza kuhusu hali yake ya afya, Papa Francisko alisema: "Nilichokuwa nacho ni ugonjwa mbaya mwishoni mwa Katekesi ya Jumatano, sikujisikia kula chakula cha mchana, nililala kidogo, sikuzimia, lakini ndio kulikuwa na homa kali, homa kali, na saa tisa alasiri daktari alinipeleka hospitalini mara moja: na nilikuwa na nimonia yenye nguvu, katika sehemu ya chini ya mapafu." Kwa kuongeza alisema: Namshukuru Mungu ninaweza kusema, kwa kiasi kwamba kiumbe, mwili, uliitikia vizuri matibabu. Asante Mungu.”
Kulazwa tarehe 4 Julai 2021
Hata katika mahojiano mengine ya hivi karibuni zaidi na Telemundo, alieleza kwamba kulazwa hospitalini kumekuwa “jambo lisilotarajiwa. Lakini tuliipata kwa wakati, waliniambia, ikiwa tungengoja masaa machache zaidi ingekuwa mbaya zaidi. Lakini ndani ya siku nne nilikuwa nimepona.” Operesheni ya upasuaji ambayo Papa alifanyiwa tarehe 4 Julai 2021 kwa ajili ya ugonjwa kwenye utumbo mkuu ilikuwa ngumu zaidi. Operesheni hiyo ilifanywa chini ya anesthesia ya jumla (ambayo, Papa Francisko mwenyewe alikuwa amefichua hadharani kwamba ilikuwa imemletea usumbufu) katika sura nzuri ya afya ya Papa ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 84.
Tumuombee Papa
Katika miaka ya hivi karibuni, matatizo ya goti yamemsumbua na ambayo Papa Francisko anatibu kwa njia mbalimbali za matibabu, ikiwa ni pamoja na laser na magnetotherapy, vyombo viwili ambavyo aliielezea kuwa vimeimarisha mfupa na kumfanya aweze kutembea tena kwa fimbo kwa safari fupi na wakati mwingine kuwa na msaada wa msindikizaji. Kwa matembezi marefu anatumia kiti cha magurudumu. Kwa sasa, ambapo anakabiliwa kwa upya na upasuaji, tumsindikize kwa sala.
Hata hivyo Dk. Bruni pia akijibu maswali ya waadhishi wa habari kuhusu Papa amesema "shughuli za adhara kwa Papa zimezitishwa hadi tarehe 18 Juni 2023 ili kutazamia afya yake inavyoendelea".