Papa Francisko:Udugu una kitu chanya cha kutoa kwa uhuru na usawa!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Hata kama siwezi kuwapo hapo kuwapokea kinafsi, ninataka kuwakaribisha na kuwashukuru kwa moyo kufika kwenu. Ninayofuraha ya kuthibitisha pamoja na ninyi shauku ya udugu na amani kwa maisha ya ulimwengu. Ndivyo imeanza hotuba ya Papa iliyosomwa mbele ya Umati mkubwa na Kardinali Mauro Gambetti Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro aliwalekeza waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican na viwanja vingine 8 vilivyopo katika ulimwengu katika tukio la Udugu wa Kibinadamu kwa kuongozwa na kauli mbiu “ Nota Alone, yaani , siyo pekee yake, Jumamosi jioni tarehe 10 Juni 2023. Kwa hiyo Baba Mtakatifu katika ujumbe huo anabainisha kwamba Mwandishi mmoja aliweka katika midomo ya Francis wa Assisi maneno haya: “Bwana yuko pale mahali walipo ndugu zako”(E. Leclerc, La sapienza di un povero). Kiukweli, mbingu iliyopo juu yetu inatualika kutembea katika dunia pamoja, ili kujigundua kama ndugu na kuamini katika udugu kama hatua msingi kwa ajili ya hija yetu.
Katika Waraka wa Fratrelli tutti, Papa anakumbusha alivyoandika kuwa “Udugu una kitu chanya cha kutoa kwa uhuru na usawa” (Ft 103), kwa sababu anayemuona ndugu, anamwona mwingine katika uso na sio idadi: daima ni mtu ambaye ana hadhi na anastahili heshima, sio kitu cha kutumia, kunyonya au kubagua. Katika ulimwengu wetu, ambapo umechanika kwa sababu ya vurugu na vita, haitoshi kuguswa na kurekebishwa: Ni Mshikamano mkubwa tu wa kiroho na kijamii ambao unazaliwa katika mioyo na kuzungukia udugu unaweza kupelekea kituo cha mahusiano ya utakatifu na usiokiukwa wa hadhi ya kibinadamu. Kwa maana hiyo udugu hauna haja ya kinadharia, lakini kwa ishara ya dhati na changuzi za kushirikisha ambazo zinafanya utamaduni wa amani. Swali la kujiuliza sio labda ni nini jamii na ulimwengu unaweza kunipatia, bali ni kitu gani mimi ninaweza kutoa kwa kaka na dada zangu na marafiki; kusali kwa ajili ya yule aliyenijeruhi, kujua na kusaidia yule mwenye kuwa na hitaji, kuchukua neno la amani shuleni, chuo kikuu au katika maisha ya kijamii, kupaka mafuta ya ukaribu kwa mtu ambaye yuko peke yake.
Baba Mtakatifu Francisko anakazia kusema kwamba “tunahisi kualikwa kupaka mafuta ya huruma ndani ya uhusiano ambao umechafuka, kati ya watu wote. Kwa hiyo Papa amehimiza kwamba wasichoke kupaza sauti kuwa “hapana kufanya vita kwa jina la Mungu na katika jina la kila mwanamke na mwanaume ambaye anauisha amani. Papa amefikiria ushairi wa Giuseppe Ungareti ambao katika moyo wa vita, alihisi hitaji la kuzungumzia juu ya ndugu kama: “Neno linalotetemeka/katika usiku/jani ambalo limezaliwa papo/. Udhaifu ni wema mdhaifu na wa thamani. Bado ni ukweli katika bahari ya dhoruba ya migogoro ambayo inapanda ulaghai, Kuomba ni kukumbuka ambaye anapambana na wote ambao wanahisi udugu ambao unatuunganisha ni mwenye nguvu zaidi ya chuki na vurugu, na zaidi unatuunganisha wote katika uchungu. Na hapo ndipo panaanzia kwa maana ya kuhisi pamoja, cheche ambayo inaweza kuwasha mwanga ili kuondoa usiku wa migogoro.
Kuamini kwamba mwingine ni ndugu na kusema mwingine ni ndugu sio neno tupu, bali ni jambo la dhati zaidi ambalo kila mmoja wetu anaweza kufanya. Hakika, ina maana ya kujikomboa kutoka katika umaskini wa kujiamini katika ulimwengu kama mtoto wa pekee. Inamaanisha, wakati huo huo, kuchagua kushinda mantiki ya washirika, ambao hukaa pamoja kwa maslahi tu, pia kujua jinsi ya kwenda zaidi ya mipaka ya mahusiano ya damu au kikabila, ambao wanatambua tu sawa na kukataa alye tofauti. Katika hotuba ya aliyoiandaa Papa Francisko amewaelekeza kuwa anakumbuka msemo wa Msamaria mwema (Lk 10,25-37), aliyesimama kwa huruma mbele ya Myahudi mwenye kuhitaji msaada. Utamaduni wao ulikuwa adui, historia yao ilikuwa tofauti, Mikoa yao yenye vizingiti mmoja na mwingine, lakini kwa mtu yule aliyekutwa njiani na hitaji lake, alisaidiwa awali ya yote.
Wakati watu na jamii zinachagua udugu hata siasa zinabadilika: watu wanarudi kutawala faida, nyumba tunayoishi sote juu ya mazingira iliyokuwa ikinyonywa kwa masilahi yake, na kazi inalipwa kwa ujira unaostahili, ukarimu unageuka kuwa utajiri, maisha tumaini, haki inafungua ukarabati na kumbu kumbu ya ubaya uliotendeka unaonywa katika mkutano kati ya waathirika na wahalifu. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo anawashukuru kwa kuandaa mkutano huo na kutoa maisha kwa ‘Tamko’ juu ya Udugu wa kibinadamu, ulifanyiwa kazi asubuhi ya tarehe 10 Juni na Watu waliopata Tuzo ya Nobel waliokuwapo. Papa anaamini kwamba hiyo inatoa uhalisia wa udugu na iwe ndiyo kiongozi mwafaka kwa ajili ya kuushi na kushuhudia kila siku kwa namna ya dhati.
Papa amewasifu kwamba wamefanya kazi vizuri na amewashuru sana! Amewaomba wafanye kwa namna ya kuishi siku hiyo ili iwe hatua ya kwanza ya mchakato wa safari ambayo inaweza kuanzisha mchakato wa udugu. Na viwanja vilivyounganishwa kutoka sehemu za miji mbali mbali duniani, ambao amewasalimia kwa upendo na kwamba ushuhuda huo uwe utajiri wa utofauti, uwe na uwezekano wa kuwa ndugu hata wasipokuwa karibu, kama ilivyojitokeza kwake Papa. Amewaomba waendelee mbele! Baba Mtakatifu kwa kuhitimisha amependa kuwaachia picha ya mkumbatio na kwamba katika siku hiyo waliyopitia mchana wote pamoja anawatakia kuhiifadhi katika moyo. Na katika kumbu kumbu shauku ya mkumbatio wa wanawake na wanaume.