Tafuta

 Papa Pio XII  na kulipuliwa kwa mji wa Roma mnamo tarehe 19 Julai 1943. Papa Pio XII na kulipuliwa kwa mji wa Roma mnamo tarehe 19 Julai 1943. 

Papa akumbuka mlipuko wa Bomu katika mji wa Roma mnamo 19 Julai 1943!

Kumbukizi la shambulio la bomu jijini Roma ambapo mabomu 4,000 yalirushwa kwenye jiji mnamo 19 Julai 1943.Katika mtaa wa Mtakatifu Lorenzo pekee walikufa watu 717 na kujeruhiwa 4,000.Kwa ujumla walikufa watu 3,000 na 11,000 walijeruhiwa katika mitaa mingine.Nyumba 10elfu ziliharibiwa na raia 40elfu waliachwa bila makazi.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika kuelekea siku ya kumbukumbu la shambulio la bomu kwenye mtaa wa Mtakatifu Lorenzo jijini Roma ambapo inasadikika ni mabomu 4,000 yalirushwa kwenye jiji mnamo tarehe  19 Julai 1943. Katika tukio hilo, Mtaa wa Mtakatifu Lorenzo pekee kulikuwa na watu 717 waliokufa na watu 4,000 waliojeruhiwa. Kwa ujumla watu 3,000 walikufa na 11,000 walijeruhiwa katika mitaa mingine ya Tiburtina, Prenestino, Casilino, Labicana, Tuscolano na Nomentano jijini Roma pia nyumba 10 elfu ziliharibiwa wakati  raia 40elfu waliachwa bila makazi. Hili lilikuwa shambulio la kwanza la bomu katika jiji la Roma.

Papa Pio XII na watu wa Roma walioshambuliwa na bomu
Papa Pio XII na watu wa Roma walioshambuliwa na bomu

Katika muktadha huo mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko amesema: “Ninataka kuwakumbusha kwamba miaka themanini iliyopita, tarehe 19 Julai 1943, baadhi ya mitaa ya  Roma, hasa ya Mtakatifu Lorenzo, yalipigwa bomu na Papa, Mtumishi wa Mungu Pio XII, alitaka kwenda miongoni mwa watu hao walioshtuka. Kwa bahati mbaya, hata leo hii majanga haya yanarudiwa. Inawezekanaje? Tumepoteza kumbukumbu zetu? Bwana atuhurumie na aikomboe familia ya wanadamu kutoka katika janga la vita, tuwaombee hasa watu wapendwa wa Ukraine wanaoteseka sana.”

Wakati Papa Pio XII akiwabariki wakazi wa mtaa wa Mtakatifu Lorenzo waliokuwa wameangamizwa, Mfalme Vittorio Emanuele II pia alifika lakini idadi ya watu ilimfunika kwa matukano. Mwisho wa ufashisti hata hivyo ulikuwa karibu, kutangazwa rasmi mnamo tarehe 25 Julai 1943. Kwa hiyo Mtaa wa Mtakatifu Lorenzo, ulipata medali ya dhahabu kwa ushujaa wa kijeshi na upinzani, ambapo inawakilisha kumbukumbu ya karne ya ishirini, ya kupambana na ufashisiti na vita vya ukombozi. Baada ya miaka themanini, kilichobaki sasa cha tukio hilo la kutisha ni gofu la jengo ya orofa tatu, lililochomwa kwenye njia ya Tiburtina na ambalo, kwa nia njema kabisa, lingepaswa kuwa Nyumba ya Kumbukumbu na Historia, lakini halijajengwa kamwe!

Papa baada ya tafakari na sala 16 Julai
16 July 2023, 13:10