Papa akutana karibia na watoto 250 wanaocheza pamoja mjini Vatican

Kama kawaida yake Papa alikutana kwenye ukumbi wa Paulo VI takriban watoto 250 wenye umri kati ya miaka 5 -13 ambao wanashiriki katika toleo la 2023 la mpango wa kiangazi wa Vatican.Walisindikizwa na muziki na ngomana tumbuizo,baadaye Papa alizungumza na vijana na kupokea zawadi zao.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, watoto na vijana wanaoshiriki katika kituo cha michezo ya kiangazi mjini Vatican tarehe 18 Julai 2023 walitembelewa na Baba Mtakatifu Francisko akisindikizwa na  Padre  Franco Fontana, S.D.B., mwenye jukumu la kuandaa Juma za shughuli za kimwili, kielimu na kiroho katika kituo hicho.  Watoto hao na vijana walimpokea kwa kuimba wimbo wa ‘Yesu Kristo ni maisha yangu” na hivyo vilisikika vifijo vya watoto wakishangilia. Na Padre Franco hata hivyo aliwachangamsha vijana hao. Baada ya hapo kulikuwa na watoto watatu ambao waliwakilisha wengine kuuliza maswali ambayo Papa Francisko alijibu.  Kama vile babu kati ya wajukuu zake, siku chache kabla ya maadhimisho ya Siku ya Mababu na Wazee Duniani ambayo  Papa alitamani sana  itakayoadhimishwa Dominika 22 Julai, Baba Mtakatifu  alizungumza nao, huku akitoa ishara za upendo  kwa watoto na vijana wanaofanya uzoefu wa kukaa pamoja katika kituo kilichoandaliwa katika majira ya kiangazi mjini Vatican.

Kikundi cha kijani
Kikundi cha kijani

Hawa ni takribani watoto 250 ambapo Papa Francisko ameanza kwa kuulizwa swali na mtoto mmoja kwamba ni ujumbe gani wanaoweza kuchukua kwa washujaa wao ambao ni wazazi. Kwa kujibu Papa amesema ni ‘asante mama  na baba kwa jitihada za kuwafanya wakue”. Je Mashujaa wa Papa ni akina nani? Hilo lilikuwa ni swali la mtoto mwingine ambalo Papa, kwa mguso wa hisia, alijibu kuwa “ni Mababu na mabibi kwa sababu wana hekima. Na ndiyo sababu ni muhimu kuzungumza nao.”  Mtoto mwingine mkubwa alipendekeza swali gumu zaidi kwamba: “Katika ulimwengu wa kidijitali, tunawezaje kuwa mashujaa?”. Jibu lka Papa lilikuwa ni “Kuitumia kwa manufaa yake, kwa namna ya kuitumia na si kinyume chake”.

Kikundu cha rangi ya blu cha watoto
Kikundu cha rangi ya blu cha watoto

Hata hivyo Padre Franco alionesha vigezo vya kugawanya watoto, kulingana na umri, katika timu za kijani (kutoka miaka 5 hadi 7), njano" (8-10), na bluu (11-13). Vijana wengine wawili waliwasilisha kwa Papa  Francisko maana na malengo ya mpango huo ambao utaendelea hadi tarehe 4 Agosti 2023.  Kwa mujibu wao walisema: “Tunashukuru sana na tunafurahi kushiriki kikamilifu katika uzoefu huu mzuri. Uzoefu wa thamani kwa sisi sote wahuishaji na wahuishaji wasaidizi, kwa sababu unatupatia fursa ya kukua pamoja na watoto hawa ambao hutupatia tabasamu nyingi na kukumbatiwa kila siku”.

Kikundi cha njano cha watoto
Kikundi cha njano cha watoto

Na walisisitiza hasa jinsi toleo hilo linavyoongozwa na Waraka wa Fratelli tutti yaani Wote ni ndugu  ambayo inafanya kama dira katika safari yao, ambayo inalenga kuwafanya vijana kuelewa jinsi ilivyo muhimu kuunda udugu unaoambukiza kati ya watu, ili kwamba kila mtu ahisi kutambuliwa na kuheshimiwa kama ndugu, ili kugundua tena nguvu, thamani na uzuri wa uhusiano wa kindugu”. Njia, ambayo inalenga kusisitiza umuhimu wa mahusiano na kushirikiana kupitia ugunduzi wa hisia na mitazamo ya fadhili kulingana na uaminifu badala ya kuogopa wengine, kwenye mazungumzo badala ya mabishano, kwa ishara za bure na nzuri dhidi ya jeuri na ubinafsi.”

Incontro na vijana
Incontro na vijana

Ni Sinodi ya kweli, yaani mchakato wa safari ya pamoja, ambayo inasaidia wao  wahuishaji na  wasaidizi pia katika kuelewa uzuri wa kile wanachofanya, kwa sababu kutokana na uzoefu huo  wanaweza kujionea umuhimu wa kuishi mahusiano kati ya watu na kuwa ndugu,” alihitimisha mwakilishi huyo wa vijana Giuditta. Na aliyemuunga mkono ni Giacomo, ambaye ni sehemu ya watumbuizaji wasaidizi, yaani watoto wote ambao, baada ya uzoefu wao katika kiangazi, wanaanza tukio jipya, wakati huu wakiwa watumbuizaji halisi. Kwa upande wake amemweleza Papa kwamba wanaposhiriki uzoefu huo kama waigizaji wanakuwa mashujaa wao, wanakuwa watoto ambao walitaka kuwa na shauku yao, mapenzi yao, kwa uwezo waliokuwa nao wa kuwafanya kutabasamu na kupendana kwa sababu hiyo, kuvaa fulana hiyo siku hiyo ilikuwa ni zawadi kubwa  kwao wote na kuwa  fursa nzuri kwa sababu inawasaidia kukua, kuwajibika kwa matumaini kwamba wao pia wataweza kuwa wahuishaji na kuwa sehemu zaidi ya familia hiyo kubwa.

Vijana watoto
Vijana watoto

Mashujaa ni neno lililojirudia katika siku hiyo  likisisitizwa na maelezo ya wimbo wa mwimbaji wa Kiitaliano Mr. Rain ambao unazungumza kwa usahihi umuhimu wa kuwa ndugu. Watoto waliokuwapo waliimba  kwa sauti kubwa, na wakati wa onesho hilo baadhi ya washiriki wa timu ya njano walimzawadia Papa Francisko michoro iliyochorwa kwenye katuni kubwa za rangi, ambayo aliitazama kwa uangalifu mkubwa, akiwapa wafadhili waliochangamkia. Ni neno shujaa lililoandikwa kwenye medali ya kadibodi iliyotolewa kwa Papa, ambaye mara moja aliivaa shingoni mwake. Baada ya mazungumzo mafupi, yaliyojumuisha maswali matatu na majibu mengi, mwigizaji Sergio pamoja na watoto wadogo Federica na Giulia walimpelekea Papa, kwa kuzingatia maandlizi ya kwanda kwenye  Siku ya Vijana Ulimwenguni itakayofanyika Lisbon nchini Ureno,  mkoba wenye ‘T-shirt ya Vijana wa kiangazi’, ili aweze kuuchukua katika safari hiyo. Hatimaye wimbo kuhusu Mashujaa wa Nyuki wa Majira ya kiangazi kwa vijana na timu za mashujaa.

Watoto wakisikiliza Papa
Watoto wakisikiliza Papa

Kabla ya kuondoka katika Ukumbi huo, Papa Francisko aliongoza sala ya Baba Yetu na kuwapatia baraka wale waliohudhuria, akiwataka wawapitishie hata wazazi, mababu na marafiki zao na wasisahau kumwombea. Hata hivyo kabla Baba Mtakatifu alikuwa amekutana katika Ukumbi wa Ukumbi mdogo wa Paulo VI na watumbuizaji na wahuishaji ma  washirika waliounga mkono mpango wa “Majira ya Kiangazi ya Watoto, na ambao  mara moja waliamini katika mpamgo huo na kuuchangia kwa bidii pia na warsha na mipango mingine.

Papa na watoto wa kituo cha kiangazi mjini Vatican.
18 July 2023, 15:59