2023.07.17 Kikundi cha Sala cha "Kijito cha Kanisa hai" kutoka Poland kilikutana na Papa Francisko mjini Vatican. 2023.07.17 Kikundi cha Sala cha "Kijito cha Kanisa hai" kutoka Poland kilikutana na Papa Francisko mjini Vatican.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko alikutana na kikundi cha vijana wa Poland wakiwa hija jijini Roma

Walikuwa ni vijana karibia 150 ambao walikutana kwa faragha na Baba Mtakatifu wakiwa wanahija kutoka Poland hadi Roma tangu tarehe 15 Julai kwa kufanya mafungo ya Jumuiya ya Nur una Uzima yaliyoongozwa na Askofu Mkuu Grzegorz Ryś,wa Jimbo Kuu Katoliki la Łódź,ambaye ni miongozi mwa makardinali wateule.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kulikuwa na takriban vijana 150 na familia za mahujaji kutoka Poland ambao Baba Mtakatifu Francisko aliwapokea katika mkutano wa faragha mjini Vatican asubuhi tarehe 17 Julai 2023. Hawa ni washiriki katika mafungo, yaliyoanza Jumamosi tarehe 15 Julai, wa  jumuiya ya Nuru na Uzima inayojulikana zaidi kama “Oasis of the Living Church”Yaani “Chemi chemi za Kanisa hai”, ambalo ni harakati kubwa zaidi la kikanisa nchini Poland.  Kwa mujibu wa waandishi wetu wa habari  Radio Vatican, wa lugha ya Kipoland Paweł Kowalski SJ na Tomasz Matyka SJ , wametaarifu kuwa   Vijana na familia hizi  hufuata njia ya majiundo ya Kikristo katika vikundi vyao katika parokia wakati wa mwaka na kushiriki katika kipindi kikali zaidi cha mafungo, ambacho kwa kawaida huwaleta pamoja watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Jumuiya hiyo ilianzishwa na Padre Franciszek Blachnicki, aliyeuawa mnamo mwaka 1987 na vyombo vya usalama vya kikomunisti.

Askofu mkuu wa Lodz aliyesindikiza kikundi cha sala " Kijito cha Kanisa hai akizungumza mbele ya Papa
Askofu mkuu wa Lodz aliyesindikiza kikundi cha sala " Kijito cha Kanisa hai akizungumza mbele ya Papa

Hija ya kuja Roma na kukutana na Papa ni hatua muhimu zaidi za mafungo ya ngazi ya tatu kwa vijana na familia. Washiriki walialikwa kuonja fumbo la Kanisa katika utofauti wake na lengo ni kuwasaidia kutafuta njia yao katika jumuiya ya waamini. Wanajifunza kuhusu aina na desturi mbalimbali za maombi, kushiriki katika mikutano ya kindugu na kugundua kina cha historia ya Kikristo na hali ya sasa ya Kanisa kwa kutembelea madhabahu mbalimbali.

Papa na kikundi cha vina wa sala nchini Poland
18 July 2023, 15:16