Papa Francisko Asistisha Huduma za Mfuko wa Msamaria Mwema, Haki na Amani
Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko tarehe 3 Julai 2023 alikutana na kuzungumza na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu, na kumwambia kuhusu nia yake ya kusitisha huduma ya Mfuko wa Msamaria Mwema na Haki na Amani pamoja na Katiba ya Mfuko wa Van Thuân na hivyo kumwelekeza atekeleze nia hii kwa vitendo mintarafu Sheria za Kanisa namba 120 Ibara ya kwanza.
Kumbe, amana na urithi wa Mfuko wa Msamaria Mwema na ule wa Haki na Amani vinaingizwa moja kwa moja kwenye Mfuko wa Van Thuân. Baba Mtakatifu aliamua kwamba, utekelezaji wa agizo hili uanze mara moja tarehe 25 Julai 2023 mara baada ya kuchapishwa kwenye Gazeti la “L’Osservatore Romano” pamoja na kutolewa maoni yake kwenye Jarida la “Acta Apostolica Sedis” linalohifadhi nyaraka zote za Vatican.