Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje ni fursa kwa vijana kufanya hija ya maisha ya kiroho inayowawezesha kukutana na Kristo Yesu. Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje ni fursa kwa vijana kufanya hija ya maisha ya kiroho inayowawezesha kukutana na Kristo Yesu. 

Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje:

Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje ni fursa kwa vijana kufanya hija ya maisha ya kiroho inayowawezesha kukutana na Kristo Yesu katika Ibada ya Misa Takatifu na Kuabudu Ekaristi Takatifu; Kiti cha huruma ya Mungu, yaani katika Sakramenti ya Upatanisho; Katekesi, Sala, Ukimya na katika Rozari Takatifu muhtasari wa historia nzima ya ukombozi. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa kwa 2023.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje, nchini Bosnia na Erzegovina kuanzia tarehe 26-30 Julai 2023 yananogeshwa na kauli mbiu “Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu.” Mt 12:49. Kristo Yesu “Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.” Hawa ndio jamaa za kweli za Kristo Yesu. Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje ni fursa kwa vijana kufanya hija ya maisha ya kiroho inayowawezesha kukutana na Kristo Yesu katika Ibada ya Misa Takatifu na Kuabudu Ekaristi Takatifu; Kiti cha huruma ya Mungu, yaani katika Sakramenti ya Upatanisho; Katekesi, Sala, Ukimya na katika Rozari Takatifu muhtasari wa historia nzima ya ukombozi. Vijana wanakutana na Kristo Yesu kupitia shuhuda mbalimbali, tayari kutambua na kutekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha yao kama ndugu zake Kristo Yesu.

Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!
Tazama, Mama yangu na ndugu zangu!

Hii ni sehemu ya ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje, nchini Bosnia na Erzegovina kuanzia tarehe 26-30 Julai 2023 yanayonogeshwa na kauli mbiu “Tazama, Mama yangu na ndugu zangu.” Mt 12:49. Baba Mtakatifu anasema, kwa haraka haraka majibu ya Kristo Yesu yanaonekana kana kwamba, hayana adabu mbele ya Mama yake, lakini kwa njia ya maneno haya anawanesha wafuasi wake jinsi ya kuambata na kutekeleza mapenzi ya Mungu kwa kujenga mahusiano na mafungamano ya dhati yanayosimikwa katika nguvu ya damu. Utashi wa Mungu ni amana na utajiri usiokuwa na kifani, ni kwa njia hii, Bikira Maria anajenga mahusiano na mafungamano na Kristo Yesu, kiasi hata cha kuwa ni Mfuasi wake amini, Mama wa Mungu, kiasi kwamba, tangu wakati ule, maisha yake yote yalijielekeza katika kutimiza mapenzi ya Mungu. Wakati mwingine ni vigumu kuyafahamu na hatimaye, kuyatekeleza mapenzi ya Mungu katika maisha; kwa kutamani maisha yasiyo na changamoto, mateso na mahangaiko; kwa kutamani kuwa tofauti pengine kwa kuwa na akili nyingi, utajiri mkubwa, karama na mapaji mbalimbali. Lakini hakuna utashi wa Mungu katika maisha; huu ni utashi wa uwepo wa Ufalme wa Mungu, kutokana na kumwogopa Mwenyezi Mungu, wakidhani kwamba, atawatenda kinyume cha matarajio yao au atawapoka uhuru wao. Vijana wanapaswa kwa udi na uvumba kutafuta na kuambata mapenzi ya Mungu katika maisha na kumwomba Kristo Yesu, ili kweli mapenzi ya Mungu yaweze kutendeka katika maisha yao, ili kuwa kweli watoto wa Baba wa milele na kukuza upendo kwa jirani.

Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa
Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa

Baba Mtakatifu anawaalika vijana wa kizazi kipya kujiaminisha mbele ya Mwenyezi Mungu na katika neema yake, kwani wao ni watu wenye thamani kubwa matunda ya kazi ya mikono yake na kwamba, anatambua mahitaji yao ya ndani kabisa; anawapenda upeo kiasi hata cha kutekeleza matamanio yao halali na furaha ya kweli katika maisha. Lakini jambo la msingi kwa vijana ni kutikia wito wake kwa kukubali mpango wake. Baba Mtakatifu anawataka vijana wa kizazi kipya kufurahia maisha ya ujana wao, ili kutengeneza msingi wa maisha yao kwani kesho yao kama mtu binafsi, kitaalum na kijamii inategemea na maamuzi waliyofanya wakati wa ujana wao. Baba Mtakatifu anawaambia vijana wa kizazi kipya kwamba, Bikira Maria awasindikize katika hija hii ya maisha ya kiroho, ili kung’amua na hatimaye, kufahamu mapenzi ya Mungu katika maisha yao, daima wakiwa na matumaini, ari na mwamko mpya. Baba Mtakatifu Francisko anahitimisha ujumbe wake kwa Maadhimisho ya Siku ya 34 ya Vijana Kimataifa huko Medjugorje, nchini Bosnia na Erzegovina kuanzia tarehe 26-30 Julai 2023 kwa kuwataka vijana wawe wamisionari wenye ari na mwamko wa uinjilishaji mpya! Wawapelekee wale wanaoteseka na wale wanaotafuta furaha ya kweli kutoka kwa Kristo Yesu. Vijana wahakikishe kwamba, wanapeleka furaha ya Injili kwenye familia zao, shule, maeneo ya kazi pamoja na kwenye makundi ya vijana wenzao wanakoishi. Wahakikishe kwamba, wanatoa fursa kwa neema ya Mungu itende kazi ndani mwao, kwa kuonesha ukarimu na kwa njia hii, kwa hakika watautengeneza ulimwengu huu kuwa ni mahali pazuri zaidi pa watu wote kuishi!

Vijana Kimataifa

 

27 July 2023, 15:31