Ubalozi wa Vatican,Lisbon Papa asalimia mwanamke wa miaka 106 na kijana mgonjwa
Vatican News
Mkutano mara mbili, asubuhi tarehe 4 Agosti 2023 wa Papa Francisko katika Ubalozi wa Vatican, Lisbon. Kabla ya kuondoka katika makazi yake kwa siku hizi za ziara yake kuelekea mji mkuu wa Ureno kwenye bustani ya Vasco da Gama ambako ataungamisha baadhi ya vijana, Papa Francisko alikutana kwa muda mfupi na bibi mwenye umri wa miaka 106, Maria da Conceição Brito Mendonça, aliyezaliwa katika siku ya tokeo la Mama Maria wa Fatima, tarehe 13 Mei 1917.
Hayo yameripotiwa na Ofisi ya Habari ya Vatican, ikifahamisha kwamba, mara baada ya hapo, Papa Francis koalimsalimia kijana mmoja Edna Pina Lopes Rodrigues, ambaye anaumwa ugonjwa mbaya na ambaye Papa mwenyewe alimtumia ujumbe wa upendo na sala mnamo mwezi Juni uliyopita.