Papa Akutana na Vijana wa Chuo Kikuu Katoliki:Ishara ya Ukarimu Huzaa Mabadiliko

Papa akihutubia wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno aliokutana nao,Lisbon aliwahimiza wasibadilishe nyuso zao na skrini ,badala yake wawe wajasiriamali wa ndoto, sio wasimamizi wa hofu na kujikita na elimu katika huduma ya wengine. Amegusia kuhusu umuhimu wa ikolojia,ya siasa na uchumi mpya na kutoa kipaumbele cha kwanza kwa ubinadamu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Kutazama changamoto kubwa, kulia kwa uchungu ambayo ndiyo sifa ya wakati huu wa kihistoria lakini si vizuri kukumbatia hatari ya kufikiria kuwa hatuko kwenye uchungu, bali kuwa mwanzoni mwa onesho kubwa. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko amewatikisa wanafunzi vijana wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno alipokutana nao, Alhamisi  tarehe 3 Agosti 2023, kama sehemu ya mpango wa mikutano yake kwenye fursa ya Siku ya Vijana duniani iliyoanza  tarehe Mosi na itahitimishwa Dominika tarehe 6 Agosti 2023. Kwa njia hiyo wanafunzi wa Chuo Kikuu Katoliki, Ureno walimkaribisha kwa shangwe kubwa kati ya nyimbo za kwaya. Baba Mtakatifu katika hotuba yake amewaalika kuwa wajasiriamali wa ndoto, na sio wasimamizi wa hofu, wasiridhike na majibu rahisi ambayo yanatia ganzi, wawe na ujasiri wa kubadilisha hofu ziwe ndoto. Katika chuo kikuu, kujilinda ni kishawishi, kielelezo kinachosababishwa na woga. Kwa hiyo amesema "Ingekuwa ni kupoteza kufikiria chuo kikuu kilichojitolea kufundisha vizazi vipya ili kuendeleza mfumo wa sasa wa wasomi na usio na usawa wa ulimwengu, ambayo elimu ya juu imesalia kuwa fursa kwa wachache; ikiwa wale waliopata elimu ya juu hawafanyi jitihada za kurudisha kile ambacho wamefaidika nacho, hawajaelewa kikamilifu kile ambacho wamepewa”.

Papa amehutubia vijana wa Chuo Kikuu katoliki Ureno
Papa amehutubia vijana wa Chuo Kikuu katoliki Ureno

Kiukweli, sifa ya elimu haipaswi kuonekana kama leseni ya kujenga ustawi wa kibinafsi tu, bali kama jukumu la kujitolea kwa haki zaidi na jumuishi, yaani, jamii iliyoendelea zaidi. Sisi sote ni mahujaji na kila msafiri hutafuta na kuwa na hatari kwa hiyo Papa Francisko amesisisitiza akitoa mwaliko wa "kutoamini fomula zilizotungwa, zenye majibu ambayo yanaonekana kufikiwa, mapendekezo ambayo yanaonekana kutoa kila kitu bila kuuliza chochote”. Papa amesisitiza kwamba wasiogope kamwe kuhisi kutokuwa na utulivu: kiukweli, kutoridhika ni dawa nzuri dhidi ya dhana ya kujitosheleza na kiburi. Kila mmoja wetu ni msafiri, mtafutaji, ambaye anahisi mara kwa mara kutokamilika kwake, kama Yesu asemavyo, kuwa "Tumo ulimwenguni, lakini si wa ulimwengu’. Hivyo basi Papa amesema huku "ni kutiwa moyo ili tusiwe na wasiwasi tukijikuta tuna kiu ndani mwetu. Sisi sio wagonjwa, lakini tuko hai! Afadhali tuwe na wasiwasi wakati tuko tayari kubadilisha barabara iliyo mbele yetu na sehemu yoyote ya kiburudisho, mradi tu inatupatia udanganyifu wa faraja; tunapobadilishwa nyuso na skrini, halisi na za mtandaoni; wakati badala ya kujiuliza maswali ya kurarua, tunapendelea majibu rahisi ambayo yanatia ganzi", Papa alifafanua.

Papa amehutubia wanachuo Kikuu katoliki cha Ureno
Papa amehutubia wanachuo Kikuu katoliki cha Ureno

Papa akiendelea na hotuba yake kwa vijana hao  “Ni wakati wa kufafanua upya kile tunachokiita maendeleo na mageuzi kwa sababu katika jina la maendeleo kuna kurudi nyuma sana kunakojionesha. Ndiyo kwa maono ya jumla, lakini hapana katika ubaguzi. Ninyi ndiyo kizazi kinachoweza kushinda changamoto hii: kwa sababu mna zana za hali halisi ya juu zaidi za kisayansi na kiteknolojia, lakini tafadhali msiingie kwenye mtego wa maono kidogo. Msisahau kwamba tunahitaji ikolojia fungamani, kusikiliza mateso ya sayari pamoja na yale ya maskini; kujikita katika dharura ya kuenea kwa jangwa sambamba na ile ya wakimbizi; mada ya uhamiaji pamoja na ile ya kushuka kwa viwango vya kuzaliwa; kukabiliana na mwelekeo halisi wa maisha ndani ya mwelekeo wa kiroho”, Papa ameorodhesha majanga ya kisasa.

Ushuhuda wa mwanafunzi wa chuo Kikuu katoliki Ureno
Ushuhuda wa mwanafunzi wa chuo Kikuu katoliki Ureno

Mkutano katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lisbon kwa hiyo ulikuwa mazungumzo ya kweli! Kwa hakika, maneno ya Papa Francisko yalikuja kama jibu kwa yale ambayo vijana wanne walikuwa wamezungumza naye muda mfupi kabla  ya kuanza hotuba yake kuhusu mada za Laudato Sì, Mkataba wa Elimu ya Kimataifa, Uchumi wa Francisko na Utamaduni wa kukutana. Kwa vijana Beatriz, Mohoor, Mariana, Tomás,  Baba Mtakatifu amewashukuru kila mmoja kwa ushuhuda wao wa matumaini, shauku ya kweli, bila malalamiko au kukurupuka kiukweli. Ni kweli, yeye alisema, “ikolojia fungamani haiwezekani bila Mungu; haitoshi kwa Mkristo kusadikishwa, lazima awe anasadikisha kwa kuakisi furaha ya Injili; bila kujikita ndani mwake, hata katika uwanja wa utamaduni, Ukristo unakuwa itikadi”. Kwa kila mtu, Baba Mtakatifu ameuliza “Je mnataka kuona nini kikitengenezwa nchini Ureno na ulimwenguni?” Na kwa hiyo aliwambia shauku yake kwamba “ Hata Mzee huyu anayezungumza nanyi  pia ana ndoto ya kizazi chenu kuwa kizazi cha walimu. Walimu wa hubinadamu. Walimu wa  Huruma. Walimu wa fursa mpya kwa ajili ya sayari na wakazi wake. Walimu wa Matumaini.”

Papa akisalimiana na wanachuo kikuu katoliki Ureno
Papa akisalimiana na wanachuo kikuu katoliki Ureno

Akiitazama sayari iliyotishiwa na uharibifu mkubwa wa ikolojia na vita vya tatu vya ulimwengu, Papa Francisko alihimiza kila mtu kusoma Mkataba wa Kielimu kimataifa kwa shauku, ili kukabiliana na migogoro. Kwa njia hiyo alitoa wito kwa ajili ya uongofu wa moyo unaoongoza mabadiliko katika maono ya kianthropolojia ya siasa na uchumi; Wito wa kukubalika na kujumuishwa kwa wale walio mbali na nchi yao wenyewe. Kwa kuongezea Papa amesema: “Ishara ya ukarimu huleta mabadiliko”. Miongoni mwa mambo mengine ya mkataba Kimataifa wa kielimu ambao  Papa Francisko ametoa nuru yake  ni ushiriki kamili wa wanawake.  Papa amesema “Mara nyingi sana katika fahamu ya pamoja tunazingatia wanawake kuwa wa daraja la pili, mbadala, hatuwapi nafasi ya wahusika wakuu. Kiukweli, mchango wa mwanamke ni muhimu sana. Kwani, Biblia huonesha jinsi uchumi wa familia ulivyo katika  sehemu kubwa mikononi mwa wanawake. Yeye ndiye mtawala wa kweli wa nyumba, na hekima ambayo haina faida pekee kama lengo lake, lakini la utunzaji, kuishi pamoja, ustawi wa kimwili na kiroho kwa wote, pamoja na kushirikiana na maskini na wageni.”, Papa alisisitiza.

Kama haitoshi Baba Mtakatifu kwa vijana hawa ametumia picha halisi ya Hija ili kuwatia moyo wanafunzi vijana wa chuo kikuu kwenda mbele. Akinukuu semi za salamu ambazo, kulingana na mapokeo ya enzi za kati, wasafiri wa Njia ya Santiago ya Compostela walibadilishana hivi: “Nenda mbele zaidi, juu zaidi; njoo na songa mbele”. Kwa hiyo kuwa chuo kikuu katoliki kunamaanisha zaidi ya haya yote kwamba kila kipengele kinahusiana na kitu kizima na kwamba kitu kizima kinapatikana kutoka katika sehemu. Kwa hivyo, wakati wa kupata ujuzi wa kisayansi, mtu hukomaa kama mtu, kwa kujijua mwenyewe na katika utambuzi wa njia yake mwenyewe”. Kwa hivyo amewahimiza wasonge mbele zaidi.

Mkuu wa Chuo kikuu katoliki Ureno akimkaribisha Papa
Mkuu wa Chuo kikuu katoliki Ureno akimkaribisha Papa

Hatimaye katika mkutano, Papa Francisko alibariki jiwe la Msingi la Campus  mpya Veritati. Na wakati huo huo Baba Mtakatifu  alisalimiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ureno, Profesa Isabel Capeloa ambaye katika hotuba yake ya kumkaribisha alisisitiza kuwa : “Chuo kikuu hakipo ili kujihifadhi kama taasisi, lakini kujibu kwa ujasiri changamoto za sasa na za baadaye na  itakuwa mpango  kila wakati, sio kazi iliyokamilika. Mkuu huyo wa chuo kikuu katoliki baadaye alitangaza kuzaliwa chombo kipya kiitwacho “Uchumi wa Francisko na Clara”, aliyejitolea kukaribisha mipango katika Vyuo vyote vya kukuza kanuni za Uchumi wa Francisko na kukuza mtindo wa kijamii unaothamini watu na mazingira.

Papa akutana na vijana wa Chuo Kikuu katoliki Ureno
03 August 2023, 12:19