Tafuta

Papa alikutana na kikundi cha wathirika wa unyanyasaji  katika Jengo la Ubalozi wa kitume Lisbon. Papa alikutana na kikundi cha wathirika wa unyanyasaji katika Jengo la Ubalozi wa kitume Lisbon.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa anakutana na kundi la wahanga wa unyanyasaji wa makasisi,Ureno

Katika Ubalozi wa kitume wa Vatican huko Lisbon,Papa alikutana na watu 13 waliosindikizwa na baadhi ya wawakilishi wa taasisi za kikanisa wanaohusika na ulinzi wa watoto.Mkutano huo ulikuwa na usikilizaji kwa makini na ulidumu kwa zaidi ya saa moja baada ya Masifu ya jioni.Mnamo Februari,Kanisa la Ureno lilitoa ripoti ya Tume huru ya uchunguzi kuhusu unyanyasaji.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Mkutano wa Papa Francisko jioni  ya tarehe 2 Agosti 2023 na kundi la watu 13, waathiriwa unyanyasaji kutoka kwa makasisi wa Ureno, ulichukua zaidi ya saa moja na ulifanyika katika hali ya usikilizaji mkubwa.  Hayo ndiyo yalidhibitishwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, ikieleza kwamba mkutano huo ambao ulikuwa unahitimisha siku ya kwanza nchini Ureno  ulifanyika mwisho wa mikutano ya kitaasisi na Kikanisa  kumalizika muda mfupi baada ya 2:15 usiku. Papa alipokea kikundi hicho katika Ubalozi wa Vatican huko Lisbon, makazi yake kwa siku hizi za safari ya 42 ya kitume kwa siku ya Vijana Ulimwenguni(WYD). Walioandamana na wahanga hao pia walikuwamo baadhi ya wawakilishi wa taasisi za Kanisa la Ureno zinazosimamia ulinzi wa watoto wadogo na katika mapambano dhidi ya janga hili la Kanisa. Moja ya kashfa ambayo inaharibu sura yake, ambayo Papa alitaja wakati wa  Tafakari ya Masifu ya jioni  na Maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume, wasemiari, mashemasi, na watu wa huduma ya kichungaji katika Monasteri ya Jeronimos.

Kuchapishwa huko Lisbon kwa ripoti ya mwisho ya Tume Huru (CI) ya uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto katika Kanisa Katoliki nchini Ureno ilianza hadi Februari iliyopita, ambayo ilithibitisha shuhuda 512, kati ya jumla ya 564 zilizopokelewa, zinazohusiana na kesi zilizotokea kati ya  mwaka 1950 na 2022. Ripoti hiyo ilitangazwa na Baraza la Kudumu la Maaskofu wa Ureno (CEP) wakati wa mkutano wa mtandaoni mwezi Desemba 2022. Katika kuhusiana na  hilohilo, habari zilitolewa kuhusu mkutano huo usio wa kawaida wa maaskofu wa Kanisa hilo na ambapo Nchi ya Ureno mnamo  tarehe 3 Machi 2023,  walikutanika kuchambua utafiti wa Tume Huru kuhusu unyanyasaji.


Mkutano ulifanyika Fatima na kuona maaskofu wakiahidi kuongeza juhudi zao ili kupambana na uhalifu huu ndani ya Kanisa. Kwa ajili hiyo, Askofu José Ornelas, rais wa Baraza la Maaskofu(CEP), alikuwa ametangaza kuhusika kwa Majimbo na taasisi mbalimbali za kitawa, pamoja na maaskofu wa majimbo  na wasimamizi wakuu wa mashirika. Kisha Baraza la Maaskofu wa Ureno lilihakikisha kuwa kwa msaada wa kiroho, kisaikolojia na kiakili kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia katika miundo iliyopo katika Kanisa na kutangaza katika taarifa kwamba maaskofu watatoa ishara inayoonekana ya kujitolea kwao kwa ajili ya  “Ukumbusho wa Siku ya Vijana Duniani wa waathirika.“

Baraza la Kudumu la CEP lilikutana tena huko Fatima, katikati ya mwezi Aprili iliyopita, ili kuthibitisha ahadi zilizotolewa na Kanisa ili tabia na mitazamo ya zamani isirudiwe tena. Tarehe 20 Aprili 2023  ilifanyika siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya wahanga wa unyanyasaji wa kijinsia, matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya dhamiri katika Kanisa; Maaskofu pia walikuwa wametangaza kuundwa kwa kikundi cha kusindikiza  kwa ajili ya kuandamana na wahasiriwa wa unyanyasaji, chini ya uenyekiti wa mwanasaikolojia Rute Agulhas.

Papa akutana na wahanga wa unyanyasaji
03 August 2023, 10:12