Tafuta

2023.08.26  Papa na Wawakilishi wa Tuzo ya "Ni Uandishi wa Habari." 2023.08.26 Papa na Wawakilishi wa Tuzo ya "Ni Uandishi wa Habari."  (Vatican Media)

Papa kwa waandishi wa habari:Tangaza ukweli wa Sinodi sio kauli mbiu!

Tazameni ukweli wa mambo,msijiruhusu kushawishiwa na lugha ya chuki.Haya ni baadhi ya vipaumbele vilivyooneshwa na Papa kwa Waandishi wa habari katika mkutano wao mjini Vatican,pamoja na ujumbe wa tuzo ya:“Ni Uandishi wa habari”iliyoanzishwa mwaka 1995 na kukabidhiwa kwa Baba Mtakatifu.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na Ujumbe wa Uwakilishi wa  Ulimwengu Waandishi wa habari, wakiwa katika Mkutano wao mjini Vatican, Jumamosi tarehe 26 Agosti 2023, ambapo wajumbe hao wa Tuzo iliyoanzishwa mwaka 1995 na kukabidhiwa kwa Baba Mtakatifu.  Katika hotuba yake  amewasalimia na kuwashukuru kwa mkutano huo na fursa ya kutunukiwa Tuzo ya: “Ni  Uandishi wa Habari”. Lazima wajue kwamba, hata kabla ya kuwa Askofu wa Roma, alikuwa akikataa zawadi. “Sijawahi kupokea, na sikutaka. Na Papa amesema aliendelea kufanya hivyo hata akiwa Papa. Hata hivyo, kuna sababu iliyomfanya akubali yao,  nayo “ni uharaka wa mawasiliano yenye kujenga, ambayo yanapendelea utamaduni wa kukutana na sio wa kugombana; utamaduni wa amani na sio wa vita; utamaduni wa uwazi kwa wengine na sio chuki”. “Nyinyi nyote ni wafuasi mashuhuri wa uandishi wa habari wa Italia. Niruhusu, basi, niwe na  tumaini na pia kushughulikia kwa uwazi ombi la usaidizi. Lakini siwaombei pesa, tulieni”, Papa aliongeza.

Baba Mtakatifu amesema kwa waandishi wa habari hao kuwa: “Tumaini ni hili: kwamba leo, wakati ambapo kila mtu anaonekana kutoa maoni juu ya kila kitu, hata bila kujali ukweli na mara nyingi hata kabla ya kujijulisha, kanuni ya ukweli itagunduliwa tena na kurudishwa kuchimba zaidi na zaidi kwamba  ukweli ni bora zaidi, kuliko  wazo, daima kwamba ukweli wa ukweli, mabadiliko ya ukweli; ambayo hautembei kamwe na hubadilika kila mara, kuelekea mema au mabaya, ili kutoweka hatari ya jamii ya habari kugeuka kuwa jamii ya upotoshaji. Baba Mtakatifu amekazia kusema kwamba upotoshaji ni moja ya dhambi za uandishi wa habari, ambazo ni nne: upotoshaji, wakati uandishi wa habari hautoi taarifa au kupotosha; kashfa (na wakati mwingine hii hutumiwa); kashfa, ambayo ni tofauti na upotoshaji lakini huharibu; na ya nne ni (coprophilia), yaani, upendo kwa kashfa, kwa uchafu, kashfa inauzwa. Kashfa  ni ya kwanza ya dhambi, ya makosa  na  tuseme  ya uandishi wa habari.”

Ili kupinga hili, hata hivyo, kuna haja ya kueneza utamaduni wa kukutana, utamaduni wa mazungumzo, utamaduni wa kusikiliza mwingine na sababu zake. Utamaduni wa kidijitali umetuletea uwezekano mwingi mpya wa kubadilishana, lakini pia unahatarisha kubadilisha mawasiliano kuwa kauli mbiu. Papa ameongeza kusema “Hapana, mawasiliano yamekuwa yakienda na kurudi. Ninasema, sikiliza na ujibu, lakini mazungumzo kila wakati. Sio kauli mbiu.” Kwa mfano, nina wasiwasi kuhusu ghiliba za wale wanaoeneza habari za uwongo kwa ubinafsi ili kuongoza maoni ya umma. Tafadhali, tusikubali mantiki ya upinzani, tusikubali kuathiriwa na lugha za chuki,”, Papa ameonya

Katika hali ya kutisha ambayo Ulaya inapitia, pamoja na kuendelea kwa vita huko Ukraine, tunaitwa kuchuchumalia uwajibikaji. Matumaini ya Baba Mtakatifu  ni kwamba nafasi itatolewa kwa ajili ya  sauti za amani, kwa wale ambao wamejitolea kukomesha hii kama migogoro mingine mingi, kwa wale wasiosalimu amri kwa mantiki ya vita lakini wanaendelea kuamini, licha ya kila kitu, katika amani, kwa ajili ya mantiki ya mazungumzo, na kwa mantiki ya diplomasia. Baba Mtakatifu Francisko akiendelea hotuba yake kwa waandishi wa habari amekijita katik kutoa wito wa msaada. Hasa katika wakati huu, ambapo kuna mazungumzo mengi na usikilizaji mdogo, na mahali ambapo maana ya hatari ya manufaa ya wote inadhoofika, Kanisa zima limeanza mchakato wa safari ya kugundua tena neno  la pamoja. Kwa hiyo “Lazima tugundue tena neno hilo pamoja.”

Kutembea pamoja. Kujiuliza  kwa pamoja. Kuchukua jukumu la utambuzi wa jumuiya, ambalo kwetu sisi ni sala, kama Mitume wa kwanza walivyofanya: ni sinodi, ambayo tungependa kufanya tabia ya kila siku katika usemi wake wote. Kwa kusudi hili hasa, katika muda wa zaidi ya mwezi mmoja tu, maaskofu na waamini kutoka sehemu zote za dunia watakusanyika jijini  Roma kwa ajili ya Sinodi ya kisinodi: kusikiliza pamoja, kupambanua pamoja, kusali pamoja. Kwa hiyo “Neno pamoja ni muhimu sana. Tuko katika utamaduni wa kutengwa, ambao ni aina ya ubepari wa mawasiliano. Labda sala ya kawaida ya kutengwa hivyo kwa kusema: “Nakushukuru, Bwana, kwa sababu mimi si hivyo, mimi si kama hivyo, mimi si ... wanatengana.  Badala yake Tunapaswa kumshukuru Bwana kwa mambo mengi mazuri!”

Papa amesisitiza kuwa anaelewa vizuri kwamba kuzungumzia juu ya “Sinodi ya kisinodi kunaweza kuonekana kuwa jambo lisiloeleweka, la kujirejea, la kiufundi kupita kiasi, lisilovutia sana umma. Lakini kile kilichotokea katika mwaka uliopita, ambao utaendelea na Mkutano wa mwezi Oktoba ijayo na kisha kwa hatua ya pili ya Sinodi ya 2024, ni jambo muhimu sana kwa Kanisa.” Papa amethibitisha. “Ni safari ambayo Mtakatifu Paulo VI aliianzisha, mwishoni mwa Mtaguso, II alipounda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu, kwa sababu alitambua kwamba katika Sinodi ya Kanisa la Magharibi ilishindikana, ambapo katika Kanisa la Mashariki wana mwelekeo huo. Ni Mchakato wa safari  hii ya miaka mingi, miaka 60 ambayo imezaa matunda mazuri. Kwa hiyo Papa ameomba sana kuzoea  kusikilizana, kuzungumza, na sio  kusumbuka vichwani kwa neno lolote.”

Baba Mtakatifu aidha amejikita na kipengele cha Kusikiliza, kujadili kwa njia ya ukomavu. Hii ni neema ambayo sote tunahitaji kusonga mbele”. Na ni jambo ambalo Kanisa linaupatia ulimwengu leo hii , ulimwengu ambao mara nyingi hauwezi kufanya maamuzi, hata wakati uhai wetu huko hatarini. Tunajaribu kujifunza njia mpya ya kuishi mahusiano, kusikilizana ili kusikia na kufuata sauti ya Roho. “Tumefungua milango yetu, tumempa kila mtu fursa ya kushiriki, tumezingatia mahitaji na mapendekezo ya kila mtu. Tunataka kuchangia pamoja katika kujenga Kanisa ambapo kila mtu anahisi yuko nyumbani, ambapo hakuna anayetengwa. “Neno hilo la Injili ambalo ni muhimu sana na la  kila mtu. Hakuna Wakatoliki wa daraja la kwanza, la pili, na la tatu, hapana. Wote pamoja. Kila mtu. Ni mwaliko wa Bwana.”

Kwa hilo Papa Francisko amethubutu kuomba msaada kutoka kwa waandishi wa habari ambao amewaita “mabwana wa uandishi wa habari”: kwamba wamsaidie kuelezea mchakato huo kwa nini ni kweli na kuacha nyuma mantiki ya itikadi na historia zilizowekwa tayari.  Na kumbe hapana bali ni ukweli. Mtu fulani alisema: “Ukweli pekee ni ukweli”. Ndiyo, ukweli. Sote tutafaidika na, nina hakika, huu pia ni uandishi wa habari!. Kwa kuhitimisha Papa kwa mara nyingine tena amewashukuru kwa mkutano huo, kwa maana yake kuhusiana na ahadi yao ya pamoja ya ukweli na amani. Amewakabidhi wote kwa maombezi ya Maria na kuwaomba wasisahau kumuombea.

Papa na wanahabari
26 August 2023, 12:12