Tafuta

 Schola Occurrentes ni harakati ya kimataifa ambayo pia Papa atatembelea huko Lisbon. Schola Occurrentes ni harakati ya kimataifa ambayo pia Papa atatembelea huko Lisbon.  (ANSA)

Papa Francisko na mchoro wa kihistoria,mkutano na vijana wa Scholas huko Cascais

Tarehe 3 Agosti 2023, Papa atakwenda karibu na Lisbon kukutana na wavulana na wasichana wanaoshiriki katika jumuiya hiyo,mwishoni mwa mpango wa Maisha kati ya walimwengu.Baba Mtakatifu atapaka rangi kwa brashi kwenye ukuta wenye kilomita 3 ambao vijana wamefanyia kazi na ambao unawakilisha umoja kati ya ulimwengu tofauti.

Vatican News

Papa Francisko atapaka rangi kwa brashi kwnye ukuta uliopewa jina: Mapinduzi ya ulimwengu mpya  ambao vijana wa Scholas Occurrentes wanaota. Mnamo tarehe 3 Agosti, 2023 kama sehemu ya ziara yake  nchini  Ureno kwa ajili ya  Siku ya WYD, Papa  Francisko anatarajiwa kusafiri hadi Cascais, mji wa magharibi mwa Lisbon, hasa kukutana na wavulana na wasichana wanaoshiriki katika jumuiya hiyo. Wakati wa shughuli hiyo, atazungumza na vijana na kuweka miguso ya mwisho na rangi kwa kutumia brashi  kwenye ukuta wa kilomita 3 ambao jumuiya inafanyia kazi. Mkutano huo utakuwa ni kufunga mpango uitwao ‘Maisha kati ya walimwengu’, ambao unajumuisha uundaji wa ukuta unaounganisha watu ulimwengu.  Kwa hiyo  Wazee, vijana, matajiri, maskini, watoto wa dini mbalimbali na wasioamini na vijana wa mataifa mbalimbali walishiriki katika mchoro huo.

Del Corral: Uzoefu ambao unabadilisha maisha yetu

José María Del Corral, rais wa Kimataifa  wa Harakati ya Scholas Occurrentes, alisema kuwa: “Tunamshukuru sana Papa Francisko na waandaaji wa Siku ya Vijana Ulimwenguni Lisbon 2023 kwa juhudi za kuja kututembelea Cascais na kushiriki nasi uzoefu huu wa elimu hiyo inayobadilisha maisha yetu na kutupatia tena hisia ya kusimama na kuendelea kupambana. Ziara ya Papa Francisko katika makao makuu yetu ni uthibitisho ambao Scholas ameupokea kwa kujitolea kwake katika elimu bora, ushirikiano na kukuza maadili ya binadamu.”

Mpango wa maisha kati ya ulimwengu

Mpango wa  ‘Maisha kati ya ulimwengu’ unalenga kumwilisha dira ya ufundishaji wa Baba Mtakatifu Francisko kwa kumulika  umuhimu wa kile kiitwacho KATI, ambapo watu wanakutana, kati ya watu na dunia, kati ya dunia na maisha, ambapo maisha yanapata tena maana yake. Mpango huo unahusisha uundaji wa mchoro wenye urefu wa kilomita 3 uliotokana na mikutano ya kidini, ya vizazi na ya kiutamaduni iliyofanywa kwa ajili ya maandalizi ya ziara ya Papa Francisko na  jumuiya ya Scholas huko Cascais, nchini Ureno.

Ukuta wa  vijana

Ukuta wa Maisha kati ya Ulimwengu  iliyoundwa na jumuiya nzima, ulizaliwa kutoka makao makuu ya Scholas, ambapo vijana kutoka nchi mbalimbali walikutana ili kushiriki maumivu na ndoto zao na kuunda kazi ya sanaa ya kina, yaani walifanya kama ‘darasa bila kuta halisi’. Kwa wiki mbili, vijana walikutana na kuishi, kama katika kila moja ya uzoefu ambao ni sehemu ya mpango huu, wa Sanaa, Mchezo na Mawazo. Zaidi ya watu 2000 walishiriki katika uundaji wa ukuta huo, katika vikundi vya watu 5-10, ambao kwa pamoja waliunda ukuta 300 ambazo zililetwa pamoja katika kazi moja ya sanaa.

Scholas Occurrentes ni Harakati ya kimataifa yenye haki ya kipapa

Ikumbukwe kuwa  Scholas Occurrentes ni Harakati ya Kimataifa ya Kielimu yenye Haki ya Kipapa, kwa hiyo inayotambulika ambayo iliyoundwa na hati ya  Baba Mtakatifu Francisko, na ambayo imetawanyika kwenye mabara 5 na ambayo kupitia mtandao wake inaunganisha zaidi ya shule nusu milioni na mitandao ya elimu. Dhamira yake ni kuitikia wito wa kuunda Utamaduni wa Kukutana kwa kuwaleta vijana pamoja katika elimu inayozalisha “MAANA”.

01 August 2023, 15:59