2023.08.03 Papa amechora kwenye ukuta wa mchoro mkubwa uliotengenezwa na vijana wa Scholas Occurrentes  mara baada ya kuzungumza nao 2023.08.03 Papa amechora kwenye ukuta wa mchoro mkubwa uliotengenezwa na vijana wa Scholas Occurrentes mara baada ya kuzungumza nao  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko na vijana wa Scholas Occurrentes&mchoro mkubwa sana!

Papa Francisko amekutana na vijana wa Scholas Occurrentes ambao wameshiriki katika mpango wa Maisha kati ya walimwengu, ambao umehusisha watu wa mataifa na dini tofauti,waliojitolea kuunda moja ya mchoro mkubwa zaidi ulimwenguni. Papa ametania kuwa kama kikanisa cha Sistina na kujibu maswali ya vijana kwamba maisha bila shida hayana maana

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ni kama Kikanisa cha Sistine mlichora amesema Papa akiinua kichwa chake juu na kugeuza macho kulia na kushoto kakitazama uzuri wa ndani, jinsi unavyofurahisa sana mchoro wenye kilomita 3.5 ambao umechorwa na vijana wa Scholas Occurrentes, ambapo yeye mwenyewe kabla ya kuondoka kama jinsi ilivyokuwa imepangwa ameweka mkono wake kwa kuchora midura mitatu.  Ili kuwa kama saini ya kiongozi wa Roma kwa wakatoliki wa ajili ya ulimwengu mpya anaouota kwa  vijana ambapo yeye mwenyewe amewaalika kuchafua mikono yao, ili wasichafue maisha ya! Baba Mtakatifu Francisko akiwa huko Cascais,  Asubuhi tarehe 3 Agosti 2023, katika pwani ya kilomita chache magharibi mwa Lisbon, aliweza kukaa na vijana wa kike na kiume takriban saa moja ambalo ni Shirika la Kimataifa la Scholas Occurrentes  lililoenea katika nchi 190,  na ikiwa ni sehemu ya siku yake ya pili akiwa nchini Ureno kwa ajili ya Siku ya vijana Duniani ( WYD) iliyofunguliwa tarehe Mosi Agosti  2023 na ambayo itamuona Papa  Francisko katika matukio mbali mbali hadi 6 Agosti 2023.

Papa ameulizwa maswali na vijana wa Scholas
Papa ameulizwa maswali na vijana wa Scholas

Akiwasili kwa gari dogo jeusi, Papa alikaribishwa na nyimbo na vifijo vya "karibu Francisko” katika shule hii ya zamani iliyogeuzwa kuwa nyumba, iliyotolewa kutokana na makubaliano na serikali ya Ureno na ambayo imekuwa makao makuu ya mpango wa “Maisha kati ya walimwengu”. Mpango uliohusisha wazee na vijana, matajiri na maskini, waamini na wasioamini, mataifa tofauti, wote walijitolea kuunda kazi adhimu ya sanaa.  Ni mojawapo ya michoro mikubwa zaidi ulimwenguni, kwa  maoni ya Mkurugenzi José Maria del Corral, ambaye alimpatia Papa  Francisko brashi fulani, iliyopachikwa sanamu nyeupe iliyotengeneza na   watu wa Afrika. Papa alitabasamu, kisha anainuka kutoka kwenye kiti  katikati ya macho ya vijana, alikwenda kwenye ukuta nyuma yake ili kuchora miduara mitatu ya kijani katika hatua ambayo tayari ina alama za rangi tofauti!

Mchoro mzuri iliochorwa na watu wa mataifa katika Scholas Occurentes
Mchoro mzuri iliochorwa na watu wa mataifa katika Scholas Occurentes

Katika mkutano huo kama ule uliofanyika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huuu katika Chuo Kikuu cha Baba wa Kanisa Augustinianum, Roma, ulikuwa kwanza ni  mfululizo wa maswali na ushuhuda kutoka kwa vijana. Wakati huu sio tu vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia, lakini kutoka hata dini mbalimbali ambao waliuliza  baadhi ya maswali Papa au kushirikisha maoni yao juu ya mpango huo unaounganisha sanaa, utamaduni na kwa namna fulani, imani. Kuna Paulo, mwinjili, ambaye alisema ameridhika kwa sababu watu wanajieleza kwa kila mmoja katika dini tofauti, tamaduni tofauti, haijalishi, kila mtu anakaribishwa katika Scholas”. Kisha Mariana, Mkatoliki, ambaye alizungumzia ukuta kama kitu ambacho ni zaidi ya uchoraji au kuwa pamoja lakini badala ya historia, maisha na kushiriki mengi. “Nadhani kuna matumaini kidogo sana kwa watu siku hizi na inabidi tuelewe kweli kwamba ndani ya watu pia kuna tumaini hilo na nia ya kuishi, hata ikiwa wakati mwingine imefichwa nyuma ya tabasamu kidogo”, alisema

Papa akutana na vijana Vijana wa Scholas Ocurrentes

Hatimaye Aladje, Muislamu, ambaye alifichua kuwa alipenda harakati hiyo ambayo "haioni rangi, haioni dini, haioni utamaduni wetu kwa kila hali, bali inathamini tamaduni zilizopo na kuishia kusaidia watu kutoka asili tofauti. Scholas ni eneo la tamaduni nyingi kwa maana hii na tunaingia shuleni bila kuacha dini yetu kando”, alisema kijana huyo. Papa alisikiliza na kisha alijibu kwa kihispania. Juu ya yote alijikita na dhana ya mgogoro. Yale ambayo yana maana hasi lakini ambayo matunda mazuri yanaweza pia kutokea. “Katika mizozo lazima utembee, mara chache peke yako na hii pia ni muhimu. Kukabiliana na shida pamoja na kusonga mbele, kukua, kwani maisha bila shida ni kama maji yaliyotiwa mafuta”. Ni ya asili, hauna ladha, hauwezi kunywewa, hana faida isipokuwa kuhifadhiwa. Mgogoro huo, hata hivyo, kulingana na Papa Francisko lazima ukumbwe, kukubaliwa, kukabiliwa na kutatuliwa. Pia kwa sababu kutoka kwake, hiyo ni kutoka kwa machafuko haya  ambayo kila mmoja wetu anapitia maishani, maisha mapya yanaweza kuzaliwa.

Vijana wa Scholas Occurrentes wakizungumza na Papa
Vijana wa Scholas Occurrentes wakizungumza na Papa

Kulikuwa na mtu ambaye alisema kwamba safari ya mwanadamu, maisha ya mwanadamu, ni kutengeneza maelewano  kutokana na machafuko Papa Francisko alisema akimaanisha Carl Gustav Jung. Kwa kile kisicho na maana, ni nini kibaya, huunda ulimwengu. Kwa maana iliyo wazi ya kuvutia na inayojumuisha. Hapa sitaki kuwa katekista, Papa alitania, lakini masimulizi yale yale ya uumbaji, yenye lugha ya kishairi yanaonesha hilo kwamba  bila kitu, kitu kinazaliwa: Mungu siku moja hufanya nuru na huenda akabadilisha mambo. Jambo hilo hilo hufanyika katika maisha yetu kwani  kuna wakati muhimu, wenye machafuko sana, ambapo hatujui jinsi ya kusimama. Sote tunapitia nyakati hizi… alisema  Papa. Na hapa ndipo kazi ya kibinafsi na kazi ya kikundi huchukua nafasi. Inaunda ulimwengu. Kamwe msisahau hili, aliwambia vijana wa Scholas.

Papa aliwazawadia Picha ya Msamaria mwema na kuelezea maana yake
Papa aliwazawadia Picha ya Msamaria mwema na kuelezea maana yake

Papa alihitimishwa mkutano huo kwa kuwapa picha inayoonesha mfano wa Msamaria Mwema, anayependwa sana naye. Hakuna mwenye uhakika kwamba yeye ni Msamaria mwema, lakini lazima tuwe kwa kila mtu, alisisitiza Papa Francisko. Alikumbuka kisa cha mtu huyu pale chini, akiwa amejeruhiwa, na kupuuzwa na wapita njia pia kwa sababu alikuwa anavuja damu na “kulingana na sheria ya wakati ule yeyote aliyegusa damu alibakia kuwa najisi”. Kwa hiyo aliuliza swali “Ni mara ngapi usafi wa kiibada hupendelewa kuliko ukaribu wa kibinadamu,”. Kwa hiyo aliwaachia swali “Je  ni nini kinakufanya uhisi huruma? Au moyo wako ni mkavu kiasi kwamba huwezi kuhisi huruma? Nini kinatokea?” Papa aliwauliza vijana. Kwa kuongezea “Wakati mwingine katika maisha inabidi uchafue mikono yako ili usiuchafue moyo wako”.

Kabla ya kuondoka Papa alibariki mzeituni
Kabla ya kuondoka Papa alibariki mzeituni

Watu wakiwa wanampigia makofu, Papa Francisko aliondoka katika nyumba ya Cascais, akimhakikishia baraka zake kwamba anawapatia lakini wamwahidi pia kumwombea. “Niombee Bwana anibariki. Na yeyote asiyeomba, anitumie mawimbi chanya. Wakati wa kutoka bado kilio cha salamu, picha kutoka kwa madirisha ya wenyeji wa majengo karibu na makao makuu ya Scholas, saini kwenye mpira wa mikono. Kwa nyuma, fado ya kugusa kipengele cha tabia ya utamaduni wa Lisbon iliyoimbwa na mwanamke katikati ya uwanja. Hatimaye, Papa alibariki mti wa mzeituni, ambayo ni  ishara ya amani.

Papa na Scholas
03 August 2023, 12:16