Kuanzia tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba ni kipindi cha kuombea kazi ya uumbaji na utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Kuanzia tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba ni kipindi cha kuombea kazi ya uumbaji na utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. 

Papa Francisko:tarehe 4 Oktoba itachapishwa sehemu ya II ya Laudato si'

Katika katekesi yake,Papa alikumbuka Siku ya Kuombea kazi ya Utunzaji wa Uumbaji duniani ambayo inaadhimishwa tarehe 1 Septemba.“Ni muhimu kusimama pamoja na waathiriwa wa ukosefu wa haki wa mazingira na hali ya tabianchi, kujitahidi kumaliza vita visivyo na maana juu ya nyumba yetu ya pamoja ambayo ni vita vya kutisha vya ulimwengu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Wito wa Baba Mtakatifu Francisko umetolewa katika Ukumbi wa Paulo VI, mjini Vatican, Jumatano  tarehe 30 Agosti 2023  wakati tunaelekea katika Siku ya Kuombea kazi ya Uumbaji Duniani itakayofanyika tarehe 1 Septemba 2023 ambayo mwaka huu kwa inaongozwa na mada ya “Haki na amani vimiminike.” Papa Francisko kwa hiyo mara baada ya tafakari amekumbusha kwamba siku hiyo inazindua msimu wa kipindi cha kazi ya Uumbaji utakaodumu hadi tarehe 4 Oktoba 2023,  sambamba na sikukuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi. Na kama alivyokuwaamesema tarehe 21 Agosti 2023 alipokutana na ujumbe wa wanasheria kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ulaya, alirudia kusema kwamba "sehemu ya pili ya waraka wa Laudato Si ingechapishwa hivi karibuni, hasa tarehe 4 Oktoba."

Kusimama pamoja na wahasiriwa wa dhuluma ya mazingira

Kwa mujibu wa Papa amesema: “Katika tarehe hiyo ninakusudia kuchapisha Waraka, wa Pili wa Laudato si' Kwa hiyo tujiunge na kaka  na dada zetu Wakristo katika ahadi ya kulinda kazi ya Uumbaji kuwa zawadi takatifu kutoka kwa Muumba. Hivyo Papa Francisko ambaye ametoa muhtasari wa kiini cha Ujumbe ambao tayari ulitolewa mwezi wa Mei kwamba “Ni muhimu kuchukua upande wa waathirika wa ukosefu wa haki wa mazingira na hali ya tabianchi, tukijitahidi kukomesha vita visivyo na maana dhidi ya nyumba yetu ya pamoja, ambayo ni ulimwengu wa kutisha, katika vita. “Ninawasihi nyote mfanye kazi na kuomba kwamba iweze kujaa maisha tena.”

Badilisha sera za umma

Katika Ujumbe huo, Papa anapendekeza kubadilisha mioyo yetu, mitindo yetu ya maisha na sera za umma zinazoongoza jamii zetu. Alizungumza tena juu ya uongofu wa kiikolojia na haja ya kutozingatia tena uumbaji kama kitu cha kunyonywa, lakini ukweli unaopaswa kuhifadhiwa kama zawadi takatifu kutoka kwa Muumba. Pia katika andiko hilo, Baba Mtakatifu anasisitiza juu ya haja ya kubadilisha sera za umma zinazotawala jamii zetu na kuunda maisha ya vijana wa leo na wa kesho, anasisitiza umuhimu wa sinodi na anatumai kwamba katika Kipindi hiki cha Uumbaji, kama wafuasi wa Kristo katika safari yetu ya pamoja ya sinodi, tunaishi, tunafanya kazi na kusali kwamba nyumba yetu ya pamoja ijae tena uzima.

Baada ya katekesi Papa ametoa wito wa kuombea kazi ya uumbaji 1-9 Septemba hadi 4 Oktoba
30 August 2023, 15:05