Papa Francisko:Imani sio lebo za kidini ni uhusiano binafsi na Bwana

Makananayo ana Imani ambayo siyo lebo ya kidini,lakini ni uhusiano binafsi wa mtu na Bwana.Ni mara ngapi tunaangukia katika jaribu la kuchanganya imani na lebo?Imani ya mama huyo haijatengenezwa na kanuni za kitaalimungu,lakini kwa msisitizo;anabisha mlangoni,sio kwa maneno,lakini kwa sala.Na Mungu hana kikwazo iwapo anaombwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya 20 ya Mwaka A tarehe 20 Agosti, Baba Mtakatifu akiwa katika dhirisha la Nyumba ya kitume ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliikusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mkini Vatican. Akianza Papa amesema “  Injili ya leo inasimulia mkutano wa Yesu na mwanamke mkananayo nje ya eneo la Israeli (Mt 15,21-28). Yeye aliomba Bwana ili mtoto wake apone kwa kuwa alikuwa amepagawa sana na pepo, lakini Bwana hakumsikiliza. Yeye alisisitiza na wanafunzi wake wakamshauri ili amsikilize na aweze kunyamaza, lakini Yesu alieleza kuwa utume wake ulikuwa ni kwa ajili ya wana wa Israeli na anatumia sura hii kuwa: “Si vema kukitwaa chakula cha watoto kuwatupia mbwa.” Na mwanamke jasiri akajibu: “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa hula chakula kiangukacho mezani kwa mabwana zao. Kwa hiyo Yesu akasema, Mama imani yako ni kubwa, na iwe kwako utakavyo. Na wakati huo huo mwanae akapona”(15,26-28). Hii ni histroia nzuri na hiyo ilitokea kwa Yesu.

Waamini wakisililiza tafakari ya Papa 20 Agosti 2023
Waamini wakisililiza tafakari ya Papa 20 Agosti 2023

Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo ameanza kudadavua Yesu alivyoanza kubadili mwelekeo  wake na kilichomfanya kubadilika ni nguvu ya imani ya mama yule. Kwa kifupi Baba Mtakatifu ametaka kujikita na mantiki hizo  mbili juu ya mabadiliso ya Yesu na imani ya yule mama. Kwa upande wake akianza na mabadiliko ya Yesu amsema “Yeye alikuwa anaelekeza mahubiri yake kwa watu wateule; baadaye Roho Mtakatifu aliweza kusukuma Kanisa hadi miisho ya dunia. Lakini hapa inakuja tusema, utangulizi kwa hiyo katika tukio hili, ambalo mama mkananayo tayari anajionesha  katika ulimwengu wa kazi ya Mungu. Ni jambo la  kuvutia la uwezekano huu wa Yesu, kwani mbele ya sala ya mama yule, inatanguliza mipango, mbele ya kesi yake ya kweli, inageuka kuwa zaidi ya kukubaliwa na huruma.

Baba Mtakatifu ameongeza kusema: “ Mungu ndio hivyo. Ni upendo na anayependa habaki mgumu. Ndiyo anabaki na msimamo. Lakini sio mgumu, katika msimamo wake binafsi, lakini anajiachia kuguswa na hisia; anabadili ratiba zake. Na upendo ni ubunifu na sisi wakristo, ikiwa tunataka kumuiga Kristo, tunaalikwa kuwa na uwezekano wa kubadilika. Jinsi gani ilivyo nzuri katika mahusiano yetu, lakini hata katika maisha ya imani, kuwa wanyoofu, kuwa na umakini wa kweli wa kusikiliza, ambao unalainisha kwa niaba ya huruma na wema wa wengine kama alivyofanya Yesu kwa mkananayo. Unyenyekevu wa kubadilika. Mioyo mitulivu kwa ajili ya mabadiliko. Kwa upande wa mantiki ya pili Baba Mtakatifu amesema, “Tutatazame katika imani ya mama huyo ambaye Bwana anamsifu akisema: “ni imani kubwa(Mt 15,28). Wanafunzi utafikiri msisitizo wake ndio mkubwa tu, lakini Yesu anamsifu akisema kuwa ni mkubwa, Yesu anatazama imani; Wanafunzi wanaona msisitizo tu. Ikiwa tunafikiria, yule mwanamke mgeni, inawezekana alikuwa labda anamjua kidogo au bila kujua, sheria na amri za kidini za Israeli.

Waamini kutoka pande za dunia bila kuogopa jua kali wamesali sala na Papa
Waamini kutoka pande za dunia bila kuogopa jua kali wamesali sala na Papa

Je imani yake inatokana na nini?  Mwanamke sio tajiri wa mantiki, lakini ni tajiri wa matendo: Mkananayo alimkaribia, aliinama na kusisitiza, alikaa katika mazungumzo pamoja na Yesu, akashinda kila kizingiti, licha ya kuzungumza naye tu. Alishinda vizingiti vyote kwa ajili ya kuzungumza naye. Papa  akiendelea amesisitiza kuwa tazama uthibitisho wa Imani ambayo siyo lebo ya kidini, lakini ni uhusinao binafsi wa mtu na Bwana. Ni mara ngapi tunaangukia katika jaribu la kuchanganya imani na lebo? Ameuliza Papa. “Imani ya mama huyo haijatengenezwa na kanuni za kitaalimungu, lakini kwa msisitizo; anabisha mlangoni, anabisha, anabisha”:  sio kwa maneno, lakini kwa sala. Na Mungu hana kikwazo iwapo anaombwa. Kwa sababu alisema “Ombeni na mtapewa, tafuteni na mtapata, bisheni na mtafunguliwa(Mt 7,7).

Ziadi ya watu 10,000 walikuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro 20 Agosti 2023
Ziadi ya watu 10,000 walikuwapo katika uwanja wa Mtakatifu Petro 20 Agosti 2023

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa katika nuru ya yote hayo tunaweza kujiuliza maswali. Kuanza na mabadiliko ya Yesu: Je mimi ninaweza kubadili maoni yangu? Je ninajua kuelewa na kuwa na huruma au nibaki na ugumu wa msimamo wangu?Katika moyo wangu kuna kitu chenye ugumu? Ambacho hakina uimara, kwa sababu ugumu ni mbaya na uimara ni mzuri. Na kuanzia na imani ya mwanamke yule, imani yangu ikoje? Je, inaishia kwenye dhana na maneno, au inaishi kweli kwa maombi na matendo? Je, ninajua jinsi ya kuzungumza na Bwana, je, ninajua jinsi ya kusisitiza Naye, au ninaridhika kukariri fomula nzuri? Mama Yetu atujalie kupatikana kwa kutenda wema na thabiti katika imani. Papa Francisko amehitimisha Tafakari yake.

Tafakari ya Angelus 20 Agosti 2023
20 August 2023, 13:38