Tafuta

2023.08.04 Baba Mtakatifu amekula chakula cha mchana na vijana wanaowakilisha nchi mbali mbali duniani katika Ubalozi wa Vatican, jijini Lisbon. 2023.08.04 Baba Mtakatifu amekula chakula cha mchana na vijana wanaowakilisha nchi mbali mbali duniani katika Ubalozi wa Vatican, jijini Lisbon.  (Vatican Media)

Papa kwa mlo wa mchana na vijana na mazungumzo kuhusu changamoto za dunia na mwaliko wa furaha

Wavulana na wasichana kumi wa rika tofauti na kutoka sehemu mbalimbali za dunia,wakiwa wamekaa mezani pamoja na Papa Francisko katika Ubalozi wa Kitume,alijibu maswali na maombi yao juu ya mada kama vile amani,ulinzi wa maisha,changamoto za vizazi vipya.Na alihimiza kila mtu kamwe asipoteze furaha.Zawadi pia zilitolewa kwa Papa.

Vatican News

Katika Ubalozi wa Vatican jijini Lisbon kama sehemu ya mpango wa maadhimisho ya Siku ya vijana duniani (WYD), tarehe 4 Agosti 2023,  Sebastião, Clara Ysabel, Joana, Luis Carlos, Beatriz, Pedro, Audrey, Hannah, Karam, Maria Magdalena ni vijana kumi wakiwa  wasichana sita na wavulana wanne  ambao walipata chakula cha mchana na Baba Mtakatifu. Hawa ni vijana wenye umri tofauti (kuanzia 34 hadi 24) na wa mataifa tofauti: watatu kutoka Ureno, mmoja kutoka Peru, mmoja kutoka Ufilipino, msichana kutoka Guinea ya Ikweta; na tena Marekani, Palestina, Colombia, na Brazil. Wamechaguliwa ili kupyaisha ule utamaduni ambao umekuwa ukirudiwa kwa miaka katika kila Siku ya Vijana Ulimwenguni. Kadinali Manuel José Macário do Nascimento Clemente, Patriki wa Lisbon, na askofu msaidizi Amèrico Aguiar, ambaye ni rais Mfuko wa WYD Lisbon 2023, na  kardinali mteule  kati ya makardinali wajao pia walikuwepo kwenye chakula cha mchana pamoja na vijana.  Kwenye orodha ya chakula cha mchana kulikuwa na Pasta, nyama na ice cream.

Muonekana wa meza na washiriki wa chakula cha Mchana na Papa Francisko katika Ubalozi wa Vatican huko Lisbon.
Muonekana wa meza na washiriki wa chakula cha Mchana na Papa Francisko katika Ubalozi wa Vatican huko Lisbon.

Mazungumzo kwenye meza

Baba Mtakatifu akiwa na wavulana na wasichana, alianzisha mazungumzo. Hakuuliza maswali, lakini alisikiliza historia zao, akijibu maombi yao, na huku akifafanua mashaka ya hoja ya mawazo yao. Na pia kuwatia moyo daima kuwa na furaha, kama watakatifu ambao hawana huzuni kamwe. Kulikuwa na mada mbalimbali ambazo Papa Fransisko na wageni waalikwa vijana walijadili kama vile amani, ulinzi wa maisha kwa kurejea pia maswala ya utoaji mimba na euthanasia, changamoto zinazowasubiri vijana na  matarajio yao. Vijana wanane kati ya hao hao walisimulia kwa furaha sana, katika chumba cha waandishi wa habari kilichowekwa Lisbon kwa  ajili ya Siku ya Vijana duniani (WYD) 2023.

Maswali kwa Papa

Kwa upande wa kijana Audrey alisema: “Tuliwasilisha zawadi zetu na wakati wa chakula cha mchana tulipata fursa ya kumuuliza maswali machache. Nilimuuliza jinsi ya kuwa rafiki mzuri, hasa na vijana, wakati ambapo kuna mapendekezo mengi ya uongo kuhusu jinsi ya kuwa na furaha. Niliguswa sana na majibu. Alisema kwamba furaha haifundishwi, bali inaoneshwa, na ndiyo nitaondoka nayo kwenye mkutano huu. Pia alizungumza kuhusu furaha ya Injili na umuhimu wa kutenda kwa njia ambayo inatia shangwe. Vijana wenzangu pia wameuliza maswali, lakini sio yangu kushirikisha.”

Matumaini

“Nilimwambia kwamba kwa sisi vijana, matumaini ni muhimu sana - alielezea  kijana Luis Carlos, ambaye alifanya kazi kwenye upande wa picha za siku ya WYD, kwamba tunaweza kupata matumaini ya kupambana na mambo yote mabaya katika maisha, hasa yale yanayoathiri vijana  kama madawa ya kulevya. Matumaini hukuruhusu kupambana na kwa hivyo kuwa na furaha. Kutokana na  kazi yote ambayo nimefanya kutayarisha WYD na michoro, hili limekuwa hitimisho zuri kwa kazi yangu yote ya nyuma ya pazia. Nilipomwona Papa nilihisi amani ya ndani. Nilifikiri nitalia, lakini ilinituliza tu. Nilikuwa wa kwanza kumsalimia. Pia tulikuwa na kahawa za Colombia mwishoni mwa chakula cha mchana. Mungu hujidhihirisha kwa njia za ajabu.”

Kundi la vijana waliopata mlo wa mchana na Papa Francisko katika ubalozi wa Vatican, Lisbon.
Kundi la vijana waliopata mlo wa mchana na Papa Francisko katika ubalozi wa Vatican, Lisbon.

Kila mmoja wa vijana alitoa zawadi kwa Papa Francisko. Kutoka kwa Pedro Luis pia barua, ambayo anaandika: “Ninataka kutoa maisha yangu kwa Kanisa.”

 

04 August 2023, 17:44