Papa,masifu ya jioni:Yesu anakuja kututafuta katika majanga yetu ili kutusaidia kuanza upya

Kanisa la kisinodi,katika mazungumzo na wote,juu ya utume katika wakati huu wa neema.Ndivyo Papa Fransisko nchini Ureno amewakumbusha maaskofu,mapadre,mashemasi,watu waliowekwa wakfu,waseminari na wahudumu wa kichungaji na kuwasihi wasikubali ukasisi,hadi kukatisha tamaa ya kushindwa,kuanzia kuwakaribisha ambao wamekumbwa na kashfa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo maaskofu, mapadre, mashemasi, watawa wa kike na kiume, waseminari na wachungaji wa Lisbon wakati wa Masifu ya jioni pamoja na waamini wapatao 1,100 katika Monasteri ya Kifalme ya Mtakatifu  Maria wa Belèm, inayojulikana kama ‘Mosteiro dos Jeronimos’, tarehe 2 Agosti 2023 jioni ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara yake ya Kitume 42 nchini Ureno, Katika fursa ya Siku ya XXXVII ya Vijana Ulimwenguni. "Safari ya kikanisa haiepukiki kutokana na uchovu na kukatishwa tamaa na mara nyingi tunakuwa katika hatari ya kunaswa na mitandao ya kujiuzulu, kukata tamaa au majuto. Tunahitaji kumka na kuacha kutotulia kwa ajili ya Injili". Baba Mtakatifu katika tafakari yake amesema na kwamba "Kanisa sio mpakani ambao unawatenganisha wenye haki na wenye dhambi kwa sababu linawakumbatia kila mtu na halimnyooshei kidole yeyote. Kwa njia hiyo Papa Francisko alionya dhidi ya hatari za kugeuza imani na kuwa maafisa wa huduma.  "Uchovu wa Petro na wanafunzi wa kwanza ambao walikwenda kuvua samaki usiku na kurudi mikono mitupu ni hisia ambayo pia inaunganisha na kijikita ndani ya Kanisa leo hii. Na ni hisia iliyoenea sana katika nchi zenye mapokeo ya kale ya Kikristo, yaliyopitiwa na mabadiliko mengi ya kijamii na kiutamaduni na yanazidi kuashiriwa na usekula, kutomjali Mungu na kuongezeka kwa kizuizi kutokana na mazoezi ya imani. Na hii mara nyingi inasisitizwa na tamaa na hasira ambayo wengine wanayo kuelekeza Kanisa, wakati mwingine kutokana na ushuhuda wetu mbaya na kashfa ambazo zimeharibu uso wake, na ambazo zinatuita kwenye utakaso wa unyenyekevu na wa mara kwa mara, kuanzia na kilio cha maumivu cha waathirika, kukaribishwa na kusikilizwa kila mara."

Wakati wa masifu ya jioni
Wakati wa masifu ya jioni

Mtazamo wa kushindwa husababisha jaribu la kutaka kushuka kwenye mtumbwi, amesema Papa. Badala yake "ni lazima tulete juhudi zetu na  machozi kwa Bwana, ili kisha kukabiliana na hali ya kichungaji na ya kiroho kwa kukabiliana na kila mmoja kwa moyo ulio wazi na kujaribu pamoja na njia mpya kusonga mbele, tukiamini kwamba Yesu anaendelea kumwinua Bibi arusi wake mpendwa kwa mkono na kumwinua tena. Kama ilivyokuwa kwa wanafunzi, kiukweli, Yesu anakuja kututafuta katika upweke wetu na shida ili kutusaidia kuanza upya". Anapanda kwenye mashua ili kubadilisha maisha yao, anawaalika watoke kwenye kilindi, wakati huo wavuvi ni ambao walishuka kwenda kuosha nyavu tupu, hawakuwa na chaguo ila kwenda nyumbani mikono mitupu. Baba Mtakatifu amewaeleza kuwa, kile ambacho tunachoishi kwa hakika ni wakati mgumu, lakini Bwana leo  hii anauliza Kanisa hili kwamba: “Je! Unataka kushuka kutoka kwenye mtumbwi na kuangukia kwenye kukata tamaa au kupanda na kwa mara nyingine tena habari mpya ya Neno langu na kuchukua usukani mkononi? Je! unataka tu kuhifadhi yale ya wakati uliopita uliyo nayo nyuma ya mabega yako au kuwa na shauku kurusha nyavu zako za uvuvi?”

Masifu ya Jioni katika Monasteri ya Jeronimos
Masifu ya Jioni katika Monasteri ya Jeronimos

Papa ameongeza kusema “Tumeitwa kushusha nyavu tena na kukumbatia ulimwengu kwa tumaini la Injili. Ni hali nzuri ya kutotulia kwa Yesu kwamba ukubwa wa bahari leo hii unasukuma kwa Wareno. Kusukuma, ng’ambo ya ufuko si kwa kuushinda ulimwengu, bali kuufurahisha kwa faraja na furaha ya Habari Njema. Kwa hiyo sio wakati wa kukata tamaa, wa kuweka mtumbwi ufukweni au kutazama nyuma au kukimbia wakati huu kwa sababu ya kutiwa hofu na kukimbilia katika mifumo na mitindo ya zamani, hapana badala yake  huu ndio wakati ambao Bwana anatupatia kujitosa ndani ya bahari ya uinjilishaji na utume, yaani kupeleka kilindini na kupita, kwa sababu kamwe bila kuchoka, na  kamwe bila kusali kwa kuabudu mbele za Bwana ili kuweza kuondokana na kushindwa kwa imani. 

Masifu ya Jioni
Masifu ya Jioni

Tunahitaji kuondoka kwenye benki ya kukatishwa tamaa na kutoweza kusonga mbele, tujitenge na huzuni hiyo tamu na wasiwasi wa kejeli ambao hutushambulia katika uso wa shida. Papa ameonya kwamba wasichukulie kimbilio katika siku za zilizopita. Hapana  kuwa  na huduma ya kichungaji ya kujutia kwani kuna hamu moja tu kwamba Injili imfikie kila mtu. Baba Mtakatifu anamemnukuu kijana Mtakatifu João de Brito, ambaye aliondoka kwenda India karne nyingi zilizopita, ambaye ili kumtangaza Yesu alizungumza na kuvaa sawa na wale aliokutana nao. Kwa hiyo “ Sisi pia tumeitwa kuzamisha nyavu zetu katika wakati tunaoishi, mazungumzo na kila mtu, ili kuifanya Injili ieleweke, hata kama kwa kufanya hivyo tunaweza kuhatarisha dhoruba fulani.

Watawa na waamini pamoja katika masifu ya jioni na Papa
Watawa na waamini pamoja katika masifu ya jioni na Papa

Baba Mtakatifu ameeleza kuwa kamwe wasisahau kwamba utunzaji wa kichungaji lazima ufanyike pamoja na bila mazungumzo, uwajibikaji na ushiriki, mbamo hayawezi kwenda mbele na kwa hiyo Papa ameonya, dhidi ya madai ya kujitosheleza na kumwalika kila mtu juu ya umuhimu wa uhusiano na sinodi katika zama za Kanisa. Baba Mtakatifu  amesema Petro anaongoza mtumbwi, lakini kwenye mtumbwi huo kila mtu anaitwa kushusha nyavu. Kanisa ni la kisinodi, ni ushirika, kusaidiana na msaada wa pande zote na mchakato wa safari ya pamoja. Hili ndilo lengo la Sinodi inayoendelea, ambayo itakuwa na mkutano wake wa kwanza mwezi Oktoba ujao. Katika mtumbwi wa Kanisa lazima kuwe na nafasi kwa kila mtu, yaani wote waliobatizwa wanaoitwa kupanda na kushusha nyavu, wakijitolea kibinafsi kutangaza Injili. Ni changamoto kubwa, hasa katika mazingira ambayo mapadre na watakatifu wamechoka kwa sababu, wakati mahitaji ya kichungaji yanaongezeka, wao ni kidogo na kidogo. Hata hivyo, tunaweza kuitazama hali hii kama fursa ya kuwashirikisha walei kwa ari ya kidugu na ubunifu wa kichungaji wenye afya.

Maskofu wakishiriki masifu ya jioni
Maskofu wakishiriki masifu ya jioni

Kamwe bila kuwa na wengine, lakini kamwe bila ulimwengu. Bila utaifa, lakini si bila ulimwengu katika hali ya udugu wenye kujenga amesisitiza  Papa ambaye anawaambia Wareno: “wao ni mawe ya thamani ya sakafu ile ya kukaribisha na kung’aa ambayo Injili inahitaji kutembea hata jiwe haliwezi kukosekana, vinginevyo linaonekana mara moja”.  Mwaliko uliotolewa na Yesu kwa wanafunzi wake miaka elfu mbili iliyopita ni wa wakati ufaao kama hapo awali. Kuwa wavuvi wa watu maana yake ni wavuvi wa watu na kuwatoa baharini, mara nyingi huhusishwa katika Maandiko na mahali pa uovu. Wasaidie warudi walikoanguka, muwafufue kutoka katika aina zote za kifo. Agizo ambalo Baba Mtakatifu amewaachia  Kanisa la Ureno katika siku ya kwanza ya safari yake ya 42 ya kitume kimataifa ni ile ya kupelea ukaribu wa kukubalika kwa Injili katika jamii yenye tamaduni nyingi, ukaribu wa Baba katika hali ya hatari na umaskini unaozidi kukua, hasa miongoni mwa vijana; upendo wa Kristo ambapo familia ni tete na mahusiano yanajeruhiwa; furaha ya Roho ambapo kukata tamaa na kushindwa kunatawala”.

Masifu ya jioni
Masifu ya jioni

Baba Mtakatifu amesema kuwa kuna giza kubwa sana katika jamii ya leo, hata hapa Ureno. Tuna hisia kwamba shauku, ujasiri wa ndoto, nguvu ya kukabiliana na changamoto, imani katika siku zijazo imekosa; na wakati huo huo, tunasafiri katika hali ya kutokuwa na uhakika, katika hatari ya kiuchumi, katika umaskini wa urafiki wa kijamii, katika ukosefu wa tumaini. Sisi, kama Kanisa, tumekabidhiwa jukumu la kuzama ndani ya maji ya bahari hii kwa kuushusha wavu wa Injili, bila kunyooshea vidole, badala yake kuwaletea watu wa nyakati zetu pendekezo la maisha mapya, yaani, maisha mapya katika Yesu, Papa alihitimisha.

02 August 2023, 21:15