Papa amesema yuko anashughulikia sasisho la Waraka wa Laudato Si wakati akizungumza na wanasheria kutoka Baraza la Ulaya 21 Agosti 2023. Papa amesema yuko anashughulikia sasisho la Waraka wa Laudato Si wakati akizungumza na wanasheria kutoka Baraza la Ulaya 21 Agosti 2023. 

Papa:“Niko naandika sehemu ya pili ya Laudato si’”

Akizungumza na wajumbe wa Wanasheria kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ulaya,Papa Francisko alisema anafanyia kazi sasisho la Waraka uliochapishwa mnamo 2015.Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican alisema kwamba huo ni Waraka unaozungumzia hasa mgogoro wa hali ya Tabianchi ya hivi karibuni.

Vatican News

“Niko ninaandika sehemu ya pili ya Laudato si',  ili  kusasisha matatizo ya sasa”. Haya ndiyo aliyoyasema Papa Francisko tarehe 21 Agosti 2023 alipokuwa akihutubia wajumbe wa mawakili kutoka nchi wanachama wa Baraza la Ulaya waliotia saini juu ya Wito wa Vienna, huku matukio makali yakiendelea kufuatana duniani,na kuathiri idadi ya watu katika mabara yote. Msemaji wa Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, Dk. Matteo Bruni, alibainisha kuwa ni Waraka ambao unajikita kushughulikia hasa majanga ya tabianchi ya hivi karibuni. Papa Francisko, wakati wa Mkutano na hao wajumbe wanasheria alikuwa akitoa shukrani zake kwa ahadi inayolenga kuandaa mfumo wa udhibiti kwa ajili ya ulinzi wa mazingira na kwa hiyo alisema: “Hatupaswi kamwe kusahau kwamba vizazi vijavyo vya vijana  vina haki ya kupokea kutoka kwetu ulimwengu mzuri na wa kuishi,na kwamba hii inatuwekea majukumu mazito kwa kazi ya uumbaji ambayo tumepokea kutoka katika mikono ya ukarimu wa Mungu. Asante kwa mchango huu”.

Laudato si' ni Waraka wa  pili wa Papa Francisko uliochapishwa mnamo  tarehe 18 Juni 2015, na  kutolewa  tarehe 24 Mei  mwaka huo huo, katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Pentekoste. Hati hiyo, iliyojitolea kwa ajili ya “utunzaji wa nyumba yetu ya Pamoja ambo  unachukua jina lake kutoka katika Wimbo wa Sifa ya Viumbe wa Mtakatifu Francis wa Assisi unafunguliwa hivi: “Laudato si', mi' Signore”,  yaani, “Sifa Iwe kwako, Ee Bwana,” aliimba Mtakatifu Francis wa Assisi. Katika wimbo huo mzuri, alitukumbusha kwamba nyumba yetu ya pamoja  pia ni kama dada, ambaye tunaishi naye, na kama mama mzuri anayetukaribisha mikononi mwake: “Laudato si', mi' Signore, per sora nostra matre.  Yaani Sifa iwe kwako Ee Bwana, Mama yetu”. Ardhi, ambayo hudumisha na kuitawala, na hutoa matunda mbalimbali yenye maua ya rangi na nyasi”.

Muda mfupi baada ya kuchapishwa, Waraka huo Papa Francisko mwenyewe alitaka kufafanua maana ya Waraka huo katika katekesi yake ya  tarehe 21 Julai 2015 kwa washiriki wa Warsha iliyokuwa na mada: “Utumwa mamboleo na mabadiliko ya Tabianchi: kujitolea kwa ajili ya miji",  ambapo Papa alisema: Utamaduni huu wa utunzaji wa mazingira sio mtazamo tu, yaani ninamaanisha hii kwa maana halisi ya neno kijani, sio mtazamo wa kijani, ni zaidi yake. Kutunza mazingira kunamaanisha kuwa na mtazamo wa ikolojia ya binadamu. Hatuwezi kusema, kwamba mtu yuko hapa na uumbaji, mazingira yapo. Ikolojia ni jumla, ni binadamu. Na hili ndilo nililotaka kueleza katika Waraka wa Laudato si': kwamba mwanadamu hawezi kutengwa na wengine; kuna uhusiano ambao una athari ya pande zote mbili, ya mazingira kwa mtu na mtu kwa jinsi anavyoshughulikia mazingira; na pia athari ya kurudi nyuma dhidi ya wanadamu wakati mazingira yanatumiwa vibaya. Kwa sababu hiyo, nikikabiliwa na swali waliloniuliza, nilijibu: “Hapana, sio Waraka kijani ni waraka wa kijamii.

Kwa sababu katika jamii, katika maisha ya kijamii ya mwanadamu, hatuwezi kupuuza utunzaji wa mazingira. Zaidi ya hayo, utunzaji wa mazingira ni mtazamo wa kijamii, ambao unatushirikisha, kwa maana moja au nyingine ,  kila mtu anaweza kuipatia thamani anayotaka  na kwa upande mwingine, inatufanya tupate kama ninavyopenda usemi wa Kiitaliano, wanapozungumzia mazingira, ya Uumbaji, ya kile ambacho tumepewa kama zawadi, yaani, mazingira. Kwa maana hiyo katika Waraka  anakumbuka kuwa alichagua jina la Francis kama mwongozo na msukumo kwa papa wake: “Ninaamini kwamba Francis ni mfano bora wa utunzaji kwa kile ambacho ni dhaifu na ikolojia fungamani, aliishi kwa furaha na ukweli. Yeye ndiye mtakatifu mlinzi wa wote wanaosoma na kufanya kazi katika uwanja wa ikolojia, anayependwa pia na wengi ambao si Wakristo.

21 August 2023, 17:48