Tafuta

Mabomu ya Urussi yanaharibu miji ya Ukraine. Mabomu ya Urussi yanaharibu miji ya Ukraine.  (ANSA)

Papa:tuwaombee Waukraine wanaoteseka sana,vita ni ukatili

Mara baada yaa Katekesi,Jumatano tarehe 23 Agosti 2023 katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican,Papa Francisko mawazo yake kwa mara nyingine tena ni kwa ajili ya Ukraine iliyopigwa na kukumbuka vifo vingi vilivyosababishwa na migogoro na watoto waliopotea na anaomba kuiombea nchi hiyo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Mawazo ya Baba Mtakatifu yamegeukia nchini wakati mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku 546. Kw amata nyingine tena  mwishoni mwa katekesi yake  Jumatano, tarehe 23 Agosti 2023 akihitimisha salamu kwa lugha ya  Kiitaliano, Papa Francisko ameikabidhi nchini hyo kwa “maombezi ya Mtakatifu Bartholomayo nchi iliyojaribiwa vikali na vita”;   kwa kuhuzunishwa na maisha mengi ya binadamu yaliyofifishwa na migogoro hiyo, ameomba kila mmoja asali bila kukoma, siku ambayo bendera ya taifa inaadhimishwa, mkesha wa siku ya uhuru uliopatikana mnamo tartehe 24  Agosti 1991.

“Tuwaombee ndugu zetu wa Kiukraine, wanateseka sana, vita ni ukatili, watoto wengi wamepotea, watu wengi waliokufa, tuombe, tafadhali, tusiwasahau Ukraine wanaoteswa, leo ni tarehe muhimu kwa nchi yao.”

Waamini na mahujaji kutoka pande za Dunia amewaomba kuombea Ukraine inayoteseka
Waamini na mahujaji kutoka pande za Dunia amewaomba kuombea Ukraine inayoteseka

Hapo awali, pia katika salamu zake kwa waamini walitoka  Poland, Papa alitaja  nchi ya Ukraine na hasa akikumbuka Sikukuu inayokuja ya Mama Yetu wa Czestochowa, tarehe 26 Agosti, kuadhimisha siku kuu nchini Poland kutokana na ibada kubwa kwake, ambayo huleta kwa pamoja  idadi kubwa ya watu kwenye madhabahu yake, Papa aliomba kwamba ibada hii izidi kuwasha upendo wa watu wa Poland kwa ajili ya jirani zao Ukrainiane, wanaoteseka kutokana na vita" na kuwabariki kutoka moyoni mwake.

Papa aombea nchi ya Ukraine
23 August 2023, 14:14