Tafuta

2023.08.30 Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican afafanua kuhusu ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Mongolia 31 Agosti hadi Septemba 4. 2023.08.30 Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican afafanua kuhusu ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Mongolia 31 Agosti hadi Septemba 4. 

Parolin:Francisko,Mongolia,mwanahija wa matumaini kwa Ulimwengu wote

Safari kwa ajili ya kuimairisha imani “Jumuiya ndogo katoliki na hai” ya Mongolia na kwa ajili ya kuongeza nguvu hata mafungamano kati ya Vatican na Nchi hiyo ndogo ya Asia.Ndivyo Katibu wa Vatican,Kardinali Parolin amesema kuhusiana na ziara ya Kitume ya Ulaanbaatar.Amani,mikutano na mazungumzo ni ncha tatu za ziara hiyo.

Na Massimiliano Menichetti.

Mongolia iko tayari kumkumbatia kwa mara ya kwanza katika historia Papa ambaye ana shauku kubwa. Ndivyo Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican anabainisha akihojiwa na vyombo vya habari Vatican, huku akizungumzia juu ya shauku ambayo Jumuiya ndogo katoliki ya Nchi hiyo ya Asia iko inajiandaa kumpokea Baba Mtakatifu. Katika ziara yake ya 43 ya kitume, Papa Francisko kuanzia tarehe 31 Agosti hadi tarehe 4 Septemba atakuwa huko Ulaanbaatar, mji Mkuu wa Mongolia, Nchi kubwa sana ya mara tano ya Italia na ina watu karibia milioni 3,300,000, Nchi ambayo inapakana na Urusii na China.  Kwa hiyo ili kueleza ziara yake inapatikana katika Kauli mbiu isemayo: “Kutumaini pamoja”, kwa sababu, Kardinali Parolin ameeleza kuwa “kuna haja  sana ya matumaini, matumaini ambayo siyo mategemeo ya utupu, lakini ambayo yana msingi angalau kwa sisi wakristo, juu ya imani kuhusu uwepo wa Mungu katika historia yetu na wakati huo huo iweze kubadilika katika jitihada binafsi na kwa ujumla.”

Mwashamu, ni matarajio yapi ya Baba Mtakatifu?

Ziara hii katika moyo wa Asia inajibu mwaliko kwa Mamlaka ya Nchi na ya Jumuiya Katoliki. Matarajio ni kwa uhakika makubwa,  iwe kwa upande wa Baba Mtakatifu na hata kwa upande wa Mongolia,  ambao kwa mara yao ya  kwanza wanamuona mfuasi wa Mtume Petro katika ardhi yao.  Shauku ya Papa ni kukutana na Jumuiya hii, jumuiya moja ambayo ni dogo kwa idadi, lakini kijana, iliyo hai na ya kushangaza kwa ajili ya historia yake muhimu na muundo wake. Zaidi ya hayo, itakuwa na maana katika ukuu wa kidini, katika Nchi ambayo itapyaisha tamaduni yake kubwa ya kibudha.

Papa ataimarisha imani karibu watu 1500 wakatoliki  waliopo nchini Mungolia. Ni umuhimu gani wa uwepo wa Francisko kwa jumuiya hii ndogo ya kimisionari?

Nam, shauku ni dhairi na ambapo wakatoliki wako wanajiandaa kumpokea Baba Mtakatifu. Uwepo wake ni matarajio iwe kama udhibitisho na kutiwa moyo katika mchakato wa safari ya maisha ya kikristo na safari ya imani, matumaini na mapendo; lakini pia kama uthibitisho wa kutimiza kipindi cha kushangaza ya utamadunisho wa kimisionari. Kwa hakika, ikiwa tunafikiria suala la Kanisa hili hatuweza kutoshangaa na ninaweza kusema hata kuwa na hisia, hasa ya karne ya kukosa, hadi  mwanzoni mwa miaka ya 90 na kuendelea amani ya mpito wa kidemokrasia wa Nchi, kwa hiyo walianza kiukweli na sufuri. Wamisionari wa kwanza walifika kama waanzilishi, walijifunza lugha, walianza kuadhimisha katika nyumba, walihisi kuwa njia na mbinu, lazima iwe ile ya upendo na kukumbatia watu mahalia kama vile ni watu wao.  Kwa kufanya hivyo baada ya siku, na  miongo michache, kuna jumuiya ya Kikatoliki kwa maana halisi ya neno hili, yaani jumuiya ya ‘ulimwengu,’ iliyoundwa na wajumbe mahalia, lakini hata wajumbe wanaotoka katika nchi tofauti ambao kwa unyenyekevu, upole na maana ya kushirikishana  shauku ya kuwa mbegu ndogo ya udugu.

Umakini utakuwa hata kwa ajili ya mkutano wa kiekumeni na kidini utakaofanyika Dominika tarehe 3 Septemba

Ndiyo. Kama Baba Mtakatifu alivyokumbusha mara nyingi, safari ya kidini, safari ya mazungumzo ya kidini sio uchaguzi wa fursa au unaowezekana, lakini ni njia ambazo tangu Mtaguso na kuendelea, Kanisa Katoliki linapitia bila wasiwasi. Na kutokana na mtazamo huo, Mkutano na wajumbe wa madhehebu mengine ya kidini daima umekuwa na lengo la ujenzi wa amani na wa udugu na tunajua jinsi gani kuna haja leo hii hasa katika jitihada  za ujenzi wa amani na udugu! Na kwa hakika, baadaye ziara hii inajikita hata katika wakati muhimu wa kukutana na Wabudha, ambao nchini Mongolia ndiyo walio wengi na wana historia moja yenye maana kubwa, yenye tabia ya hekima inayotafuta ukweli, lakini pia sifa ya mateso makubwa, mateso katika siku za nyuma

Katika miaka hii ya mwisho karibu na mtindo wa  maisha ya kiutamaduni, kuna ukuaji wa miji. Katika muktadha huo wa kukua kijamii, ni nafasi gani ya kijamii inaweza kuwa nayo katika ziara ya Baba Mtakatifu?

Papa Francisko anasisitiza mara nyingi umuhimu wa kutafuta maelewanao. Katika maelezo hata, kwa neno hili lina maana ya kushauri ukuaji wa ulimwengu mzima yaani kukua kibinadamu, kijamii na kiroho ambayo inazingatia kutoruhusu umbali na hatari kwa kujuua kwamba kinyume chake ufungamanishwaji wa tofauti na mabadiliko kama muktadha wa kukua, kiasi ili mkutano wa wapinzani na tofauti ushinde mgongano na upinzani. Jamii ya Mongolia inapitia bila shaka kipindi cha kihistoria kinachosisimua, mahali ambapo hekima iliyosimika mizizi kwa watu inaitwa kufungamanisha tamaduni na siasa bila  kupoteza mizizi  na kuhamasisha maendeleo kwa wote. Papa ambaye yuko katika ishara ya urafiki na kwa heshima kubwa anayofuraha ya kukutana na watu wa Mongolia, atajionesha kwa hakika umakini hata kwa mantiki hizi.

Kardinali Parolin,Katibu wa Vatican,aelezea ziara ya Kitume ya Papa Francisko nchini Mongolia

Mazungumzo kati ya Vatican na Mongolia yalianzia karibu miaka 800 iliyopita, katika nyakati za Papa  Inocent IV. Ni mahusiano gani leo hii yaliyopo?

Kuhusiana na mwendelezo wa kihistoria ambao umemaliza kukumbusha muunganiko wa maslahi ulipelekea kuanzishwa rasmi mahusiano ya kidiplomasia mnamo 1992. Na ushirikiano ambao ulipyaishwa wakati ule hata kwa ngazirasimo tusema,  unaendelea kukua! Hatua kubwa za  mbele zimefanywa katika muktdha wa maslahi ya pamoja kama ilivyobainisha kwa mtazamo wa Ziara maalum ya  Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, mnamo Juni iliyopita. Na yataendelezwa katika njia hii. Ziara ya Kitume inayokaribia kwa hiyo ni fursa hasa kwa ajili ya kuongeza kwa kina mafungamano hayo, ili kuhamasisha  kwa dhati wema wa pamoja, dhima ya  kidini, amani  maendeleo fungamani ya kibinadamu, Elimu, kubadilishana kiutamaduni na hata kukabiliana na changamoto za pamoja ambazo zinatazama kanda na jumuiya ya kimataifa.

Kwa maana hiyo, tunaweza kusubiri kutoka kwa Baba Mtakatifu upyaisho wa wito kwa ajili ya amani, katika nyakati hizi ambazo dunia nzima imechanika na migogoro?

Baba Mtakatifu anaendelea kutoa wito kwa ajili ya amani;  kwa nini? Ni kwa sababu anabeba ndani ya moyo wake uchungu mkali  uliosababishwa na kile ambacho  yeye mwenyewe kwa muda mrefu anakiita “Vita ya tatu ya ulimwengu iliyoganwanyika vipande vipande”. Mbali na miito hiyo iliyoelezwa ya amani ambayo Papa atawaelekea katika muktadha huo, ninadhani kwamba ni uwepo huo wa Papa nchini Mongolia wa kujenga mwaliko wa amani. Nani kwa nafasi muhimu ambayo nchi hii inachukuwa katika muktadha mkubwa wa Asia. Ziara hii kulingana na Nchi, ilivyo ndogo au kubwa ambayo iwe katika mtazamo wa haki za kimataifa, kwa kuachana na kanuni ya nguvu ya kusuluhisha mizozo, kujenga uhusiano wa ushirikiano, mshikamano na udugu kati ya majirani na nchi zote za dunia.

Nchi kubwa inayopakana na Mongolia ni China, taifa ambalo Francisko analitazama kwa hamu kubwa. Je, safari ya kwenda Jamhuri ya Watu wa Uchina inazingatiwa, hata kama si hivi karibuni?

Wote wanajua nia ya Papa Francisko mlango kwa ajili ya China, Na kwa mtazamo  wa swali lako, ninaweza kusema kuwa ndani ya Moyo wa Baba Mtakatifu kuna shauku kubwa,  hiyo shauku ambayo kwa yote hayo inaeleweka ambayo aliionesha tayari mara nyingi kwa umma ya kutaka kwenda katika Nchi tukufu ile, iwe kwa ajili ya kutembea Jumuiya Katoliki na kuitia moyo katika safari yao ya imani na umoja, iwe kwa ajili ya kukutana na Mamlaka ya kisiasa, ambayo Vatican imeanzisha kwa muda mazungumzo,  katika imani kuwa licha ya matazo na vizingiti ambavyo vipo katika safari, kwa hakika katika njia ya mazungumzo na kukutana, zaidi ya ile ya kusigana kiitikadi inawezakana kufikia matunda mema kwa akili ya wema wa wote.

Baba Mtakatifu amerejea hivi karibuni kutoka WYD huko Lisbon ambako, kama alivyosisitiza, matumaini yameonekana kwa vijana. Safari hii ya kwenda Mongolia inatupeleka wapi?

Hapa, kauli mbiu ya safari,  tunaijua ni:  “Kutumaini pamoja” na kwa hiyo kwa mara nyingine tena lafudhi ni juu ya tumaini, ambayo itakuwa pia mada ya Jubilei ya 2025. Kwa nini kusisitiza sana juu ya matumaini? Ni dhahiri, kwa sababu kuna mahitaji mengi katika ulimwengu wetu! Ulimwengu wetu hauna matumaini, unakabiliwa na majanga mengi ya kibinafsi na ya pamoja ambayo hupitia. Tumaini ambalo sio kusubiri utupu, kusubiri mambo yawe bora, karibu kwa njia ya kiini macho; lakini ambayo msingi wake, angalau kwa sisi Wakristo, juu ya imani, yaani, uwepo wa Mungu katika historia yetu, na ambayo wakati huo huo inageuzwa kuwa kujitolea kibinafsi na kwa pamoja, kujitolea kwa ufanisi, kwa ajili ya kuboresha ulimwengu na tunaweza kufanya hivyo pamoja, waamini na walei, wale wote ambao wana hakika ya uwezekano huu. Naam, inaonekana kwangu  ukweli kwamba Papa katika kwenda nchi za mbali kijiografia na pia anakabiliwa na usumbufu unaosababishwa unaashiria nia yake ya kushuhudia kikamilifu na kukuza matumaini leo.

Mwashamu nini matumaini yako, na nini matarajio yako?

Ninashiriki matarajio ya Baba Mtakatifu, yale ambayo nimejaribu kuelezea hivi punde. Zaidi ya hayo, inaonekana kwangu kwamba, ziara za kitume za Papa, Mrithi wa Petro, zina umuhimu na ufanisi mkubwa katika kuvuta hisia za Kanisa zima kwa jumuiya fulani zinazoliunda na ambazo, kama ilivyokuwa kwa Mongolia ni ndogo kwa idadi na kwa hivyo wana hatari kidogo, labda, ya kutojulikana kila wakati vya kutosha, kwanza kabisa, lakini pia kuthaminiwa na kuzingatiwa; na kwa upande mwingine, inaziruhusu jumuiya hizi kutoa mchango wao kwa Kanisa kwa ujumla, zikivuta hisia kwenye kile ambacho ni cha msingi kwa maisha yake na utume wake. Ningesema kwamba zinafanana kidogo na jumuiya za kwanza za Kikristo ambazo ni lazima tuige mfano. Ninaamini kuwa hii itatokea, itatokea pia katika hafla hii. Na kwa hili pia ninahakikishia maombi yangu.

Mahojiano na Katibu wa Vatican Kard.Parolin kuhus ziara ya Papa Mongolia
30 August 2023, 15:46