Tafuta

2023.08.04  Vijana wako tayari katika Njia ya Msalaba na Papa Francisko 2023.08.04 Vijana wako tayari katika Njia ya Msalaba na Papa Francisko  (Vatican Media)

Udhaifu wa ulimwengu utapaza sauti kutoka katika Njia ya Msalaba ya WYD!

Vijana kutoka mataifa 22 watahuisha njia ya msalaba pamoja na Papa Francisko,wakitafakari machungu ya sasa yanayotokea mioyoni mwao,kama vile matatizo ya afya ya akili,vurugu na migogoro ya kibinadamu.

Felipe Herrera-Espaliat; – Lisbon &Angella Rwezaula, - Vatican.

Mapungufu kumi na nne ya jamii ya kisasa yataoneshwa katika kila moja ya Vituo vya Njia ya Msalaba katika Siku ya Vijana Duniani 2023. Ijumaa tarehe 4 Agosti 2023, Papa Francisko na zaidi ya mahujaji 350,000 watasali wakati wa Utamaduni wa Njia ya Msalaba wa Yesu, wakitafakari maumivu yanayowasumbua wanadamu. Haya ni majeraha na miungurumo ambayo inasikika katika mioyo ya vijana kutoka mabara yote ambao wameshiriki katika mashauriano kwa njia ya mtandaoni. Matokeo ya kura ya maoni yalitumika kama msingi wa kuunda simulizi ambayo itatafsiriwa leo hii  na watu 50 kutoka nchi 22, zikiwemo pia  Zimbabwe, Chile na Vietnam.

Vijana wanajitambulisha na Njia ya Msalaba

Mkurugenzi wa kisanii, Matilde Trocado, ameelezea kuwa afya ya akili, kutovumilia, vurugu, migogoro ya kibinadamu, uharibifu wa Uumbaji na upweke zilioneshwa kati ya vipindi vya  mara kwa mara.  Kwa hiyo “Kila mtu anatambuliwa na Njia hii ya Msalaba udhaifu huu, ambayo kiukweli,ni nini kinachowatia wasiwasi. Kwa hiyo, pamoja na Yesu na Msalaba, tutaweza kuombea kila mmoja wao.”Alieleza Trocado.

Bahari ya vijana katika kusubiri kusali njia ya Msalaba
Bahari ya vijana katika kusubiri kusali njia ya Msalaba

Tafakari ziliandikwa  na Mjesuit

Kutokana na mapendekezo hayo kutoka kwa vijana hao, Padre Mjesuit Nuno Tovar de Lemos aliandika tafakari zitakazosomwa katika bustani ya Eduardo VII, Lisbon, huku kila kituo kikipambwa kwa jopo lililoundwa na Mjesuit mwingine, Nuno Branco. Wakati wa  Njia ya Msalaba, Papa Francisko  ambaye kwa mara nyingine tena atawasili ndani ya gari la Kipapa, atasikia kilio cha ulimwengu unaoteseka, atahutubia ujumbe mpya kwa walitakaohudhuria, atasali pamoja nao na kuwapa baraka zake!

04 August 2023, 18:54