Kardinali Zuppi anakwenda Beijing kwa kutumwa na Papa kwa ajili ya amani ya haki
Vatican News
Mara baada ya miezi kadhaa ya kungoja na kutazamia, kwenda Beijing, kwa ajili ya utume wa amani hatimaye uthibitisho umefika kwamba Kadinali Matteo Maria Zuppi, kwa kile ambacho Papa alikiita "chukizo la amani" ili "kupunguza mivutano" katika Ukraine inayoteswa, unaendelea nchini China. Safari yake ni mpango wa kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba 2023. Ni Vatican iliyotangaza juu ya safari mpya ya Kadinali ambayo tayari ilikuwa imemwona akiwa na shughuli nyingi kati ya mwezi Juni na Julai huko Kyiv, nchini Ukraine, Moscow nchini Urussi na Washington nchini Marekani.
Kwa njia hiyo "tarehe 13 - 15 Septemba 2023, Kardinali Matteo Maria Zuppi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Bologna na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Italia (CEI) akifuatana na afisa kutoka Sekretarieti ya Vatican, watasafiri kwenda Beijing, kama mjumbe wa Baba Mtakatifu Francisko". Kwa mujibu wa maandiko ya taarifa ya Vatican, inasomeka kuwa. “Ziara hiyo inajumuisha hatua zaidi katika utume kwa utashi wa Papa wa kuunga mkono mipango ya kibinadamu na kutafuta njia ambazo zinaweza kuleta amani ya haki".
Kwa "Hakika sala za wengi kwa siku hizi, za kidini na za kiekumeni, ni sababu zaidi ya kutafuta zawadi ya amani ambayo ni zawadi kwa kila mtu, kutoka kwa kila mtu na ambayo kila mtu anapaswa kuipata". Hayo yalikuwa ni maoni yake mwenyewe Kardinali Zuppi, mara baada ya kufunguliwa rasmi tukio la taarifa hiyo ya safari mpya, huku akisema kukabiliana na hatua hii kwa matumaini ya kuweza "kufuma mtandao mgumu wa amani."
Kardinali Zuppi alizungumza hayo akiwa Berlin nchini Ujerumani ambako amekuwako tangu tarehe 11 Septemba 2023, katika mkutano uliohamasishwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, ukiongozwa na mada: “Bidii ya amani” uliowaona viongozi wa dini kuu za ulimwengu, pamoja na wawakilishi wa siasa na utamaduni kutoka nchi 40. Miongoni mwao, kulikuwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Bwana Antonio Tajani ambaye Kardinali huyo alikuwa na mazungumzo marefu ya faragha tarehe 11 Septemba 2023 mchana katika Ubalozi wa Italia.