Papa amefika Marsiglia kwa ajili ya Mkutano kuhusu mediteranea
Vatican News
Ninatumaini nitakuwa na ujasiri wa kusema kile ninachotaka kusema. Haya ni matumaini binafsi ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliwashirikisha kwa waandishi wa habari takriban 70 wanaoandamana naye katika ziara yake ya 44 ya kitume hadi Marsiglia, ambapo Papa atashiriki katika Kufunga "Rencontres Méditerranéennes" yaani Mikutano ya kimeteranea, ambalo ni tukio linaoongozwa na mada ya uhamiaji. Akichukua kipaza sauti kwenye ndege kuwageukia waandishi wa habari, Papa Francisko alisema: "Habari za mchana wote na asante kwa kuja, ninawatakia kazi njema. Inaweza kuwa muda mfupi lakini mambo mengi katika jiji hilo ambalo ni mlango, dirisha, kwa hiyo ni kila kitu. ... kwenye Mediterania… Asanteni.”
Kama kawaida ya ziara zake, Papa aliwasalimia waandishi na wapiga picha wote wa magazeti ya kimataifa mmoja baada ya mwingine. Kwa wale waliomkumbusha juu ya hali ya siku za hivi karibuni huko Lampedusa na katika maeneo mengine ya kutua kwa idadi ya wahamiaji damu" wa kutisha. Papa pia alielezea uchungu wake kwa picha iliyooneshwa kwake ya mama mmoja mhamiaji akiwa na mtoto wake, maumivu kwa wengi kama mwanamke huyu aliyezuiliwa katika "kambi" za Libya na kisha kuwekwa kwenye boti baharini, akikabiliwa na hatari nyingi.