Papa ameaga Mongolia:Shukrani kwa ukarimu wao mkuu!
Vatican News.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 4 Septemba 2023, ameondoka nchini Mongolia, kwenye ziara yake ya 43 ya kitume kimataifa ambayo ilimwona akifanya hija hiyo katika mji mkuu Ulaanbaatar nchini humo katika Kanisa dogo la taifa la Asia ya Kati. Ndege ya Shirika la Ndege Ita A330, pamoja na Papa, wasaidizi wake na waandishi wa habari wapatao 70 kutoka mashirika ya vyombo mbalimbali vya habari na magazeti waliondoka saa 6.03 hivi kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chinggis Khan huko Ulaanbaatar. Baada ya takriban saa tisa na nusu ya kuruka ndege itatua kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa Leonardo da Vinci huko Fiumicino Roma karibu saa 11 jioni hivi.
Afla za kuaga
Kama kawaida, sherehe za kuaga zilifanyika katika uwanja wa ndege kabla ya kuruka ambapo Papa Francisko aliwasili kwa gari mwishoni mwa mkutano na Wahudumu wa Upendo katika Casa della Misericordia, yaani Nyumba ya Huruma. Baada ya kuwasili, Papa alikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mongolia, Batmunkh Battsetseg. Mara baada ya salamu za wajumbe na wasaidizi wa eneo husika, mwanamke kijana alimwinamia Papa Francisko kumpa shada la maua. Papa amewahakikishia kwamba atayapeleka kwa Mama Maria. Kisha alisalimiana na Kardinali Giorgio Marengo, Msimamizi wa Kitume wa Ulaanbaatar, aliyekuwa kando yake wakati wote wa ziara hiyo, kwa kupeana mkono kwa nguvu, Papa Francisko alipanda ndege kurejea nchini Italia. Wakati wa safari ya ndege, mkutano wa kiutamaduni na waandishi wa habari utafanyika na waandishi wa habari.
Telegramu kwa rais
Mara baada ya kuondoka, Papa alimtumia rais wa Mongolia, Khürel Sükh Ukhnaa, telegramu ambayo, mwishoni, alionesha kwa mara nyingine tena, hisia ya shukrani kwa mamlaka ya Mongolia na watu kwa mapokezi ya joto na ukarimu aliyopokea siku hizi. Papa Francisko aidha ametoa salamu zake huku akiwahakikishia maombi yake endelevu kwa ajili ya amani, umoja na ustawi wa taifa na akiwaombea kwa moyo mkunjufu baraka nyingi za kimungu juu yao wote.
Safari ya siku nne
Kwajiyo, ndivyo ilivyohitimisha ziara hii ya kwanza ya kitume ya Papa kwenda Mongolia. Ziara iliyoanza rasimi tarehe 1 Septemba 2023 ambayo ilishuhudia Papa Francisko akikutana na mamlaka ya nchi katika mji mkuu Ulaanbaatar na jumuiya ndogo ya Wakristo katika Kanisa Kuu la Watakatifu Petro na Paulo, pamoja na viongozi wa kidini na wahudumu wa vyama vya kutoa msaada na uzinduzi wa Nyumba ya Huruma. Kwa njia hiyo kni katika kukumbatia kimataifa kwa nchi, inayopakana Urussi na China ambayo kama Papa Franciso mwenyewe alisema katika hotuba yake ya kwanza kwa mamlaka ya nchi kuwa inaweza kuchukua jukumu msingi katika eneo la kimataifa, na juu ya yote kwa ajili ya amani ya ulimwengu.