Tafuta

Papa amemtembelea Kardinali Luis Francisco Ladaria na kumshukuru kwa kazi yake yote katika miaka yake akihudumu kama Msimamizi Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Papa amemtembelea Kardinali Luis Francisco Ladaria na kumshukuru kwa kazi yake yote katika miaka yake akihudumu kama Msimamizi Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa.  (AFP or licensors)

Papa amemshukuru Kardinali Ladaria kwa huduma yake

Baba Mtakatifu Francisko Jumanne 5 Septemba 2023,alifanya ziara ya kushtukiza katika Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa na kumshukuru Kardinali Luis Francisco Ladaria kwa kazi yake katika miaka yake ya utumishi kama Mkuu wa Baraza hilo.Hivi karibuni Papa alimteua Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 5 Septemba 2023 amefanya ziara ya kushtukiza katika Baraza la Kipapa Mafundisho Tanzu ya Kanisa  kabla ya masaa 24 baada ya kurejea kutoka katika ziara yake ya Kitume nchini Mongolia. Msemaji wa vyombo vya habari Vatican Dk. Matteo Bruni, alitangaza katika taarifa yake kwamba Baba Mtakatifu Francisko alitembelea Baraza hilo Jumanne  mara baada ya saa 3.00 asubuhi, ambapo alikutana na kumshukuru Kardinali Luis Francisco Ladaria kwa kazi yake yote katika miaka yake akihudumu kama Msimamizi wa Baraza hilo.

Kardinali Ladaria
Kardinali Ladaria

Baada ya kukutana na Kardinali huyo Mjesuit, Baba Mtakatifu Francisko pia alisalimiana na viongozi mbalimbali ndani ya Baraza hilo. Mnamo Julai 2008, Baba Mtakatifu Benedikto XVI, alimteua Ladaria, Mjesuit na Mtaalimungu kutoka Hispania, kuwa Katibu wa Baraza hilo wakati huo na kumfanya kuwa Askofu Mkuu. Na Papa Francisko alimteua kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo wakati wa upapa wake, akimrithi Kardinali Gerhard Ludwig Muller.

Kardinali Ladari wakati wa kuvalishwa kikofia chekundu, 2018
Kardinali Ladari wakati wa kuvalishwa kikofia chekundu, 2018

Kadinali Ladaria aliyeteuliwa mnamo mwaka wa 2018, kuwa Kadinali alihudumia kama Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa tangu  2017 hadi 2023. Kadinali mteule Victor Manuel Fernández wa La Plata, nchini Argentina, anaye mrithi Kadinali Ladaria mwenye umri wa miaka 79,  kama Mwenyekiti wa Baraza hilo  hivi karibuni atachukua madaraka katikati ya mwezi  Septemba 2023. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko amehitimisha ziara yake ya siku nne ya Kitume katika nchi ya Asia ya Mongolia  kwa kutembelea jumuiya ya  Wakatoliki yenye watu 1,500, wengi wao wakiwa wamejikita kukaa katika mji mkuu wa taifa hilo Ulaanbaatar. Ziara hiyo imekuwa ni ziara ya 43 ya kitume ya Papa kuwa Nje ya Nchi kwa kuzitembelea nchi 61 akiwa kama Papa.

05 September 2023, 20:51