Papa ametoa wito wa kujali maisha:hatuwezi kuzoea ajali kazini
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Papa Francisko, Jumatatu tarehe 11 Septemba 2023 amekutana wanachama wa kitaifa Ulemavu na walemavu kazini(ANMIL) ambapo katika hotuba yake, amewakaribisha katika fursa ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanza chama hicho. Papa amesema ilikuwa mnamo 1943, ambao ulikuwa ni mwaka wa maamuzi kwa Italia katika Vita vya Kidunia vya pili. Kwa hiyo walichukua hatua za kwanza katika muktadha huo, ambao Papa amesema unakumbusha kwamba kila mzozo wa kivita huleta pamoja na kundi kubwa la watu wenye ulemavu, hata leo hii; na kwamba idadi ya raia wanateseka na matokeo makubwa ya wenda wazimu ambayo ni vita. Mgogoro huo ukiisha, kifusi hubaki hata katika miili na mioyo, na amani lazima ijengwe siku baada ya siku, mwaka hadi mwaka, kwa kulinda na kukuza maisha na hadhi kuanzia wanyonge, kuanzia wale wasiojiweza zaidi. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu amependa kutoa shukrani za dhati kwa wote.
Awali ya yote kwa kile wanachoendelea kufanya kwa ajili ya ulinzi na uwakilishi wa wahanga wa ajali kazini, wajane na yatima wa waliofariki. Bado Papa alikuwa anakumbuka wale ndugu watano waliouawa na treni walipokuwa wakifanya kazi hivi karibuni. Amewashukuru kwa kuweka umakini wa hali ya juu ya suala la usalama mahali pa kazi, ambapo vifo na maafa mengi bado yanatokea. Aidha ameshukuru kwa juhudi wanazokuza ili kuboresha sheria za kiraia kuhusu ajali kazini na kuwajumuisha tena kitaaluma watu wanaopata walemavu. Kwa hakika, ni suala si tu la kuhakikisha ustawi sahihi na utunzaji wa hifadhi ya jamii kwa wale wanaoteseka na aina za ulemavu, lakini pia kutoa fursa mpya kwa watu ambao wanaweza kuunganishwa tena na ambao hadhi yao na utu unadai kutambuliwa kikamilifu. Hatimaye Papa ametoa shukrani kwa kazi yao ya kuhamasisha umma kuhusu sera za kuzuia ajali na usalama, hasa kwa wanawake na vijana. Mikasa na majanga mahali pa kazi kwa bahati mbaya havikomi, licha ya teknolojia zilizopo zakukuza maeneo salama na nyakati. Wakati
Papa amesema kuwa hii hutokea pale kazi inapokosa ubinadamu na, badala ya kuwa chombo ambacho binadamu hujitambua nacho kwa kujitolea kwa jamii, inakuwa mbio iliyokasirishwa ya kupata faida. Na hii ni mbaya. Mikasa huanza pale wakati lengo sio mwanadamu tena, lakini tija na mwanadamu anakuwa mashine ya uzalishaji. Kwa njia hiyo Papa amesema kazi za elimu na mafunzo zinazowangoja wao bado ni za msingi, kuhusu wafanyakazi na waajiri, na ndani ya jamii. Usalama mahali pa kazi ni kama hewa tunayovuta: tunatambua umuhimu wake pale tu inapokosekana kwa bahati mbaya, na huwa tumechelewa sana!” Baba Mtakatifu aidha amesema Mfano wa Msamaria Mwema (rej. Lk 10:30-37) unajirudia. Kwani wao wanakabiliwa na watu waliojeruhiwa na ambao wana hatari ya kuachwa kwenye njia ya maisha, kwa hiyo amewashauri kuwa wao wanaweza kuwa kinyume cha kutenda kama wale wahusika wawili wa kidini, kuhani na Mlawi ambao, hawakutaka kuchafua mikono yao na wakaendelea mbele bila kujali.
Na katika ulimwengu wa kazi wakati mwingine hufanyika kama hivyo: kuendelea, kana kwamba hakuna kitu kilichotokea, kwa kujitolea katika muungu wa soko. Lakini hatuwezi kuzoea ajali kazini, wala kujikabidhi kwa kutojali ajali. Hatuwezi kukubali upotevu wa maisha ya mwanadamu. Vifo na majeraha ni umaskini mbaya wa kijamii unaoathiri kila mtu, sio tu biashara au familia zinazohusika. Hatupaswi kuchoka kujifunza na kujifunza upya sanaa ya kujali, kwa jina la ubinadamu wa kawaida. Kiukweli, usalama hauhakikishiwa tu na sheria nzuri, ambayo lazima itekelezwe, lakini pia na uwezo wa kuishi kama kaka na dada mahali pa kazi. Mtume Paulo, akitafakari juu ya thamani ya ushirika, anauliza swali lifaalo sana: “Hamjui ya kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu? Mmeipokea kutoka kwa Mungu na si mali yenu wenyewe.” Na anamalizia kwa kusema: “Mtukuzeni Mungu katika miili yenu!” ( 1 Kor 6:19-20 ).
Baba Mtakatifu Francisko amefafanua kuwa Mtakatifu Paulo anarejea upendo, lakini tunaweza pia kupanua mtazamo wetu kwa ulimwengu wa kazi. Ikiwa mwili ni hekalu la Roho Mtakatifu, inamaanisha kwamba kwa kutunza udhaifu wake, tunamsifu Mungu. Kwa hiyo ubinadamu ni mahali pa ibada na uangalifu ni mtazamo ambao tunashirikiana nao katika kazi ya Muumba mwenyewe. Imani ya Kikristo inakwenda mbali hivyo kwani ukuu wa hadhi ni, kama hekalu la Roho Mtakatifu, ambalo halijui upotevu, halijui kununua, kuuza au kubadilishana maisha ya mwanadamu. Huwezi, kwa jina la faida kubwa, kuomba saa nyingi za kazi, kupunguza umakini, au kufikiria kuhesabu au fikiria kuhesabu mifumo ya bima au maombi ya usalama kama gharama zisizo na maana na hasara ya mapato.
Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa usalama kazini ni sehemu muhimu ya utunzaji wa kibinafsi. Hakika, kwa mwajiri, ni wajibu wa kwanza na aina ya kwanza ya wema. Hata hivyo, mitindo inayoendana kinyume na ambazo kwa neno zinaweza kuitwa kuwatunza zimeenea. Inatokea wakati wafanyabiashara au wabunge, badala ya kuwekeza katika usalama, wanapendelea kusafisha dhamiri zao na kazi fulani ya usaidizi. Ni mbaya. Kwa sababu wao wanaweka sura zao kwa umma kabla ya kila kitu kingine, kwa kujifanya wafadhili katika tamaduni au michezo, katika kazi nzuri, kwa kufanya kazi za sanaa au majengo ya ibada kupatikana, lakini bila kuzingatia ukweli kwamba, kama baba wa Kanisa na daktari wa Kanisa, Mtakatifu Ireneo asemavyo “utukufu wa Mungu ni mtu aliye hai
Hii ndiyo kazi ya kwanza ya kutunza kaka na dada, yaani mwili wa kaka na dada. Wajibu kwa wafanyakazi ni kipaumbele, kwani maisha hayawezi kuuzwa kwa sababu yoyote, hasa yakiwa ni duni, hatari na dhaifu. Sisi ni binadamu na si mashine, watu wa kipekee na si vipuri. Na mara nyingi waendeshaji wengine hutendewa kama vipuri. Kwa hilo Papa Francisko amependa kurudi tena shukrani zangu kwa kujitolea kwao na amewahimiza kusonga mbele, kusaidia jamii kupata maendeleo kutoka kwa mtazamo wa kiutamaduni, kuelewa kuwa wanadamu hutangulia masilahi ya kiuchumi, kwamba kila mtu ni zawadi kwa jamii na kwamba kulemaza hata mmoja wao huumiza mfumo mzima wa kijamii. Papa Francisko amewakabidhi kwa ulinzi wa Mtakatifu Joseph, mtakatifu msimamizi wa wafanyakazi wote. “Bwana awabariki na Mama yetu awalinde”. Lakini Pia wasisahau kusali kwa ajili yake maana anahitaji sala zao.