Tafuta

Jengo lilioungua moto katikati ya mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini. Jengo lilioungua moto katikati ya mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini.  (AFP or licensors)

Papa aombea makumi ya wahanga wa moto huko Johannesburg

Mwishoni mwa Katekesi ya Papa Francisko alionesha ukaribu wake kwa wale waliopoteza maisha katika moto ulioteketeza jengo katika jiji la Afrika Kusini Usiku wa tarehe 31 Agosti na watoto 12 pia walikufa.Maombi pia kwa ajili ya Ukraine ambayo inateseka sana, iliyokabidhiwa kwa Maria katika kuelekea sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bikira Maria.

Na Angella Rwezaula; - Vatican

Baba Mtakataifu Francisko ameonesha majonzi makubwa, mwishoni mwa Katekesi yake, Jumatano  tarehe 6 Septemba 2023 kutokana na moto  ambao  usiku wa Alhamisi tarehe 31 Agosti 2023  ulikumba jengo la gorofa tano katikati mwa jiji la Johannesburg, nchini Afrika Kusini, ambapo zaidi ya watu 70 walikufa, wakiwemo watoto kadhaa. Kwa upande wa Papa akiwageukia waamini na mahujaji waliokuwapo katika Katekesi hiyo kwenye Unwanja wa Mtakatifu Petro amesema “Ninawaalika kuungana nami katika kuwaombea waathirika” na ambapo alitoa rambirambi zake kwenye mazishi ya waathiriwa hao na kutuma baraka maalum kwao na kwa wale wanaofanya kila wawezalo kutoa huduma na msaada.

Moto huo umehusiana takribani familia mia mbili

Jengo hilo, linalomilikiwa na manispaa ya Jiji  lilikuwa limetelekezwa na mamlaka na kukodishwa kinyume cha sheria. Takriban familia 200 maskini ziliishi ndani yake ambazo hazikuweza kupata makao. Kulikuwa na watu wengi kiasi kwamba hata gereji ya chini ya ardhi ilichukuliwa na baadhi ya vibanda. Kulingana na maelezo ya baadhi ya mashahidi, baadhi ya watu walijirusha kutoka kwenye madirisha ya ghorofa za juu ili kuepuka moto huo. Mamlaka ya Afrika Kusini imefungua uchunguzi ili kubaini kilichotokea.

Watu sabini na sita pamoja na watoto kumi na wawili

Kwa mujibu wa takimu za nchi ni kwamba waathiriwa ni 76 wakiwemo watoto kumi na wawili. Na imekuwa vigumu kutambua baadhi ya miili kutokana na kuungua, huku takriban ya  majeruhi 90 wakiendelea kulazwa na kupatiwa matibabu hospitalini. Kulingana na mamlaka, wengi wa walioathiriwa na moto huo walikuwa wahamiaji kutoka Malawi na Tanzania. Mashirika yasiyo ya kiserikali yametayarisha baadhi ya makao ya muda kwa ajili ya walionusurika, huku baadhi ya harakati za kidini pia zikiwaamishia nje ya jengo hilo.

Kukabidhiwa kwa Maria wa Ukraine ambayo inateseka sana

Katika salamu zake kwa watu kwa lugha ya Kiitaliano,Papa  Fransisko kisha alikumbuka sikukuu ya kiliturujia ya Ijumaa 8 Septemba, Kuzaliwa kwa Bikira Maria. Kwa hiyo mwaliko wake ulikuwa  wa kuomba kutembea siku zote, kama Maria, katika njia za Bwana. Kwake, yeye mwanamke wa huruma tunakabidhi mateso na dhiki za Ukraine pendwa na inayoteswa, ambayo inateseka sana.” Alisisitiza Papa Francisko.

Katekesi ya Papa 6 Septemba 2023
Katekesi ya Papa 6 Septemba 2023

Kisha Papa aliwasalimu waamini wa Poland waliofika Roma kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 770 ya kutawazwa kwa Mtakatifu Stanislaus, Askofu, mfiadini na mlinzi wa Poland kuwa mtakatifu. Mchungaji shujaa na shupavu wa Krakow”, Francis alikumbuka, alikufa chini ya upanga wa mfalme mkuu wa Poland, akiwatetea watu wake na sheria ya Mungu. Kwa ujasiri mkuu na uhuru wa ndani, aliweka Kristo mbele ya vipaumbele vya ulimwengu. Mfano wake, ambao ni wa wakati ufaao kama zamani, alihitimisha, ukuhimize kuwa mwaminifu kwa Injili, ukiimwilisha katika familia yako na maisha ya kijamii. Hivyo mtaweza kuwa mashahidi wazi wa ukweli, haki na upendo wa kindugu”.

Tamko la  Tume ya Maaskofu wa Afrika Kusini

Kuhusiana na moto uliozuka katika mtaa wa Albert jijini Johannesburg, uliotokea usiku wa tarehe 31 Agosti 2023, hata Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Afrika Kusini walikuwa Mosi Septemba 2023, wametoa tamko lao kuhusiana na janga hilo kwamba  “Kifo cha watu 74 katika ajali ya moto katika mtaa wa 80 wa Albert mjini Johannesburg ni janga la kutisha. Idadi sawa na moto wa Grenfell Towers huko London mnamo 2017. Mioyo yetu ni ya kusikitisha waliopoteza maisha, walioathiriwa na moto, familia zao na wapendwa wao. Katika kushirikiana na mashirika mengine ya dini, tutajitahidi kutoa huduma ya kichungaji inayohitajika na msaada. Tumefurahishwa na kuhamasishwa na waliojibu kwanza waliofika kwenye eneo la moto ndani ya dakika chache, na tunatoa shukrani zetu nyingi kwao. Wahusika hasa wa mkasa huu ni wale watu duni wanaoteka majengo hayo na kuwanyonya watu wasio na makazi na maskini bila ya kujali, na kuwalazimisha kuishi katika mazingira ya kinyama na hatari huku wakiwatozwa kodi kwa ajili yamapendeleo" ya kuishi katika mitego hiyo ya kifo.”

Baada ya katekesi 6 Septemba 2023

 

06 September 2023, 16:40